Swahili
- Ukurasa Kuu    - Kumi Juu    - Mada Mpya    - Salimisha Habari    - Tafuta    - Kiswahili Jukwaa    - Kiswahili Wanachama    - Tathmini    - Ujumbe wa Kibinafsi    - Tafiti    - Majarida    - Hadithi Archive    - Maudhui    - Viungo vya Wavuti    - Vipakuliwa    - Maswali ya Kawaida    - Tunapendekeze    - Orodha ya Kuingia   
 


Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njem
 
Mkuu - teknolojia na taaluma  Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njema Baada kukumbushana maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Aayah tukufu iliyotaja sifa kumi njema, tumeona kwamba mwisho kabisa Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema: ((أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا)) ((Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Hazab:35] Vile vile Anasema katika Aayah nyingine: ((وَعَدَ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ)) ((Allah Amewaahidi waliomuamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfira na malipo makubwa)) [Al-Maaidah]
Maana kwamba; Tutasamehewa Madhambi yetu ambayo hakuna aliyeepukana nayo, lakini Mola wetu ni Mkarimu Mwingi Wa Kurehemu na Mwingi wa Msamaha Hukubali toba zetu wakati wowote kama Anavyotuahidi katika Qur-aan na pia katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

((وَهُوَ الَّذِي يَقْبَلُ التَّوْبَةَ عَنْ عِبَادِهِ وَيَعْفُو عَنِ السَّيِّئَاتِ))

((Naye Ndiye Anayepokea toba kwa waja wake, na Anasamehe makosa)) [Ash-Shuura 25]

((وَمَن يَعْمَلْ سُوءًا أَوْ يَظْلِمْ نَفْسَهُ ثُمَّ يَسْتَغْفِرِ اللّهَ يَجِدِ اللّهَ غَفُورًا رَّحِيمًا)) 

((Na anayetenda uovu au akajidhulumu nafsi yake, kisha akaomba maghfira kwa Allah, Atamkuta Allah ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu)) [An-Nisaa: 110]

((وَإِنِّي لَغَفَّارٌ لِّمَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا ثُمَّ اهْتَدَى))

((Na hakika Mimi ni Mwingi wa Kusamehe kwa anayetubia, na akaamini, na akatenda mema, tena akaongoka)) [Twaaha:82] Hadiyth ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

عن أنس رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((قال الله: يا ابن آدم إنك ما دعوتني ورجوتني غفرت لك على ما كان منك ولا أبالي، يا ابن آدم لو بلغت ذنوبك عنان السماء، ثم استغفرتني غفرت لك ولا أبالي، يا ابن آدم إنك لو أتيتني بقراب الأرض خطايا، ثم لقيتني لا تشرك بي شيئاً لأتيتك بقرابها مغفرة)) أخرجه الترمذي وحسنه الألباني في الصحيحة

Imetoka kwa Anas (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: ((Amesema Allahِ: Ee Mwana Adam! Hakika ukiniomba na ukanitaraji (kwa malipo) Nitakusamehe yale yote uliyonayo na wala Sijali, Ee Mwana Adam! Lau zingefikia dhambi zako ukubwa wa mbingu, kisha ukaniomba maghfira, Ningekughufuria bila ya kujali (kiasi cha madhambi uliyoyafanya). Ee Mwana Adam, Hakika ungenijia na madhambi yakaribiayo ukubwa wa ardhi, kisha ukakutana nami na hali hukunishirikisha chochote, basi Nami Nitakujia na msamaha unaolingana nao)) [Imetolewa na At-Tirmidhy na Shaykh Al-Albaaniy kasema daraja yake ni Hasan]Vile vile tutalipwa Pepo kutokana na Rahma Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa waja Wake. Na tumetambua kwamba Pepo hawezi kuipata Muislamu bila ya kuifanyia kazi. Kazi kama hiyo ya kujitahidi kuchuma sifa kama hizo kumi ambazo zinahitaji maazimio madhubuti, jitihada na subira, mapenzi ya kuyatenda na matumaini ya kutakabaliwa na kulipwa malipo bora kabisa ambayo ni neema kubwa kwetu. Ndio maana Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

((وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَنُبَوِّئَنَّهُم مِّنَ الْجَنَّةِ غُرَفًا تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ) ((الَّذِينَ صَبَرُوا وَعَلَى رَبِّهِمْ يَتَوَكَّلُون)) 

((Na ambao wameamini na wakatenda mema, bila ya shaka Tutawaweka katika maghorofa ya Peponi yenye kupitiwa chini yake mito, wakidumu humo. Ni ujira mwema ulioje huo wa watendao)) 

((Ambao walisubiri, na wakamtegemea Mola wao Mlezi)) [Al-'Ankabuut:58-59)

Pepo hiyo ambayo sote tunaitamani kuingia na kuishi humu milele imesimuliwa katika Aayah nyingi za Qur-aan, neema na raha zake. Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pia ametuelezea mengi kuhusu uzuri wa Pepo hiyo. Kwa uchache tutaja hapa baadhi ya Aayah na Hadiyth hizo ili tupate matumaini zaidi katika nyoyo zetu na kuzidi kujitahidi kuifanyia kazi:

إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي ظِلَالٍ وَعُيُونٍ ﴿41﴾ وَفَوَاكِهَ مِمَّا يَشْتَهُونَ ﴿42﴾ كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ ﴿43﴾ إِنَّا كَذَلِكَ نَجْزِي الْمُحْسِنينَ ﴿44﴾


41. Hakika wacha Mungu watakuwa katika vivuli na chemchem 

42. Na matunda wanayoyapenda 

43. Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyokuwa mkiyatenda. 

