1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الر ۚ تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْحَكِيمِ
Alif-lam-ra tilka ayatualkitabi alhakeem
Swahili
Alif Lam Ra. Hizo ni Aya za Kitabu chenye Hikima.
|
Ayah 10:2 الأية
أَكَانَ لِلنَّاسِ عَجَبًا أَنْ أَوْحَيْنَا إِلَىٰ رَجُلٍ مِّنْهُمْ أَنْ أَنذِرِ
النَّاسَ وَبَشِّرِ الَّذِينَ آمَنُوا أَنَّ لَهُمْ قَدَمَ صِدْقٍ عِندَ رَبِّهِمْ
ۗ قَالَ الْكَافِرُونَ إِنَّ هَٰذَا لَسَاحِرٌ مُّبِينٌ
Akana linnasi AAajabanan awhayna ila rajulin minhum an anthiriannasa wabashshiri
allatheena amanooanna lahum qadama sidqin AAinda rabbihim qala alkafiroonainna
hatha lasahirun mubeen
Swahili
Je! Imekuwa ajabu kwa watu kwamba tumemfunulia mmoja wao kuwa: Waonye watu, na
wabashirie wale walio amini ya kuwa watakuwa na cheo cha juu kwa Mola wao Mlezi?
Wakasema makafiri: Hakika huyu ni mchawi dhaahiri!
|
Ayah 10:3 الأية
إِنَّ رَبَّكُمُ اللهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ
أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ
إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا
تَذَكَّرُونَ
Inna rabbakumu Allahu allatheekhalaqa assamawati wal-ardafee sittati ayyamin
thumma istawa AAalaalAAarshi yudabbiru al-amra ma min shafeeAAin illamin baAAdi
ithnihi thalikumu Allahu rabbukumfaAAbudoohu afala tathakkaroon
Swahili
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenyezi Mungu, ambaye ameziumba mbingu na ardhi kwa
siku sita, na ametawala kwenye ufalme wake, anaendesha mambo yote. Hapana
mwombezi ila baada ya idhini yake. Huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola wenu Mlezi.
Basi muabuduni Yeye. Je! Hamkumbuki?
|
Ayah 10:4 الأية
إِلَيْهِ مَرْجِعُكُمْ جَمِيعًا ۖ وَعْدَ اللهِ حَقًّا ۚ إِنَّهُ يَبْدَأُ
الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ لِيَجْزِيَ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ
بِالْقِسْطِ ۚ وَالَّذِينَ كَفَرُوا لَهُمْ شَرَابٌ مِّنْ حَمِيمٍ وَعَذَابٌ
أَلِيمٌ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ
Ilayhi marjiAAukum jameeAAan waAAda Allahihaqqan innahu yabdao alkhalqa thumma
yuAAeeduhu liyajziyaallatheena amanoo waAAamiloo assalihatibilqisti wallatheena
kafaroo lahumsharabun min hameemin waAAathabun aleemunbima kanoo yakfuroon
Swahili
Kwake Yeye tu ndio marejeo yenu nyote. Hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu iliyo ya
kweli. Hakika Yeye ndiye aliye anzisha uumbaji, na kisha ataurejesha ili awalipe
kwa uadilifu wale walio amini na wakatenda mema. Na walio kufuru, wao watapata
vinywaji vinavyo chemka, na adhabu chungu kwa sababu ya walivyo kuwa wakikufuru.
|
Ayah 10:5 الأية
هُوَ الَّذِي جَعَلَ الشَّمْسَ ضِيَاءً وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ
لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ ۚ مَا خَلَقَ اللهُ ذَٰلِكَ إِلَّا
بِالْحَقِّ ۚ يُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ
Huwa allathee jaAAala ashshamsadiyaan walqamara nooran waqaddarahu
manazilalitaAAlamoo AAadada assineena walhisabama khalaqa Allahu thalika illa
bilhaqqiyufassilu al-ayati liqawmin yaAAlamoon
Swahili
Yeye ndiye aliye lijaalia jua kuwa na mwangaza, na mwezi ukawa na nuru, na
akaupimia vituo ili mjue idadi ya miaka na hisabu. Mwenyezi Mungu hakuviumba
hivyo ila kwa Haki. Anazipambanua Ishara kwa watu wanao jua.
|
Ayah 10:6 الأية
إِنَّ فِي اخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ وَمَا خَلَقَ اللهُ فِي
السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَتَّقُونَ
Inna fee ikhtilafi allayli wannahariwama khalaqa Allahu fee assamawatiwal-ardi
laayatin liqawmin yattaqoon
Swahili
Hakika katika kukhitalifiana usiku na mchana, na katika alivyo umba Mwenyezi
Mungu katika mbingu na ardhi, zipo Ishara kwa watu wanao mcha-Mngu.
|
Ayah 10:7 الأية
إِنَّ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا وَرَضُوا بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا
وَاطْمَأَنُّوا بِهَا وَالَّذِينَ هُمْ عَنْ آيَاتِنَا غَافِلُونَ
Inna allatheena la yarjoona liqaanawaradoo bilhayati addunyawatmaannoo biha
wallatheenahum AAan ayatina ghafiloon
Swahili
Hakika wasio taraji kukutana nasi, na wakaridhia maisha ya dunia na wakatua
nayo, na walio ghafilika na Ishara zetu,
|
Ayah 10:8 الأية
أُولَٰئِكَ مَأْوَاهُمُ النَّارُ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ
Ola-ika ma/wahumu annarubima kanoo yaksiboon
Swahili
Hao, makaazi yao ni Motoni kwa sababu ya waliyo kuwa wakiyachuma.
|
Ayah 10:9 الأية
إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ يَهْدِيهِمْ رَبُّهُم
بِإِيمَانِهِمْ ۖ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ فِي جَنَّاتِ النَّعِيمِ
Inna allatheena amanoowaAAamiloo assalihati yahdeehim rabbuhumbi-eemanihim
tajree min tahtihimu al-anharufee jannati annaAAeem
Swahili
Hakika walio amini na wakatenda mema, Mola wao Mlezi atawaongoa kwa sababu ya
Imani yao. Itakuwa inapita mito kati yao katika Mabustani yenye neema.
|
Ayah 10:10 الأية
دَعْوَاهُمْ فِيهَا سُبْحَانَكَ اللهُمَّ وَتَحِيَّتُهُمْ فِيهَا سَلَامٌ ۚ
وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ
DaAAwahum feeha subhanakaallahumma watahiyyatuhum feeha salamunwaakhiru
daAAwahum ani alhamdu lillahirabbi alAAalameen
Swahili
Wito wao humo utakuwa: Subhanaka Llahumma "Umetakasika Ee Mwenyezi Mungu!" Na
maamkio yao humo ni "Salama". Na mwisho wa wito wao ni: Alhamdulillahi Rabbil
A'lamiin "Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote."
|
Ayah 10:11 الأية
وَلَوْ يُعَجِّلُ اللهُ لِلنَّاسِ الشَّرَّ اسْتِعْجَالَهُم بِالْخَيْرِ لَقُضِيَ
إِلَيْهِمْ أَجَلُهُمْ ۖ فَنَذَرُ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا فِي
طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ
Walaw yuAAajjilu Allahu linnasiashsharra istiAAjalahum bilkhayri laqudiyailayhim
ajaluhum fanatharu allatheena layarjoona liqaana fee tughyanihimyaAAmahoon
Swahili
Na lau kama Mwenyezi Mungu angeli wafanyia watu haraka kuwaletea shari kama
wanavyo jihimizia kuletewa kheri, bila ya shaka wangelisha timiziwa ajali yao.
Lakini tunawaacha wale wasio tumainia kukutana nasi wakihangaika katika upotovu
wao.
|
Ayah 10:12 الأية
وَإِذَا مَسَّ الْإِنسَانَ الضُّرُّ دَعَانَا لِجَنبِهِ أَوْ قَاعِدًا أَوْ
قَائِمًا فَلَمَّا كَشَفْنَا عَنْهُ ضُرَّهُ مَرَّ كَأَن لَّمْ يَدْعُنَا إِلَىٰ
ضُرٍّ مَّسَّهُ ۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلْمُسْرِفِينَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Wa-itha massa al-insana addurrudaAAana lijanbihi aw qaAAidan aw qa-imanfalamma
kashafna AAanhu durrahu marra kaanlam yadAAuna ila durrin massahu
kathalikazuyyina lilmusrifeena ma kanoo yaAAmaloon
Swahili
Na mtu akiguswa na shida hutuomba naye kaegesha ubavu, au kakaa, au kasimama.
