1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
الم
Alif-lam-meem
Swahili
Alif Lam Mim (A.L.M.)
|
Ayah 32:2 الأية
تَنزِيلُ الْكِتَابِ لَا رَيْبَ فِيهِ مِن رَّبِّ الْعَالَمِينَ
Tanzeelu alkitabi la raybafeehi min rabbi alAAalameen
Swahili
Huu ni mteremsho wa Kitabu kisicho kuwa na shaka yoyote kinacho toka kwa Mola
Mlezi wa walimwengu wote.
|
Ayah 32:3 الأية
أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ ۚ بَلْ هُوَ الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ لِتُنذِرَ قَوْمًا
مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ
Am yaqooloona iftarahu bal huwa alhaqqumin rabbika litunthira qawman ma atahum
minnatheerin min qablika laAAallahum yahtadoon
Swahili
Au wanasema: Amekizua? Bali hichi ni Kweli iliyo toka kwa Mola wako Mlezi ili
uwaonye watu wasio fikiwa na mwonyaji kabla yako; huenda wakaongoka.
|
Ayah 32:4 الأية
اللهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ
أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ مَا لَكُم مِّن دُونِهِ مِن وَلِيٍّ
وَلَا شَفِيعٍ ۚ أَفَلَا تَتَذَكَّرُونَ
Allahu allathee khalaqa assamawatiwal-arda wama baynahuma fee sittatiayyamin
thumma istawa AAala alAAarshi malakum min doonihi min waliyyin wala shafeeAAin
afalatatathakkaroon
Swahili
Mwenyezi Mungu ndiye aliye umba mbingu na ardhi na viliomo baina yao kwa siku
sita, na akatawala kwenye Kiti cha Enzi. Nyinyi hamna mlinzi wala mwombezi isipo
kuwa Yeye tu. Basi, je, hamkumbuki?
|
Ayah 32:5 الأية
يُدَبِّرُ الْأَمْرَ مِنَ السَّمَاءِ إِلَى الْأَرْضِ ثُمَّ يَعْرُجُ إِلَيْهِ فِي
يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ أَلْفَ سَنَةٍ مِّمَّا تَعُدُّونَ
Yudabbiru al-amra mina assama-iila al-ardi thumma yaAAruju ilayhi fee yawmin
kanamiqdaruhu alfa sanatin mimma taAAuddoon
Swahili
Anapitisha mambo yote yalio baina mbingu na ardhi, kisha yanapanda kwake kwa
siku ambayo kipimo chake ni miaka elfu kwa mnavyo hisabu nyinyi.
|
Ayah 32:6 الأية
ذَٰلِكَ عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ
Thalika AAalimu alghaybi washshahadatialAAazeezu arraheem
Swahili
Huyu ndiye Mwenye kuyajua yasiyo onekana na yanayo onekana. Mwenye nguvu, Mwenye
kurehemu.
|
Ayah 32:7 الأية
الَّذِي أَحْسَنَ كُلَّ شَيْءٍ خَلَقَهُ ۖ وَبَدَأَ خَلْقَ الْإِنسَانِ مِن طِينٍ
Allathee ahsana kulla shay-inkhalaqahu wabadaa khalqa al-insani min teen
Swahili
Ambaye ametengeneza vizuri umbo la kila kitu; na akaanzisha kumuumba mtu kwa
udongo.
|
Ayah 32:8 الأية
ثُمَّ جَعَلَ نَسْلَهُ مِن سُلَالَةٍ مِّن مَّاءٍ مَّهِينٍ
Thumma jaAAala naslahu min sulalatinmin ma-in maheen
Swahili
Na kisha akajaalia uzao wake utokane na kizazi cha maji madhaifu.
|
Ayah 32:9 الأية
ثُمَّ سَوَّاهُ وَنَفَخَ فِيهِ مِن رُّوحِهِ ۖ وَجَعَلَ لَكُمُ السَّمْعَ
وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
Thumma sawwahu wanafakha feehi min roohihiwajaAAala lakumu assamAAa wal-absara
wal-af-idataqaleelan ma tashkuroon
Swahili
Kisha akamtengeneza, na akampulizia roho yake, na akakujaalieni kusikia na
kuona, na nyoyo za kufahamu. Ni uchache mnavyo shukuru.