44. Hakika ndio kama hivyo tunavyowalipa watendao mema. 

[Al-Mursalaat:41-44]

أُوْلَئِكَ لَهُمْ رِزْقٌ مَّعْلُومٌ ﴿41﴾ فَوَاكِهُ وَهُم مُّكْرَمُونَ ﴿42﴾ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ ﴿43﴾ عَلَى سُرُرٍ مُّتَقَابِلِينَ ﴿44﴾ يُطَافُ عَلَيْهِم بِكَأْسٍ مِن مَّعِينٍ ﴿45﴾ بَيْضَاء لَذَّةٍ لِّلشَّارِبِينَ ﴿46﴾ لَا فِيهَا غَوْلٌ وَلَا هُمْ عَنْهَا يُنزَفُونَ ﴿47﴾ وَعِنْدَهُمْ قَاصِرَاتُ الطَّرْفِ عِينٌ ﴿48﴾ كَأَنَّهُنَّ بَيْضٌ مَّكْنُونٌ ﴿49﴾

41. Hao ndio watakaopata riziki maalumu, 

42. Matunda, nao watahishimiwa 

43. Katika Bustani za neema 

44. Wako juu ya viti wamekabiliana. 

45.Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem 

46. Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao 

47. Hakina madhara, wala hakiwaleweshi 

48. Na watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri. 

49. Hao wanawake kama mayai yaliyohifadhika. 

[Asw-Swaafaat:41-48]

Hiyo ni ahadi ya kutoka kwa Mola wetu Mtukufu ambayo hakika Yeye Haivunji:

((لَكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ غُرَفٌ مِّن فَوْقِهَا غُرَفٌ مَّبْنِيَّةٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَعْدَ اللَّهِ لَا يُخْلِفُ اللَّهُ الْمِيعَادَ))

((Lakini waliomcha Mola wao Mlezi watapata ghorofa zilizojengwa juu ya ghorofa; chini yake hupita mito. Ndiyo ahadi ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu Havunji ahadi Yake [Az-Zumar: 20]

Kisa Cha Swahaba 'Amru bin Jamuuh aliyetamani Pepo:'Amru bin Jamuuh (Radhiya Allaahu 'anhu) alikuwa kilema. Alikuwa na watoto wa kiume wanne ambao daima walikuwa wakihudhuria vita mbali mbali. Ulipofika wakati wa vita vya Uhud, 'Amru (Radhiya Allaahu 'anhu) alitamani kupigana vita hivyo lakini watu walimzuia kwa vile ni kilema wakimwambia: "Wewe umeruhusiwa kutokupigana vita kutokana na hali yako, kwa hiyo huna haja ya kwenda vitani". Lakini yeye akawajibu: "Inasikitisha kuwa watoto wangu wapate Pepo nami nisiipate". Mke wake pia alitaka sana mumewe apate fadhila ya kuwa shahidi wa vita. Hivyo akamshikilia aende hivyo hivyo japokuwa hali yake ni kilema, akimwambia: "Sioni kama udhuru huo wako utakuzuia kwenda kupigana vita, ila labda naona kama una khofu tu ya kwenda vitani". Aliposikia hivyo 'Amru (Radhiya Allaahu 'anhu) alijitayarisha kwenda vitani akaelekea Qiblah na kuomba: "Ewe Allah Usinirudishe kwa familia yangu tena".

Imesemekana kwamba alikwenda vitani na alionekana akipigana na huku akisema kwa fakhari: "Naapa kwa Allah, hakika mimi naitamani Pepo". Mtoto wake alikuwa akimfuatilia nyuma yake wakipigana hadi wote wakauliwa". Mke wake aliposikia kuwa mumewe na mtoto wake wamefariki, alituma ngamia ili wachukuliwe miili yao. Imesemekana kwamba miili yao ilipopandishwa juu ya ngamia na kuondoka, ngamia huyo aligoma kusimama. Alipolazimisha kusimama aligoma kuelekea Madiynah bali alirudia kuelekea jabali la Uhud. Mkewe alipoulizwa kuhusu hilo, akasema kuwa 'Amru (Radhiya Allahu 'anhu) aliomba Du'aa kuwa asirudishwe kwetu tena. Na ndio ikawa sababu ya kugoma ngamia kurudi Madiynah.

 Posted By Posted juu ya Saturday, March 09 @ 16:58:54 PST na MediaSwahiliTeam
 

Comments 💬 التعليقات
 

For Your Membership Comments And Registered Debates Please, See Below Or Register Here :-: للحصول على تعليقات عضويتك و مناقشات الأعضاء انظر من فضلك أدناه أو سجّل هنا


Kifungu Rating

Wastani matokeo: 0
Kura: 0

Tafadhali chukua ya pili na kupiga kura kwa ajili ya makala hii:

bora
Vizuri Sana
Mema
Kawaidar
Mbaya


Chaguzi


 Chapa Rafiki Chapa Rafiki





Mada zinazohusiana

Mkuu - teknolojia na taaluma

 

Ẹsin Islam الدين الإسلامي Religion of Islam Addinin Musulunci Agama Islam Religión del Islam 伊斯兰教 Dini ya Kiislamu Религия Ислам Religião do Islã イスラム教 Esin Islam 이슬람의 종교 Portal African Muslim Website - Arabic English African Islamic Website For World News, Fatwas, Audios, Videos, Muslim News, Articles, Radio, Audio, Video, Quran, Hadith, TV Channels, Fatwas, Muslim News, Newspapers, Magazines Headlines, Forums, College, Schools, Universities, Mosques, Quranic, Sunnah, Fiqh, Prayers, Salat, Ramadan, Vidoes, Books, Fasting, PDFs On EsinIslam.Com And IslamAfrica.Com