Lakini tukimwondoshea shida yake huendelea kama kwamba hakupata kutuomba
tumwondoshee shida iliyo mpata. Ndio namna hiyo wamepambiwa warukao mipaka yale
waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 10:13 الأية
وَلَقَدْ أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ مِن قَبْلِكُمْ لَمَّا ظَلَمُوا ۙ وَجَاءَتْهُمْ
رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ وَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي
الْقَوْمَ الْمُجْرِمِينَ
Walaqad ahlakna alquroona minqablikum lamma thalamoo wajaat-humrusuluhum
bilbayyinati wama kanooliyu/minoo kathalika najzee alqawma almujrimeen
Swahili
Na kwa yakini tumekwisha ziangamiza kaumu za kabla yenu walipo dhulumu, na
waliwajia Mitume wao kwa Ishara zilizo wazi; lakini hawakuwa wenye kuamini. Ndio
kama hivyo tunavyo walipa watu wakosefu.
|
Ayah 10:14 الأية
ثُمَّ جَعَلْنَاكُمْ خَلَائِفَ فِي الْأَرْضِ مِن بَعْدِهِمْ لِنَنظُرَ كَيْفَ
تَعْمَلُونَ
Thumma jaAAalnakum khala-ifafee al-ardi min baAAdihim linanthura kayfataAAmaloon
Swahili
Kisha tukakufanyeni nyiye ndio wenye kushika mahala pao baada yao katika ardhi
ili tuone jinsi mtakavyo tenda.
|
Ayah 10:15 الأية
وَإِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ آيَاتُنَا بَيِّنَاتٍ ۙ قَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ
لِقَاءَنَا ائْتِ بِقُرْآنٍ غَيْرِ هَٰذَا أَوْ بَدِّلْهُ ۚ قُلْ مَا يَكُونُ لِي
أَنْ أُبَدِّلَهُ مِن تِلْقَاءِ نَفْسِي ۖ إِنْ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰ
إِلَيَّ ۖ إِنِّي أَخَافُ إِنْ عَصَيْتُ رَبِّي عَذَابَ يَوْمٍ عَظِيمٍ
Wa-itha tutla AAalayhim ayatunabayyinatin qala allatheena layarjoona liqaana
i/ti biqur-anin ghayri hathaaw baddilhu qul ma yakoonu lee an obaddilahu min
tilqa-inafsee in attabiAAu illa ma yooha ilayyainnee akhafu in AAasaytu rabbee
AAathabayawmin AAatheem
Swahili
Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasio taraji kukutana na Sisi
husema: Lete Qur'ani isiyo kuwa hii, au ibadilishe. Sema: Hainifalii mimi
kuibadilisha kwa nitakavyo nafsi yangu. Mimi sifuati ila ninayo funuliwa kwa
Wahyi. Hakika mimi naogopa, nikimuasi Mola wangu Mlezi, adhabu ya Siku iliyo
kuu.
|
Ayah 10:16 الأية
قُل لَّوْ شَاءَ اللهُ مَا تَلَوْتُهُ عَلَيْكُمْ وَلَا أَدْرَاكُم بِهِ ۖ فَقَدْ
لَبِثْتُ فِيكُمْ عُمُرًا مِّن قَبْلِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Qul law shaa Allahu matalawtuhu AAalaykum wala adrakum bihi faqadlabithtu feekum
AAumuran min qablihi afala taAAqiloon
Swahili
Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni.
Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii?
|
Ayah 10:17 الأية
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ
ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْمُجْرِمُونَ
Faman athlamu mimmani iftaraAAala Allahi kathiban aw kaththababi-ayatihi innahu
la yuflihualmujrimoon
Swahili
Basi ni nani aliye dhaalimu zaidi kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu
na akazikanusha Ishara zake? Hakika hawafanikiwi wakosefu.
|
Ayah 10:18 الأية
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ مَا لَا يَضُرُّهُمْ وَلَا يَنفَعُهُمْ
وَيَقُولُونَ هَٰؤُلَاءِ شُفَعَاؤُنَا عِندَ اللهِ ۚ قُلْ أَتُنَبِّئُونَ اللهَ
بِمَا لَا يَعْلَمُ فِي السَّمَاوَاتِ وَلَا فِي الْأَرْضِ ۚ سُبْحَانَهُ
وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
WayaAAbudoona min dooni Allahi mala yadurruhum wala yanfaAAuhum
wayaqooloonahaola-i shufaAAaona AAinda Allahiqul atunabbi-oona Allaha bima la
yaAAlamufee assamawati wala fee al-ardisubhanahu wataAAala AAamma yushrikoon
Swahili
Nao, badala ya Mwenyezi Mungu, wanaabudu wasio wadhuru wala kuwanufaisha, na
wanasema: Hawa ndio waombezi wetu kwa Mwenyezi Mungu! Sema: Je! Mnamwambia
Mwenyezi Mungu asiyo yajua ya katika mbingu wala katika ardhi? Subhanahu wa
Taa'la! Ametakasika na ametukuka na hao wanao mshirikisha naye.
|
Ayah 10:19 الأية
وَمَا كَانَ النَّاسُ إِلَّا أُمَّةً وَاحِدَةً فَاخْتَلَفُوا ۚ وَلَوْلَا كَلِمَةٌ
سَبَقَتْ مِن رَّبِّكَ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ فِيمَا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Wama kana annasuilla ommatan wahidatan fakhtalafoo walawlakalimatun sabaqat min
rabbika laqudiya baynahum feemafeehi yakhtalifoon
Swahili
Wala watu hawakuwa ila Umma mmoja tu. Kisha wakakhitalifiana. Na lau kuwa si
neno lililo kwisha tangulia kutokana na Mola wako Mlezi, hapana shaka hukumu
ingeli kwisha katwa baina yao katika hayo wanayo khitalifiana.
|
Ayah 10:20 الأية
وَيَقُولُونَ لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْهِ آيَةٌ مِّن رَّبِّهِ ۖ فَقُلْ إِنَّمَا
الْغَيْبُ لِلَّهِ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ
Wayaqooloona lawla onzila AAalayhi ayatunmin rabbihi faqul innama alghaybu
lillahi fantathirooinnee maAAakum mina almuntathireen
Swahili
Na wanasema: Kwa nini hakuteremshiwa Ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema:
Mambo ya ghaibu ni ya Mwenyezi Mungu. Basi nyinyi ngojeni, na mimi ni pamoja
nanyi katika wanao ngojea.
|
Ayah 10:21 الأية
وَإِذَا أَذَقْنَا النَّاسَ رَحْمَةً مِّن بَعْدِ ضَرَّاءَ مَسَّتْهُمْ إِذَا لَهُم
مَّكْرٌ فِي آيَاتِنَا ۚ قُلِ اللهُ أَسْرَعُ مَكْرًا ۚ إِنَّ رُسُلَنَا
يَكْتُبُونَ مَا تَمْكُرُونَ
Wa-itha athaqna annasarahmatan min baAAdi darraa massat-hum ithalahum makrun fee
ayatina quli AllahuasraAAu makran inna rusulana yaktuboona matamkuroon
Swahili
Na tunapo waonjesha watu rehema baada ya shida waliyo ipata, utawaona wana
vitimbi kuzipangia Ishara zetu. Sema: Mwenyezi Mungu ni Mwepesi zaidi wa
kupanga. Hakika wajumbe wetu wanayaandika mnayo yapanga.
|
Ayah 10:22 الأية
هُوَ الَّذِي يُسَيِّرُكُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا كُنتُمْ فِي
الْفُلْكِ وَجَرَيْنَ بِهِم بِرِيحٍ طَيِّبَةٍ وَفَرِحُوا بِهَا جَاءَتْهَا رِيحٌ
عَاصِفٌ وَجَاءَهُمُ الْمَوْجُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَظَنُّوا أَنَّهُمْ أُحِيطَ
بِهِمْ ۙ دَعَوُا اللهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ لَئِنْ أَنجَيْتَنَا مِنْ
هَٰذِهِ لَنَكُونَنَّ مِنَ الشَّاكِرِينَ
Huwa allathee yusayyirukum feealbarri walbahri hatta ithakuntum fee alfulki
wajarayna bihim bireehin tayyibatinwafarihoo biha jaat-ha reehunAAasifun
wajaahumu almawju min kulli makaninwathannoo annahum oheeta bihimdaAAawoo Allaha
mukhliseena lahu addeenala-in anjaytana min hathihi lanakoonanna mina
ashshakireen
Swahili
Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na
yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na
yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wamesha zongwa, basi hapo
humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: Ukituokoa na haya bila ya shaka
tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru.
|
Ayah 10:23 الأية
فَلَمَّا أَنجَاهُمْ إِذَا هُمْ يَبْغُونَ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ ۗ يَا
أَيُّهَا النَّاسُ إِنَّمَا بَغْيُكُمْ عَلَىٰ أَنفُسِكُم ۖ مَّتَاعَ الْحَيَاةِ
الدُّنْيَا ۖ ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُكُمْ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ
تَعْمَلُونَ
Falamma anjahum ithahum yabghoona fee al-ardi bighayri alhaqqi yaayyuha annasu
innama baghyukum AAalaanfusikum mataAAa alhayati addunyathumma ilayna
marjiAAukum fanunabbi-okum bimakuntum taAAmaloon
Swahili
Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki. Enyi
watu! Jeuri zenu zitakudhuruni wenyewe. Hii ni starehe ya maisha ya dunia tu.