|
Ayah 32:10 الأية
وَقَالُوا أَإِذَا ضَلَلْنَا فِي الْأَرْضِ أَإِنَّا لَفِي خَلْقٍ جَدِيدٍ ۚ بَلْ
هُم بِلِقَاءِ رَبِّهِمْ كَافِرُونَ
Waqaloo a-itha dalalnafee al-ardi a-inna lafee khalqin jadeedin bal humbiliqa-i
rabbihim kafiroon
Swahili
Nao husema: Tutapo kwisha potea chini ya ardhi, ni kweli tutarudishwa katika
umbo jipya? Bali wao wanakanusha kwamba watakutana na Mola wao Mlezi.
|
Ayah 32:11 الأية
قُلْ يَتَوَفَّاكُم مَّلَكُ الْمَوْتِ الَّذِي وُكِّلَ بِكُمْ ثُمَّ إِلَىٰ
رَبِّكُمْ تُرْجَعُونَ
Qul yatawaffakum malaku almawti allatheewukkila bikum thumma ila rabbikum
turjaAAoon
Swahili
Sema: Atakufisheni Malaika wa mauti aliye wakilishwa juu yenu; kisha mtarejeshwa
kwa Mola wenu Mlezi.
|
Ayah 32:12 الأية
وَلَوْ تَرَىٰ إِذِ الْمُجْرِمُونَ نَاكِسُو رُءُوسِهِمْ عِندَ رَبِّهِمْ رَبَّنَا
أَبْصَرْنَا وَسَمِعْنَا فَارْجِعْنَا نَعْمَلْ صَالِحًا إِنَّا مُوقِنُونَ
Walaw tara ithi almujrimoona nakisooruoosihim AAinda rabbihim rabbana
absarnawasamiAAna faarjiAAna naAAmal salihaninna mooqinoon
Swahili
Na ungeli waona wakosefu wanvyo inamisha vichwa vyao mbele ya Mola wao Mlezi,
(wakisema): Mola wetu Mlezi! Tumesha ona, na tumesha sikia. Turejeshe tukatende
mema, kwani hakika sisi tumekwisha kuwa na yakini sasa.
|
Ayah 32:13 الأية
وَلَوْ شِئْنَا لَآتَيْنَا كُلَّ نَفْسٍ هُدَاهَا وَلَٰكِنْ حَقَّ الْقَوْلُ مِنِّي
لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ
Walaw shi-na laataynakulla nafsin hudaha walakin haqqaalqawlu minnee laamlaanna
jahannama mina aljinnati wannasiajmaAAeen
Swahili
Na lau tungeli taka tunge mpa kila mtu uwongofu wake. Lakini imekwisha kuwa
kauli iliyo toka kwangu : Kwa yakini nitaijaza Jahannamu kwa wote hawa, majini
na watu.
|
Ayah 32:14 الأية
فَذُوقُوا بِمَا نَسِيتُمْ لِقَاءَ يَوْمِكُمْ هَٰذَا إِنَّا نَسِينَاكُمْ ۖ
وَذُوقُوا عَذَابَ الْخُلْدِ بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Fathooqoo bima naseetum liqaayawmikum hatha inna naseenakum wathooqooAAathaba
alkhuldi bima kuntum taAAmaloon
Swahili
Basi onjeni kwa vile mlivyo usahau mkutano wa Siku yenu hii. Na Sisi hakika
tunakusahauni. Basi onjeni adhabu ya milele kwa yale mliyo kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 32:15 الأية
إِنَّمَا يُؤْمِنُ بِآيَاتِنَا الَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِهَا خَرُّوا سُجَّدًا
وَسَبَّحُوا بِحَمْدِ رَبِّهِمْ وَهُمْ لَا يَسْتَكْبِرُونَ ۩
Innama yu/minu bi-ayatinaallatheena itha thukkiroo bihakharroo sujjadan
wasabbahoo bihamdi rabbihim wahumla yastakbiroon
Swahili
Hakika wanao ziamini Aya zetu ni hao tu ambao wakikumbushwa hizo, basi wao
huanguka kusujudu, na humsabihi Mola wao Mlezi kwa kumhimidi, nao hawajivuni.