Kisha marejeo yenu ni kwetu, na hapo tutakuambieni mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 10:24 الأية
إِنَّمَا مَثَلُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَاءٍ أَنزَلْنَاهُ مِنَ السَّمَاءِ
فَاخْتَلَطَ بِهِ نَبَاتُ الْأَرْضِ مِمَّا يَأْكُلُ النَّاسُ وَالْأَنْعَامُ
حَتَّىٰ إِذَا أَخَذَتِ الْأَرْضُ زُخْرُفَهَا وَازَّيَّنَتْ وَظَنَّ أَهْلُهَا
أَنَّهُمْ قَادِرُونَ عَلَيْهَا أَتَاهَا أَمْرُنَا لَيْلًا أَوْ نَهَارًا
فَجَعَلْنَاهَا حَصِيدًا كَأَن لَّمْ تَغْنَ بِالْأَمْسِ ۚ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ
الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ
Innama mathalu alhayatiaddunya kama-in anzalnahu mina assama-ifakhtalata bihi
nabatu al-ardi mimmaya/kulu annasu wal-anAAamu hattaitha akhathati al-ardu
zukhrufaha wazzayyanatwathanna ahluha annahum qadiroonaAAalayha ataha amruna
laylan aw naharanfajaAAalnaha haseedan kaan lam taghnabil-amsi kathalika
nufassilu al-ayatiliqawmin yatafakkaroon
Swahili
Hakika mfano wa maisha ya dunia ni kama maji tuliyo yateremsha kutoka mbinguni,
kisha yakachanganyika na mimea ya ardhi wanayo ila watu na wanyama. Mpaka ardhi
ilipo kamilika uzuri wake, na ikapambika, na wenyewe wakadhani wamesha iweza,
iliifikia amri yetu usiku au mchana, tukaifanya kama iliyo fyekwa - kama kwamba
haikuwapo jana. Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.
|
Ayah 10:25 الأية
وَاللهُ يَدْعُو إِلَىٰ دَارِ السَّلَامِ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ إِلَىٰ صِرَاطٍ
مُّسْتَقِيمٍ
Wallahu yadAAoo ila dariassalami wayahdee man yashao ila siratinmustaqeem
Swahili
Na Mwenyezi Mungu anaita kwendea Nyumba ya Amani, na anamwongoa amtakaye kwenye
Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 10:26 الأية
لِّلَّذِينَ أَحْسَنُوا الْحُسْنَىٰ وَزِيَادَةٌ ۖ وَلَا يَرْهَقُ وُجُوهَهُمْ
قَتَرٌ وَلَا ذِلَّةٌ ۚ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Lillatheena ahsanoo alhusnawaziyadatun wala yarhaqu wujoohahum qatarun
walathillatun ola-ika as-habu aljannatihum feeha khalidoon
Swahili
Kwa wafanyao wema ni wema na zaidi. Wala vumbi halitawafunika nyuso zao, wala
madhila. Hao ndio watu wa Peponi. Humo watadumu.
|
Ayah 10:27 الأية
وَالَّذِينَ كَسَبُوا السَّيِّئَاتِ جَزَاءُ سَيِّئَةٍ بِمِثْلِهَا وَتَرْهَقُهُمْ
ذِلَّةٌ ۖ مَّا لَهُم مِّنَ اللهِ مِنْ عَاصِمٍ ۖ كَأَنَّمَا أُغْشِيَتْ
وُجُوهُهُمْ قِطَعًا مِّنَ اللَّيْلِ مُظْلِمًا ۚ أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ
هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Wallatheena kasaboo assayyi-atijazao sayyi-atin bimithliha watarhaquhum
thillatunma lahum mina Allahi min AAasimin kaannamaoghshiyat wujoohuhum qitaAAan
mina allayli muthlimanola-ika as-habu annari humfeeha khalidoon
Swahili
Na wale walio chuma maovu, malipo ya uovu ni mfano wake vile vile, na yatawafika
madhila. Hawatakuwa na wa kuwalinda na Mwenyezi Mungu. Nyuso zao kama kwamba
zimefunikwa na vipande vya usiku wa giza. Hao ndio watu wa Motoni, wao humo
watadumu.
|
Ayah 10:28 الأية
وَيَوْمَ نَحْشُرُهُمْ جَمِيعًا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشْرَكُوا مَكَانَكُمْ
أَنتُمْ وَشُرَكَاؤُكُمْ ۚ فَزَيَّلْنَا بَيْنَهُمْ ۖ وَقَالَ شُرَكَاؤُهُم مَّا
كُنتُمْ إِيَّانَا تَعْبُدُونَ
Wayawma nahshuruhum jameeAAan thummanaqoolu lillatheena ashrakoo makanakum
antumwashurakaokum fazayyalna baynahum waqalashurakaohum ma kuntum
iyyanataAAbudoon
Swahili
Na siku tutakapo wakusanya wote, kisha tutawaambia walio shirikisha: Simameni
mahali penu nyinyi na wale mlio wafanya washirika. Kisha tutawatenga baina yao.
Na hao walio washirikisha watasema: Nyinyi hamkuwa mkituabudu sisi.
|
Ayah 10:29 الأية
فَكَفَىٰ بِاللهِ شَهِيدًا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ إِن كُنَّا عَنْ عِبَادَتِكُمْ
لَغَافِلِينَ
Fakafa billahishaheedan baynana wabaynakum in kunna AAan AAibadatikumlaghafileen
Swahili
Mwenyezi Mungu anatosha kuwa ni shahidi baina yetu na nyinyi. Hakika sisi
tulikuwa hatuna khabari ya ibada yenu.
|
Ayah 10:30 الأية
هُنَالِكَ تَبْلُو كُلُّ نَفْسٍ مَّا أَسْلَفَتْ ۚ وَرُدُّوا إِلَى اللهِ
مَوْلَاهُمُ الْحَقِّ ۖ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ
Hunalika tabloo kullu nafsin maaslafat waruddoo ila Allahi mawlahumu
alhaqqiwadalla AAanhum ma kanoo yaftaroon
Swahili
Huko kila mtu atayajua aliyo yatanguliza. Na watarudishwa kwa Mwenyezi Mungu,
Mola wao wa Haki, na yote waliyo kuwa wakiyazua yatawapotea.
|
Ayah 10:31 الأية
قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ
وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ
مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللهُ ۚ فَقُلْ
أَفَلَا تَتَّقُونَ
Qul man yarzuqukum mina assama-iwal-ardi amman yamliku assamAAa wal-absarawaman
yukhriju alhayya mina almayyiti wayukhriju almayyitamina alhayyi waman yudabbiru
al-amra fasayaqooloona Allahufaqul afala tattaqoon
Swahili
Sema: Ni nani anaye kuruzukuni kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Au ni nani anaye
miliki kusikia na kuona? Na nani amtoaye hai kutoka maiti, na akamtoa maiti
kutoka aliye hai? Na nani anaye yadabiri mambo yote? Watasema: Allah, Mwenyezi
Mungu. Basi sema: Je! Hamchi?
|
Ayah 10:32 الأية
فَذَٰلِكُمُ اللهُ رَبُّكُمُ الْحَقُّ ۖ فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا
الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ
Fathalikumu Allahu rabbukumualhaqqu famatha baAAda alhaqqi illa addalalufaanna
tusrafoon
Swahili
Basi huyo ndiye Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wenu wa haki. Na kipo kitu gani baada
ya haki, isipokuwa upotovu tu? Basi huwaje mkageuzwa?
|
Ayah 10:33 الأية
كَذَٰلِكَ حَقَّتْ كَلِمَتُ رَبِّكَ عَلَى الَّذِينَ فَسَقُوا أَنَّهُمْ لَا
يُؤْمِنُونَ
Kathalika haqqat kalimaturabbika AAala allatheena fasaqoo annahum layu/minoon
Swahili
Ndio kama hivyo kauli ya Mola wako Mlezi itakavyo wathibitikia wale walio
potoka, ya kwamba hawatoamini.
|
Ayah 10:34 الأية
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۚ قُلِ
اللهُ يَبْدَأُ الْخَلْقَ ثُمَّ يُعِيدُهُ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ
Qul hal min shuraka-ikum man yabdaoalkhalqa thumma yuAAeeduhu quli Allahu yabdao
alkhalqathumma yuAAeeduhu faanna tu/fakoon
Swahili
Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina aliye anzisha kuumba viumbe, na
kisha akavirejesha? Huwaje, basi, mkadanganywa?
|
Ayah 10:35 الأية
قُلْ هَلْ مِن شُرَكَائِكُم مَّن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ ۚ قُلِ اللهُ يَهْدِي
لِلْحَقِّ ۗ أَفَمَن يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ أَحَقُّ أَن يُتَّبَعَ أَمَّن لَّا
يَهِدِّي إِلَّا أَن يُهْدَىٰ ۖ فَمَا لَكُمْ كَيْفَ تَحْكُمُونَ
Qul hal min shuraka-ikum man yahdeeila alhaqqi quli Allahu yahdee lilhaqqiafaman
yahdee ila alhaqqi ahaqqu anyuttabaAAa amman la yahiddee illa an yuhdafama lakum
kayfa tahkumoon
Swahili
Sema: Je! Yupo katika miungu yenu ya ushirikina anaye ongoa kwendea Haki? Sema:
Mwenyezi Mungu anaongoa kwendea Haki. Basi, je, anaye stahiki kufuatwa ni yule
Mwenye kuongoa kwendea Haki au asiye ongoa ila aongozwe yeye? Basi nyinyi mna
nini? Mnahukumu namna gani?
|
Ayah 10:36 الأية
وَمَا يَتَّبِعُ أَكْثَرُهُمْ إِلَّا ظَنًّا ۚ إِنَّ الظَّنَّ لَا يُغْنِي مِنَ
الْحَقِّ شَيْئًا ۚ إِنَّ اللهَ عَلِيمٌ بِمَا يَفْعَلُونَ
Wama yattabiAAu aktharuhum illathannan inna aththanna layughnee mina alhaqqi
shay-an inna Allaha AAaleemunbima yafAAaloon
Swahili
Na wengi wao hawafuati ila dhana tu. Na dhana haifai kitu mbele ya haki. Hakika
Mwenyezi Mungu anajua yote wanayo yatenda.
|
Ayah 10:37 الأية
وَمَا كَانَ هَٰذَا الْقُرْآنُ أَن يُفْتَرَىٰ مِن دُونِ اللهِ وَلَٰكِن
تَصْدِيقَ الَّذِي بَيْنَ يَدَيْهِ وَتَفْصِيلَ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن
رَّبِّ الْعَالَمِينَ
Wama kana hatha alqur-anuan yuftara min dooni Allahi walakin tasdeeqaallathee
bayna yadayhi watafseela alkitabi larayba feehi min rabbi alAAalameen
Swahili
Na haiwezekani Qur'ani hii kuwa imetungwa na haitoki kwa Mwenyezi Mungu. Lakini
hii inasadikisha yaliyo tangulia, na ni mfafanuo wa Kitabu kisicho na shaka
ndani yake, kutokana na Mola Mlezi wa viumbe vyote.
|
Ayah 10:38 الأية
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۖ قُلْ فَأْتُوا بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُوا مَنِ
اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Am yaqooloona iftarahu qul fa/toobisooratin mithlihi wadAAoo mani istataAAtum
mindooni Allahi in kuntum sadiqeen
Swahili
Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite
(kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.
|
Ayah 10:39 الأية
بَلْ كَذَّبُوا بِمَا لَمْ يُحِيطُوا بِعِلْمِهِ وَلَمَّا يَأْتِهِمْ تَأْوِيلُهُ ۚ
كَذَٰلِكَ كَذَّبَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ
الظَّالِمِينَ
Bal kaththaboo bima lam yuheetoobiAAilmihi walamma ya/tihim ta/weeluhu kathalika
kaththabaallatheena min qablihim fanthurkayfa kana AAaqibatu aththalimeen
Swahili
Bali wameyakanusha wasio yaelewa ilimu yake kabla hayajawajia maelezo yake.
Kadhaalika walio kabla yao walikanusha vile vile. Basi angalia jinsi ulivyo kuwa
mwisho wa madhaalimu hao.
|
Ayah 10:40 الأية
وَمِنْهُم مَّن يُؤْمِنُ بِهِ وَمِنْهُم مَّن لَّا يُؤْمِنُ بِهِ ۚ وَرَبُّكَ
أَعْلَمُ بِالْمُفْسِدِينَ
Waminhum man yu/minu bihi waminhum man layu/minu bihi warabbuka aAAlamu
bilmufsideen
Swahili
Na miongoni mwao wapo wanao iamini, na miongoni mwao wapo wasio iamini. Na Mola
wako Mlezi anawajua vyema mafisadi.
|
Ayah 10:41 الأية
وَإِن كَذَّبُوكَ فَقُل لِّي عَمَلِي وَلَكُمْ عَمَلُكُمْ ۖ أَنتُم بَرِيئُونَ
مِمَّا أَعْمَلُ وَأَنَا بَرِيءٌ مِّمَّا تَعْمَلُونَ
Wa-in kaththabooka faqul lee AAamaleewalakum AAamalukum antum baree-oona mimma
aAAmalu waanabaree-on mimma taAAmaloon
Swahili
Na wakikukanusha wewe, sema: Mimi nina a'mali yangu, na nyinyi mna a'mali yenu.
Nyinyi hamna jukumu kwa niyatendayo, wala mimi sina jukumu kwa myatendayo.
|
Ayah 10:42 الأية
وَمِنْهُم مَّن يَسْتَمِعُونَ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تُسْمِعُ الصُّمَّ وَلَوْ
كَانُوا لَا يَعْقِلُونَ
Waminhum man yastamiAAoona ilayka afaantatusmiAAu assumma walaw kanoo
layaAAqiloon
Swahili
Na wapo miongoni mwao wanao kusikiliza. Je, wewe unaweza kuwafanya viziwi
wasikie ijapo kuwa hawafahamu?
|
Ayah 10:43 الأية
وَمِنْهُم مَّن يَنظُرُ إِلَيْكَ ۚ أَفَأَنتَ تَهْدِي الْعُمْيَ وَلَوْ كَانُوا لَا
يُبْصِرُونَ
Waminhum man yanthuru ilaykaafaanta tahdee alAAumya walaw kanoo la yubsiroon
Swahili
Na wapo miongoni mwao wanao kutazama. Je, wewe utawaongoa vipofu ingawa hawaoni?
|
Ayah 10:44 الأية
إِنَّ اللهَ لَا يَظْلِمُ النَّاسَ شَيْئًا وَلَٰكِنَّ النَّاسَ أَنفُسَهُمْ
يَظْلِمُونَ
Inna Allaha la yathlimuannasa shay-an walakinna annasaanfusahum yathlimoon
Swahili
Hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote; lakini watu wenyewe
wanajidhulumu nafsi zao.
|
Ayah 10:45 الأية
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ كَأَن لَّمْ يَلْبَثُوا إِلَّا سَاعَةً مِّنَ النَّهَارِ
يَتَعَارَفُونَ بَيْنَهُمْ ۚ قَدْ خَسِرَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِلِقَاءِ اللهِ
وَمَا كَانُوا مُهْتَدِينَ
Wayawma yahshuruhum kaan lamyalbathoo illa saAAatan mina annahariyataAAarafoona
baynahum qad khasira allatheena kaththaboobiliqa-i Allahi wama kanoo muhtadeen
Swahili
Na Siku atakapo wakusanya, itakuwa kama kwamba hawakukaa ila saa moja tu ya
mchana! Watatambuana. Hakika wamekhasirika walio kanusha kukutana na Mwenyezi
Mungu, wala hawakuwa wenye kuongoka.
|
Ayah 10:46 الأية
وَإِمَّا نُرِيَنَّكَ بَعْضَ الَّذِي نَعِدُهُمْ أَوْ نَتَوَفَّيَنَّكَ فَإِلَيْنَا
مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ اللهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا يَفْعَلُونَ
Wa-imma nuriyannaka baAAdaallathee naAAiduhum aw natawaffayannaka
fa-ilaynamarjiAAuhum thumma Allahu shaheedun AAala mayafAAaloon
Swahili
Na vyovyote vile, tukikuonyesha baadhi ya tunayo waahidi, au tukakufisha kabla
yake, marejeo yao ni kwetu. Kisha Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa wanayo yafanya.
|
Ayah 10:47 الأية
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ رَسُولُهُمْ قُضِيَ بَيْنَهُم
بِالْقِسْطِ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Walikulli ommatin rasoolun fa-itha jaarasooluhum qudiya baynahum bilqisti wahum
layuthlamoon
Swahili
Na kila umma una Mtume. Alipo wajia Mtume wao walihukumiwa baina yao kwa
uadilifu, wala hawakudhulumiwa.
|
Ayah 10:48 الأية
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Wayaqooloona mata hathaalwaAAdu in kuntum sadiqeen
Swahili
Na wanasema: Lini ahadi hii, ikiwa mnasema kweli?
|
Ayah 10:49 الأية
قُل لَّا أَمْلِكُ لِنَفْسِي ضَرًّا وَلَا نَفْعًا إِلَّا مَا شَاءَ اللهُ ۗ
لِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۚ إِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ فَلَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً ۖ
وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ
Qul la amliku linafsee darranwala nafAAan illa ma shaa Allahulikulli ommatin
ajalun itha jaa ajaluhum falayasta/khiroona saAAatan wala yastaqdimoon
Swahili
Sema: Sijimilikii nafsi yangu shari wala kheri ila apendavyo Mwenyezi Mungu.