|
Ayah 32:16 الأية
تَتَجَافَىٰ جُنُوبُهُمْ عَنِ الْمَضَاجِعِ يَدْعُونَ رَبَّهُمْ خَوْفًا وَطَمَعًا
وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ
Tatajafa junoobuhum AAani almadajiAAiyadAAoona rabbahum khawfan watamaAAan
wamimmarazaqnahum yunfiqoon
Swahili
Mbavu zao zinaachana na vitanda kwa kumwomba Mola wao Mlezi kwa khofu na
kutumaini, na hutoa kutokana na tulivyo waruzuku.
|
Ayah 32:17 الأية
فَلَا تَعْلَمُ نَفْسٌ مَّا أُخْفِيَ لَهُم مِّن قُرَّةِ أَعْيُنٍ جَزَاءً بِمَا
كَانُوا يَعْمَلُونَ
Fala taAAlamu nafsun maokhfiya lahum min qurrati aAAyunin jazaan bima
kanooyaAAmaloon
Swahili
Nafsi yoyote haijui waliyo fichiwa katika hayo yanayo furahisha macho - ni
malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 32:18 الأية
أَفَمَن كَانَ مُؤْمِنًا كَمَن كَانَ فَاسِقًا ۚ لَّا يَسْتَوُونَ
Afaman kana mu/minan kaman kanafasiqan la yastawoon
Swahili
Ati aliye Muumini atakuwa sawa na aliye mpotovu? Hawawi sawa.
|
Ayah 32:19 الأية
أَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَلَهُمْ جَنَّاتُ الْمَأْوَىٰ
نُزُلًا بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Amma allatheena amanoowaAAamiloo assalihati falahum jannatualma/wa nuzulan bima
kanoo yaAAmaloon
Swahili
Ama walio amini na wakatenda mema, watakuwa nazo Bustani za makaazi mazuri. Ndio
pa kufikia kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 32:20 الأية
وَأَمَّا الَّذِينَ فَسَقُوا فَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۖ كُلَّمَا أَرَادُوا أَن
يَخْرُجُوا مِنْهَا أُعِيدُوا فِيهَا وَقِيلَ لَهُمْ ذُوقُوا عَذَابَ النَّارِ
الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ
Waamma allatheena fasaqoofama/wahumu annaru kullama aradooan yakhrujoo minha
oAAeedoo feeha waqeela lahum thooqooAAathaba annari allathee kuntum
bihitukaththiboon
Swahili
Na ama wale walio tenda uovu, basi makaazi yao ni Motoni. Kila wakitaka kutoka
humo watarudishwa humo humo. Na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mliyo
kuwa mkiikanusha.
|
Ayah 32:21 الأية
وَلَنُذِيقَنَّهُم مِّنَ الْعَذَابِ الْأَدْنَىٰ دُونَ الْعَذَابِ الْأَكْبَرِ
لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ
Walanutheeqannahum mina alAAathabial-adna doona alAAathabi al-akbari
laAAallahumyarjiAAoon
Swahili
Na tutawaonjesha adhabu khafifu kabla ya adhabu kubwa, huenda labda watarejea.
|
Ayah 32:22 الأية
وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن ذُكِّرَ بِآيَاتِ رَبِّهِ ثُمَّ أَعْرَضَ عَنْهَا ۚ إِنَّا
مِنَ الْمُجْرِمِينَ مُنتَقِمُونَ
Waman athlamu mimman thukkirabi-ayati rabbihi thumma aAArada AAanhainna mina
almujrimeena muntaqimoon
Swahili
Na ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye kumbushwa kwa Ishara za Mola wake
Mlezi, kisha akazikataa? Hakika Sisi tutajilipiza kwa wakosefu.