Kila umma una muda wao walio wekewa. Ukifika muda wao hawakawii hata saa moja
wala hawatangulii.
|
Ayah 10:50 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِنْ أَتَاكُمْ عَذَابُهُ بَيَاتًا أَوْ نَهَارًا مَّاذَا
يَسْتَعْجِلُ مِنْهُ الْمُجْرِمُونَ
Qul araaytum in atakum AAathabuhubayatan aw naharan matha yastaAAjilu
minhualmujrimoon
Swahili
Sema: Mwaonaje ikikufikieni hiyo adhabu yake usiku au mchana, sehemu gani ya
adhabu wanaihimiza wakosefu?
|
Ayah 10:51 الأية
أَثُمَّ إِذَا مَا وَقَعَ آمَنتُم بِهِ ۚ آلْآنَ وَقَدْ كُنتُم بِهِ
تَسْتَعْجِلُونَ
Athumma itha ma waqaAAa amantumbihi al-ana waqad kuntum bihi tastaAAjiloon
Swahili
Tena je! Ikisha tokea mtaiamini? Je! Ndio sasa tena? Na nyinyi mlikuwa
mkiihimiza.
|
Ayah 10:52 الأية
ثُمَّ قِيلَ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ هَلْ تُجْزَوْنَ إِلَّا
بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ
Thumma qeela lillatheena thalamoothooqoo AAathaba alkhuldi hal tujzawna illabima
kuntum taksiboon
Swahili
Kisha walio dhulumu wataambiwa: Onjeni adhabu ya kudumu. Kwani mtalipwa isipo
kuwa yale mliyo kuwa mkiyachuma?
|
Ayah 10:53 الأية
وَيَسْتَنبِئُونَكَ أَحَقٌّ هُوَ ۖ قُلْ إِي وَرَبِّي إِنَّهُ لَحَقٌّ ۖ وَمَا
أَنتُم بِمُعْجِزِينَ
Wayastanbi-oonaka ahaqqun huwa qul eewarabbee innahu lahaqqun wama antum
bimuAAjizeen
Swahili
Na wanakuuliza: Je! Ni kweli hayo? Sema: Ehe! Naapa kwa Mola wangu Mlezi! Hakika
hayo ni kweli, na wala nyinyi hamshindi!
|
Ayah 10:54 الأية
وَلَوْ أَنَّ لِكُلِّ نَفْسٍ ظَلَمَتْ مَا فِي الْأَرْضِ لَافْتَدَتْ بِهِ ۗ
وَأَسَرُّوا النَّدَامَةَ لَمَّا رَأَوُا الْعَذَابَ ۖ وَقُضِيَ بَيْنَهُم
بِالْقِسْطِ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Walaw anna likulli nafsin thalamatma fee al-ardi laftadat bihi waasarroo
annadamatalamma raawoo alAAathaba waqudiya baynahum bilqistiwahum la yuthlamoon
Swahili
Na lau kuwa kila nafsi iliyo dhulumu inamiliki kila kiliomo duniani, bila ya
shaka ingeli toa vyote kujikombolea. Na watakapo iona adhabu wataficha majuto.
Na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu, nao hawatadhulumiwa.
|
Ayah 10:55 الأية
أَلَا إِنَّ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ أَلَا إِنَّ وَعْدَ
اللهِ حَقٌّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Ala inna lillahi ma feeassamawati wal-ardi alainna waAAda Allahi haqqun
walakinnaaktharahum la yaAAlamoon
Swahili
Jueni kuwa hakika vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vya Mwenyezi
Mungu. Jueni kuwa hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki. Lakini wengi wao
hawajui.
|
Ayah 10:56 الأية
هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Huwa yuhyee wayumeetu wa-ilayhiturjaAAoon
Swahili
Yeye ndiye anaye fufua na anaye fisha. Na kwake mtarejeshwa.
|
Ayah 10:57 الأية
يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَتْكُم مَّوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَشِفَاءٌ
لِّمَا فِي الصُّدُورِ وَهُدًى وَرَحْمَةٌ لِّلْمُؤْمِنِينَ
Ya ayyuha annasuqad jaatkum mawAAithatun min rabbikum washifaonlima fee
assudoori wahudan warahmatunlilmu/mineen
Swahili
Enyi watu! Yamekujieni mawaidha kutoka kwa Mola wenu Mlezi, na poza kuponyesha
yaliyomo vifuani, na uwongofu, na rehema kwa Waumini.
|
Ayah 10:58 الأية
قُلْ بِفَضْلِ اللهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا هُوَ خَيْرٌ
مِّمَّا يَجْمَعُونَ
Qul bifadli Allahi wabirahmatihifabithalika falyafrahoo huwa khayrun
mimmayajmaAAoon
Swahili
Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na rehema yake! Basi nawafurahi kwa hayo.
Haya ni bora kuliko hayo wanayo yakusanya.
|
Ayah 10:59 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُم مَّا أَنزَلَ اللهُ لَكُم مِّن رِّزْقٍ فَجَعَلْتُم مِّنْهُ
حَرَامًا وَحَلَالًا قُلْ آللهُ أَذِنَ لَكُمْ ۖ أَمْ عَلَى اللهِ تَفْتَرُونَ
Qul araaytum ma anzala Allahulakum min rizqin fajaAAaltum minhu haraman
wahalalanqul allahu athina lakum am AAala Allahitaftaroon
Swahili
Sema: Je! Mwaonaje zile riziki alizo kuteremshieni Mwenyezi Mungu, nanyi
mkafanya katika hizo nyengine haramu na nyengine halali. Sema: Je! Mwenyezi
Mungu amekuruhusuni, au mnamzulia Mwenyezi Mungu tu?
|
Ayah 10:60 الأية
وَمَا ظَنُّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللهِ الْكَذِبَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ
إِنَّ اللهَ لَذُو فَضْلٍ عَلَى النَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا
يَشْكُرُونَ
Wama thannu allatheenayaftaroona AAala Allahi alkathiba yawmaalqiyamati inna
Allaha lathoo fadlinAAala annasi walakinna aktharahum layashkuroon
Swahili
Na nini dhana ya wanao mzulia Mwenyezi Mungu kwa Siku ya Kiyama? Hakika Mwenyezi
Mungu ana fadhila juu ya watu, lakini wengi wao hawashukuru.
|
Ayah 10:61 الأية
وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ
عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ ۚ وَمَا يَعْزُبُ
عَن رَّبِّكَ مِن مِّثْقَالِ ذَرَّةٍ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ وَلَا
أَصْغَرَ مِن ذَٰلِكَ وَلَا أَكْبَرَ إِلَّا فِي كِتَابٍ مُّبِينٍ
Wama takoonu fee sha/nin wamatatloo minhu min qur-anin wala taAAmaloona
minAAamalin illa kunna AAalaykum shuhoodan ithtufeedoona feehi wama yaAAzubu
AAan rabbika minmithqali tharratin fee al-ardi walafee assama-i wala asghara min
thalikawala akbara illa fee kitabin mubeen
Swahili
Na huwi katika jambo lolote, wala husomi sehemu yoyote katika Qur'ani, wala
hamtendi kitendo chochote ila Sisi huwa ni mashahidi juu yenu mnapo shughulika
nayo. Na hakifichikani kwa Mola wako Mlezi chenye uzito hata wa chembe katika
ardhi na katika mbingu, wala kidogo kuliko hicho wala kikubwa ila kimo katika
Kitabu kilicho wazi.
|
Ayah 10:62 الأية
أَلَا إِنَّ أَوْلِيَاءَ اللهِ لَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ
Ala inna awliyaa Allahila khawfun AAalayhim wala hum yahzanoon
Swahili
Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.
|
Ayah 10:63 الأية
الَّذِينَ آمَنُوا وَكَانُوا يَتَّقُونَ
Allatheena amanoo wakanooyattaqoon
Swahili
Hao ni ambao wameamini na wakawa wanamcha Mungu.
|
Ayah 10:64 الأية
لَهُمُ الْبُشْرَىٰ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ ۚ لَا تَبْدِيلَ
لِكَلِمَاتِ اللهِ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
Lahumu albushra fee alhayatiaddunya wafee al-akhirati latabdeela likalimati
Allahi thalika huwaalfawzu alAAatheem
Swahili
Wao wana bishara njema katika maisha ya dunia na katika Akhera. Hapana
mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
|
Ayah 10:65 الأية
وَلَا يَحْزُنكَ قَوْلُهُمْ ۘ إِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا ۚ هُوَ السَّمِيعُ
الْعَلِيمُ
Wala yahzunka qawluhum innaalAAizzata lillahi jameeAAan huwa assameeAAualAAaleem
Swahili
Wala yasikuhuzunishe maneno yao. Hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu. Yeye
ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
|
Ayah 10:66 الأية
أَلَا إِنَّ لِلَّهِ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَمَن فِي الْأَرْضِ ۗ وَمَا يَتَّبِعُ
الَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ اللهِ شُرَكَاءَ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا
الظَّنَّ وَإِنْ هُمْ إِلَّا يَخْرُصُونَ
Ala inna lillahi man fee assamawatiwaman fee al-ardi wama yattabiAAu
allatheenayadAAoona min dooni Allahi shurakaa inyattabiAAoona illa aththanna
wa-inhum illa yakhrusoon
Swahili
Jueni kuwa ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na ardhinii. Na wala
hawawafuati hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu kuwa ni washirika wake.
Wao hawafuati ila dhana tu, na hawasemi ila uwongo.
|
Ayah 10:67 الأية
هُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ وَالنَّهَارَ مُبْصِرًا ۚ
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِّقَوْمٍ يَسْمَعُونَ
Huwa allathee jaAAala lakumu allaylalitaskunoo feehi wannahara mubsiran innafee
thalika laayatin liqawmin yasmaAAoon
Swahili
Yeye ndiye aliye kujaalieni usiku mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea.
Hakika katika haya zipo Ishara kwa watu wanao sikia.
|
Ayah 10:68 الأية
قَالُوا اتَّخَذَ اللهُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۖ هُوَ الْغَنِيُّ ۖ لَهُ مَا فِي
السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ إِنْ عِندَكُم مِّن سُلْطَانٍ بِهَٰذَا ۚ
أَتَقُولُونَ عَلَى اللهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Qaloo ittakhatha Allahuwaladan subhanahu huwa alghaniyyu lahu ma fee
assamawatiwama fee al-ardi in AAindakum min sultaninbihatha ataqooloona AAala
Allahi ma lataAAlamoon
Swahili
Wamesema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu, Aliye takasika! Yeye ni Mkwasi,
Mwenye Kujitosheleza. Vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vyake peke
yake. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo
yajua?
|
Ayah 10:69 الأية
قُلْ إِنَّ الَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى اللهِ الْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ
Qul inna allatheena yaftaroona AAalaAllahi alkathiba la yuflihoon
Swahili
Sema: Hao wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa.
|
Ayah 10:70 الأية
مَتَاعٌ فِي الدُّنْيَا ثُمَّ إِلَيْنَا مَرْجِعُهُمْ ثُمَّ نُذِيقُهُمُ الْعَذَابَ
الشَّدِيدَ بِمَا كَانُوا يَكْفُرُونَ
MataAAun fee addunyathumma ilayna marjiAAuhum thumma nutheequhumu
alAAathabaashshadeeda bima kanoo yakfuroon
Swahili
Hiyo ni starehe ya katika dunia tu, kisha marejeo yao ni kwetu. Tena
tutawaonjesha adhabu kali kwa sababu ya kukufuru kwao.
|
Ayah 10:71 الأية
وَاتْلُ عَلَيْهِمْ نَبَأَ نُوحٍ إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ يَا قَوْمِ إِن كَانَ
كَبُرَ عَلَيْكُم مَّقَامِي وَتَذْكِيرِي بِآيَاتِ اللهِ فَعَلَى اللهِ
تَوَكَّلْتُ فَأَجْمِعُوا أَمْرَكُمْ وَشُرَكَاءَكُمْ ثُمَّ لَا يَكُنْ أَمْرُكُمْ
عَلَيْكُمْ غُمَّةً ثُمَّ اقْضُوا إِلَيَّ وَلَا تُنظِرُونِ
Watlu AAalayhim nabaa noohinith qala liqawmihi ya qawmi in kanakabura AAalaykum
maqamee watathkeeree bi-ayatiAllahi faAAala Allahi tawakkaltu faajmiAAooamrakum
washurakaakum thumma la yakun amrukumAAalaykum ghummatan thumma iqdoo ilayya
wala tunthiroon
Swahili
Wasomee khabari za Nuhu alipo waambia watu wake: Enyi watu wangu! Ikiwa kukaa
kwangu nanyi na kukumbusha kwangu kwa Ishara za Mwenyezi Mungu kunakutieni
mashaka basi mimi namtegemea Mwenyezi Mungu. Nanyi tengezeni mambo yenu pamoja
na washirika wenu, na wala mambo yenu yasifichikane kwenu. Kisha nihukumuni,
wala msinipe muhula.
|
Ayah 10:72 الأية
فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَمَا سَأَلْتُكُم مِّنْ أَجْرٍ ۖ إِنْ أَجْرِيَ إِلَّا عَلَى
اللهِ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُسْلِمِينَ
Fa-in tawallaytum fama saaltukum minajrin in ajriya illa AAala Allahi waomirtuan
akoona mina almuslimeen
Swahili
Lakini mkigeuka, basi mimi sikukuombeni ujira. Ujira wangu hauko ila kwa
Mwenyezi Mungu. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu.
|
Ayah 10:73 الأية
فَكَذَّبُوهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَمَن مَّعَهُ فِي الْفُلْكِ وَجَعَلْنَاهُمْ
خَلَائِفَ وَأَغْرَقْنَا الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ
عَاقِبَةُ الْمُنذَرِينَ
Fakaththaboohu fanajjaynahuwaman maAAahu fee alfulki wajaAAalnahum
khala-ifawaaghraqna allatheena kaththaboo bi-ayatinafanthur kayfa kana
AAaqibatualmunthareen
Swahili
Wakamkanusha. Basi tukamwokoa, pamoja na walio kuwa naye, katika jahazi. Na
tukawafanya wao ndio walio bakia, na tukawazamisha walio zikanusha Ishara zetu.
Basi angalia vipi ulikuwa mwisho wa walio onywa.
|
Ayah 10:74 الأية
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِ رُسُلًا إِلَىٰ قَوْمِهِمْ فَجَاءُوهُم
بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا بِهِ مِن قَبْلُ ۚ
كَذَٰلِكَ نَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْمُعْتَدِينَ
Thumma baAAathna min baAAdihi rusulanila qawmihim fajaoohum bilbayyinatifama
kanoo liyu/minoo bima kaththaboobihi min qablu kathalika natbaAAu AAalaquloobi
almuAAtadeen
Swahili
Kisha baada yake tukawatuma Mitume kwa watu wao. Nao wakawajia kwa Ishara zilizo
wazi. Lakini hawakuwa wenye kuyaamini waliyo yakanusha kabla yake. Ndio kama
hivyo tunapiga muhuri juu ya nyoyo za warukao mipaka.
|
Ayah 10:75 الأية
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ وَهَارُونَ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ
بِآيَاتِنَا فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا مُّجْرِمِينَ
Thumma baAAathna min baAAdihim moosawaharoona ila firAAawna wamala-ihi
bi-ayatinafastakbaroo wakanoo qawman mujrimeen
Swahili
Kisha baada yao tukamtuma Musa na Haruni kwa Firauni na waheshimiwa wake, kwa
Ishara zetu. Wakajivuna, na wakawa watu wakosefu.
|
Ayah 10:76 الأية
فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا إِنَّ هَٰذَا لَسِحْرٌ مُّبِينٌ
Falamma jaahumu alhaqqumin AAindina qaloo inna hatha lasihrunmubeen
Swahili
Basi ilipo wajia Haki kutoka kwetu walisema: Hakika huu ni uchawi dhaahiri.
|
Ayah 10:77 الأية
قَالَ مُوسَىٰ أَتَقُولُونَ لِلْحَقِّ لَمَّا جَاءَكُمْ ۖ أَسِحْرٌ هَٰذَا وَلَا
يُفْلِحُ السَّاحِرُونَ
Qala moosa ataqooloona lilhaqqilamma jaakum asihrun hatha walayuflihu assahiroon
Swahili
Akasema Musa: Mnasema hivi juu ya Haki ilipo kujieni? Huu ni uchawi? Na wachawi
hawafanikiwi!
|
Ayah 10:78 الأية
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ
لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ وَمَا نَحْنُ لَكُمَا بِمُؤْمِنِينَ
Qaloo aji/tana litalfitanaAAamma wajadna AAalayhi abaanawatakoona lakuma
alkibriyao fee al-ardi wamanahnu lakuma bimu/mineen
Swahili
Wakasema: Je! Umetujia ili utuachishe tuliyo wakuta nayo baba zetu, na mpate
nyinyi wawili ukubwa katika nchi? Wala sisi hatukuaminini nyinyi.