|
Ayah 32:23 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ فَلَا تَكُن فِي مِرْيَةٍ مِّن لِّقَائِهِ ۖ
وَجَعَلْنَاهُ هُدًى لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ
Walaqad atayna moosaalkitaba fala takun fee miryatin min liqa-ihiwajaAAalnahu
hudan libanee isra-eel
Swahili
Hakika Sisi tulikwisha mpa Musa Kitabu. Basi usiwe na shaka kuwa kakipokea. Na
tukakifanya kuwa ni uwongofu kwa Wana wa Israili.
|
Ayah 32:24 الأية
وَجَعَلْنَا مِنْهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا لَمَّا صَبَرُوا ۖ وَكَانُوا
بِآيَاتِنَا يُوقِنُونَ
WajaAAalna minhum a-immatan yahdoonabi-amrina lamma sabaroo wakanoo
bi-ayatinayooqinoon
Swahili
Na tukawafanya miongoni mwao waongozi wanao ongoa watu kwa amri yetu, walipo
subiri na wakawa na yakini na Ishara zetu.
|
Ayah 32:25 الأية
إِنَّ رَبَّكَ هُوَ يَفْصِلُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِيمَا كَانُوا فِيهِ
يَخْتَلِفُونَ
Inna rabbaka huwa yafsilu baynahumyawma alqiyamati feema kanoo feehiyakhtalifoon
Swahili
Hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye fafanua baina yao Siku ya Kiyama katika
waliyo kuwa wakikhitalifiana.
|
Ayah 32:26 الأية
أَوَلَمْ يَهْدِ لَهُمْ كَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَبْلِهِم مِّنَ الْقُرُونِ يَمْشُونَ
فِي مَسَاكِنِهِمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ ۖ أَفَلَا يَسْمَعُونَ
Awa lam yahdi lahum kam ahlakna minqablihim mina alqurooni yamshoona fee
masakinihim inna feethalika laayatin afala yasmaAAoon
Swahili
Je! Haijawabainikia kwamba kaumu ngapi tuliziangamiza kabla yao, nao wanapita
katika maskani zao hizo? Hakika katika hayo zipo Ishara. Basi, je, hawasikii?
|
Ayah 32:27 الأية
أَوَلَمْ يَرَوْا أَنَّا نَسُوقُ الْمَاءَ إِلَى الْأَرْضِ الْجُرُزِ فَنُخْرِجُ
بِهِ زَرْعًا تَأْكُلُ مِنْهُ أَنْعَامُهُمْ وَأَنفُسُهُمْ ۖ أَفَلَا يُبْصِرُونَ
Awa lam yaraw anna nasooqu almaaila al-ardi aljuruzi fanukhriju bihi
zarAAanta-kulu minhu anAAamuhum waanfusuhum afala yubsiroon
Swahili
Je! Hawaoni ya kwamba tunayapeleka maji kwenye ardhi kavu, kisha kwayo tunaitoa
mimea wanayo kula wanyama wao na wao wenyewe? Je! Hawaoni?
|
Ayah 32:28 الأية
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا الْفَتْحُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Wayaqooloona mata hatha alfathuin kuntum sadiqeen
Swahili
Wanasema: Ushindi huu ni lini, kama mnasema kweli?
|
Ayah 32:29 الأية
قُلْ يَوْمَ الْفَتْحِ لَا يَنفَعُ الَّذِينَ كَفَرُوا إِيمَانُهُمْ وَلَا هُمْ
يُنظَرُونَ
Qul yawma alfathi la yanfaAAuallatheena kafaroo eemanuhum wala hum yuntharoon
Swahili
Sema: Siku ya Ushindi, wale walio kufuru imani yao haitawafaa kitu, wala wao
hawatapewa muhula.
|
Ayah 32:30 الأية
فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ وَانتَظِرْ إِنَّهُم مُّنتَظِرُونَ
FaaAArid AAanhum wantathirinnahum muntathiroon
Swahili
Basi wapuuze, nawe ngonja; hakika wao wanangoja.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|