|
Ayah 10:79 الأية
وَقَالَ فِرْعَوْنُ ائْتُونِي بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ
Waqala firAAawnu i/toonee bikulli sahirinAAaleem
Swahili
Na Firauni akasema: Nileteeni kila mchawi mjuzi!
|
Ayah 10:80 الأية
فَلَمَّا جَاءَ السَّحَرَةُ قَالَ لَهُم مُّوسَىٰ أَلْقُوا مَا أَنتُم مُّلْقُونَ
Falamma jaa assaharatuqala lahum moosa alqoo ma antum mulqoon
Swahili
Basi walipo kuja wachawi, Musa aliwaambia: Tupeni mnavyo tupa!
|
Ayah 10:81 الأية
فَلَمَّا أَلْقَوْا قَالَ مُوسَىٰ مَا جِئْتُم بِهِ السِّحْرُ ۖ إِنَّ اللهَ
سَيُبْطِلُهُ ۖ إِنَّ اللهَ لَا يُصْلِحُ عَمَلَ الْمُفْسِدِينَ
Falamma alqaw qala moosama ji/tum bihi assihru inna Allahasayubtiluhu inna
Allaha la yuslihuAAamala almufsideen
Swahili
Walipo tupa, Musa alisema: Mliyo leta ni uchawi. Hakika Mwenyezi Mungu
haitengenezi kazi ya waharibifu.
|
Ayah 10:82 الأية
وَيُحِقُّ اللهُ الْحَقَّ بِكَلِمَاتِهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُجْرِمُونَ
Wayuhiqqu Allahu alhaqqabikalimatihi walaw kariha almujrimoon
Swahili
Na Mwenyezi Mungu huhakikisha Haki kwa maneno yake, hata wanga chukia wakosefu
|
Ayah 10:83 الأية
فَمَا آمَنَ لِمُوسَىٰ إِلَّا ذُرِّيَّةٌ مِّن قَوْمِهِ عَلَىٰ خَوْفٍ مِّن
فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِمْ أَن يَفْتِنَهُمْ ۚ وَإِنَّ فِرْعَوْنَ لَعَالٍ فِي
الْأَرْضِ وَإِنَّهُ لَمِنَ الْمُسْرِفِينَ
Fama amana limoosa illathurriyyatun min qawmihi AAala khawfin minfirAAawna
wamala-ihim an yaftinahum wa-inna firAAawna laAAalinfee al-ardi wa-innahu lamina
almusrifeen
Swahili
Basi hawakumuamini Musa isipo kuwa baadhi ya vijana vya kaumu yake, kwa
kumwogopa Firauni na wakuu wao wasiwatese. Kwani hakika Firauni alikuwa jeuri
katika nchi. Na kwa yakini alikuwa miongoni mwa walio pita kiasi.
|
Ayah 10:84 الأية
وَقَالَ مُوسَىٰ يَا قَوْمِ إِن كُنتُمْ آمَنتُم بِاللهِ فَعَلَيْهِ تَوَكَّلُوا
إِن كُنتُم مُّسْلِمِينَ
Waqala moosa ya qawmiin kuntum amantum billahi faAAalayhitawakkaloo in kuntum
muslimeen
Swahili
Na Musa alisema: Enyi watu wangu! Ikiwa nyinyi mmemuamini Mwenyezi Mungu, basi
mtegemeeni Yeye, ikiwa nyinyi ni Waislamu.
|
Ayah 10:85 الأية
فَقَالُوا عَلَى اللهِ تَوَكَّلْنَا رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً
لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Faqaloo AAala Allahitawakkalna rabbana la tajAAalnafitnatan lilqawmi
aththalimeen
Swahili
Wakasema: Tunamtegemea Mwenyezi Mungu. Ewe Mola wetu Mlezi! Usitufanye wenye
kutiwa misukosuko na hao watu madhaalimu.
|
Ayah 10:86 الأية
وَنَجِّنَا بِرَحْمَتِكَ مِنَ الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ
Wanajjina birahmatika minaalqawmi alkafireen
Swahili
Na utuokoe kwa rehema yako na watu makafiri.
|
Ayah 10:87 الأية
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ وَأَخِيهِ أَن تَبَوَّآ لِقَوْمِكُمَا بِمِصْرَ
بُيُوتًا وَاجْعَلُوا بُيُوتَكُمْ قِبْلَةً وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ ۗ وَبَشِّرِ
الْمُؤْمِنِينَ
Waawhayna ila moosawaakheehi an tabawwaa liqawmikuma bimisrabuyootan wajAAaloo
buyootakum qiblatan waaqeemoo assalatawabashshiri almu/mineen
Swahili
Na tukampelekea Musa na ndugu yake wahyi huu: Watengenezeeni majumba watu wenu
katika Misri na zifanyeni nyumba zenu ndio mwahali mwa ibada, na mshike Sala, na
wabashirie Waumini.
|
Ayah 10:88 الأية
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبَّنَا إِنَّكَ آتَيْتَ فِرْعَوْنَ وَمَلَأَهُ زِينَةً
وَأَمْوَالًا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا رَبَّنَا لِيُضِلُّوا عَن سَبِيلِكَ ۖ
رَبَّنَا اطْمِسْ عَلَىٰ أَمْوَالِهِمْ وَاشْدُدْ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَلَا
يُؤْمِنُوا حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ
Waqala moosa rabbanainnaka atayta firAAawna wamalaahu zeenatan waamwalanfee
alhayati addunya rabbanaliyudilloo AAan sabeelika rabbana itmis AAalaamwalihim
washdud AAala quloobihim falayu/minoo hatta yarawoo alAAathaba al-aleem
Swahili
Na Musa akasema: Mola wetu Mlezi! Hakika wewe umempa Firauni na wakuu wake
mapambo na mali katika maisha ya dunia. Hivyo wanapoteza watu na Njia yako. Mola
wetu Mlezi! Yafutilie mbali mali yao na zifunge nyoyo zao, wasiamini mpaka
waione adhabu chungu.
|
Ayah 10:89 الأية
قَالَ قَدْ أُجِيبَت دَّعْوَتُكُمَا فَاسْتَقِيمَا وَلَا تَتَّبِعَانِّ سَبِيلَ
الَّذِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Qala qad ojeebat daAAwatukumafastaqeema wala tattabiAAannisabeela allatheena la
yaAAlamoon
Swahili
Mwenyezi Mungu akasema: Maombi yenu yamekubaliwa. Basi simameni sawa sawa, wala
msifuate njia za wale wasio jua.
|
Ayah 10:90 الأية
وَجَاوَزْنَا بِبَنِي إِسْرَائِيلَ الْبَحْرَ فَأَتْبَعَهُمْ فِرْعَوْنُ
وَجُنُودُهُ بَغْيًا وَعَدْوًا ۖ حَتَّىٰ إِذَا أَدْرَكَهُ الْغَرَقُ قَالَ آمَنتُ
أَنَّهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا الَّذِي آمَنَتْ بِهِ بَنُو إِسْرَائِيلَ وَأَنَا مِنَ
الْمُسْلِمِينَ
Wajawazna bibanee isra-eelaalbahra faatbaAAahum firAAawnu wajunooduhu
baghyanwaAAadwan hatta itha adrakahu algharaqu qalaamantu annahu la ilaha illa
allatheeamanat bihi banoo isra-eela waana minaalmuslimeen
Swahili
Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa
dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa
hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa
walio nyenyekea!
|
Ayah 10:91 الأية
آلْآنَ وَقَدْ عَصَيْتَ قَبْلُ وَكُنتَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ
Al-ana waqad AAasaytaqablu wakunta mina almufsideen
Swahili
Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi!
|
Ayah 10:92 الأية
فَالْيَوْمَ نُنَجِّيكَ بِبَدَنِكَ لِتَكُونَ لِمَنْ خَلْفَكَ آيَةً ۚ وَإِنَّ
كَثِيرًا مِّنَ النَّاسِ عَنْ آيَاتِنَا لَغَافِلُونَ
Falyawma nunajjeeka bibadanikalitakoona liman khalfaka ayatan wa-inna katheeran
mina annasiAAan ayatina laghafiloon
Swahili
Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma
yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.
|
Ayah 10:93 الأية
وَلَقَدْ بَوَّأْنَا بَنِي إِسْرَائِيلَ مُبَوَّأَ صِدْقٍ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ
الطَّيِّبَاتِ فَمَا اخْتَلَفُوا حَتَّىٰ جَاءَهُمُ الْعِلْمُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ
يَقْضِي بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Walaqad bawwa/na banee isra-eelamubawwaa sidqin warazaqnahum mina
attayyibatifama ikhtalafoo hatta jaahumualAAilmu inna rabbaka yaqdee baynahum
yawma alqiyamatifeema kanoo feehi yakhtalifoon
Swahili
Na hakika tuliwaweka Wana wa Is raili kikao chema, na tukawaruzuku vitu vizuri.
Nao hawakukhitalifiana mpaka ilipo wafikia ilimu. Hakika Mola wako Mlezi
atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana.
|
Ayah 10:94 الأية
فَإِن كُنتَ فِي شَكٍّ مِّمَّا أَنزَلْنَا إِلَيْكَ فَاسْأَلِ الَّذِينَ
يَقْرَءُونَ الْكِتَابَ مِن قَبْلِكَ ۚ لَقَدْ جَاءَكَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا
تَكُونَنَّ مِنَ الْمُمْتَرِينَ
Fa-in kunta fee shakkin mimma anzalnnailayka fas-ali allatheena yaqraoona
alkitabamin qablika laqad jaaka alhaqqu min rabbika falatakoonanna mina
almumtareen
Swahili
Na ikiwa unayo shaka katika tuliyo kuteremshia, basi waulize wasomao Kitabu
kabla yako. Kwa yakini imekwisha kujia Haki kutoka kwa Mola wako Mlezi. Basi
usiwe miongoni mwa wenye shaka.
|
Ayah 10:95 الأية
وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِ اللهِ فَتَكُونَ مِنَ
الْخَاسِرِينَ
Wala takoonanna mina allatheenakaththaboo bi-ayati Allahi fatakoonamina
alkhasireen
Swahili
Na kabisa usiwe miongoni mwa wale wanao zikanusha Ishara za Mwenyezi Mungu,
usije kuwa katika walio khasiri.
|
Ayah 10:96 الأية
إِنَّ الَّذِينَ حَقَّتْ عَلَيْهِمْ كَلِمَتُ رَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ
Inna allatheena haqqatAAalayhim kalimatu rabbika la yu/minoon
Swahili
Hakika wale ambao neno la Mola wako Mlezi limekwisha thibitika juu yao,
hawataamini,
|
Ayah 10:97 الأية
وَلَوْ جَاءَتْهُمْ كُلُّ آيَةٍ حَتَّىٰ يَرَوُا الْعَذَابَ الْأَلِيمَ
Walaw jaat-hum kullu ayatin hattayarawoo alAAathaba al-aleem
Swahili
Ijapo kuwa itawajia kila Ishara, mpaka waione adhabu iliyo chungu.
|
Ayah 10:98 الأية
فَلَوْلَا كَانَتْ قَرْيَةٌ آمَنَتْ فَنَفَعَهَا إِيمَانُهَا إِلَّا قَوْمَ يُونُسَ
لَمَّا آمَنُوا كَشَفْنَا عَنْهُمْ عَذَابَ الْخِزْيِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا
وَمَتَّعْنَاهُمْ إِلَىٰ حِينٍ
Falawla kanat qaryatun amanatfanafaAAaha eemanuha illa qawmayoonusa lamma amanoo
kashafna AAanhum AAathabaalkhizyi fee alhayati addunyawamattaAAnahum ila heen
Swahili
Kwa nini usiwepo mji mmoja ukaamini na Imani yake ikawafaa - isipo kuwa kaumu
Yunus? Waliamini na Sisi tukawaondolea adhabu ya hizaya katika maisha ya dunia,
na tukawastarehesha kwa muda.
|
Ayah 10:99 الأية
وَلَوْ شَاءَ رَبُّكَ لَآمَنَ مَن فِي الْأَرْضِ كُلُّهُمْ جَمِيعًا ۚ أَفَأَنتَ
تُكْرِهُ النَّاسَ حَتَّىٰ يَكُونُوا مُؤْمِنِينَ
Walaw shaa rabbuka laamana manfee al-ardi kulluhum jameeAAan afaanta tukrihu
annasahatta yakoonoo mu/mineen
Swahili
Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe
utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?
|
Ayah 10:100 الأية
وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تُؤْمِنَ إِلَّا بِإِذْنِ اللهِ ۚ وَيَجْعَلُ الرِّجْسَ
عَلَى الَّذِينَ لَا يَعْقِلُونَ
Wama kana linafsin an tu/minailla bi-ithni Allahi wayajAAalu arrijsaAAala
allatheena la yaAAqiloon
Swahili
Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu
iwafike wasio tumia akili zao.
|
Ayah 10:101 الأية
قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَا تُغْنِي الْآيَاتُ
وَالنُّذُرُ عَن قَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ
Quli onthuroo mathafee assamawati wal-ardi wamatughnee al-ayatu wannuthuru
AAanqawmin la yu/minoon
Swahili
Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na Ishara zote na maonyo
hayawafai kitu watu wasio amini.
|
Ayah 10:102 الأية
فَهَلْ يَنتَظِرُونَ إِلَّا مِثْلَ أَيَّامِ الَّذِينَ خَلَوْا مِن قَبْلِهِمْ ۚ
قُلْ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ
Fahal yantathiroona illamithla ayyami allatheena khalaw min qablihim qul
fantathirooinnee maAAakum mina almuntathireen
Swahili
Basi, je! Wanangojea jingine ila kama yaliyo tokea siku za watu walio pita kabla
yao? Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanao ngoja.
|
Ayah 10:103 الأية
ثُمَّ نُنَجِّي رُسُلَنَا وَالَّذِينَ آمَنُوا ۚ كَذَٰلِكَ حَقًّا عَلَيْنَا نُنجِ
الْمُؤْمِنِينَ
Thumma nunajjee rusulana wallatheenaamanoo kathalika haqqan AAalaynanunjee
almu/mineen
Swahili
Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na walio amini. Ndio kama hivyo, inatustahiki
kuwaokoa Waumini.
|
Ayah 10:104 الأية
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ إِن كُنتُمْ فِي شَكٍّ مِّن دِينِي فَلَا أَعْبُدُ
الَّذِينَ تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ وَلَٰكِنْ أَعْبُدُ اللهَ الَّذِي
يَتَوَفَّاكُمْ ۖ وَأُمِرْتُ أَنْ أَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Qul ya ayyuha annasuin kuntum fee shakkin min deenee fala aAAbudu
allatheenataAAbudoona min dooni Allahi walakin aAAbudu Allahaallathee
yatawaffakum waomirtu an akoona minaalmu/mineen
Swahili
Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini yangu, basi mimi siwaabudu
mnao waabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini mimi namuabudu Mwenyezi
Mungu anaye kufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waumini.
|
Ayah 10:105 الأية
وَأَنْ أَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ
Waan aqim wajhaka liddeeni haneefanwala takoonanna mina almushrikeen
Swahili
Na uelekeze uso wako kwenye Dini ya Kweli, wala usiwe katika washirikina.
|
Ayah 10:106 الأية
وَلَا تَدْعُ مِن دُونِ اللهِ مَا لَا يَنفَعُكَ وَلَا يَضُرُّكَ ۖ فَإِن
فَعَلْتَ فَإِنَّكَ إِذًا مِّنَ الظَّالِمِينَ
Wala tadAAu min dooni Allahima la yanfaAAuka wala yadurruka fa-infaAAalta
fa-innaka ithan mina aththalimeen
Swahili
Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao hawakufai kitu wala
hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio dhulumu.
|
Ayah 10:107 الأية
وَإِن يَمْسَسْكَ اللهُ بِضُرٍّ فَلَا كَاشِفَ لَهُ إِلَّا هُوَ ۖ وَإِن يُرِدْكَ
بِخَيْرٍ فَلَا رَادَّ لِفَضْلِهِ ۚ يُصِيبُ بِهِ مَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ ۚ
وَهُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Wa-in yamsaska Allahu bidurrinfala kashifa lahu illa huwa wa-in yuridkabikhayrin
fala radda lifadlihi yuseebubihi man yashao min AAibadihi wahuwa alghafooru
arraheem
Swahili
Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa kukuondolea ila Yeye. Na
akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha fadhila yake. Huifikisha kwa
amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 10:108 الأية
قُلْ يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءَكُمُ الْحَقُّ مِن رَّبِّكُمْ ۖ فَمَنِ
اهْتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهْتَدِي لِنَفْسِهِ ۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ
عَلَيْهَا ۖ وَمَا أَنَا عَلَيْكُم بِوَكِيلٍ
Qul ya ayyuha annasuqad jaakumu alhaqqu min rabbikum famani ihtadafa-innama
yahtadee linafsihi waman dalla fa-innamayadillu AAalayha wama ana
AAalaykumbiwakeel
Swahili
Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anaye
ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye potea anapotea kwa khasara ya
nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu.
|
Ayah 10:109 الأية
وَاتَّبِعْ مَا يُوحَىٰ إِلَيْكَ وَاصْبِرْ حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللهُ ۚ وَهُوَ
خَيْرُ الْحَاكِمِينَ
WattabiAA ma yoohailayka wasbir hatta yahkumaAllahu wahuwa khayru alhakimeen
Swahili
Na wewe fuata yanayo funuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu
ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|