Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na
mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.
Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa,
haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai,
wala kufufuka.
Watasema: Subhanak, Umetakasika na upungufu! Haikutupasia sisi kuchukulia
walinzi badala yako, lakini Wewe uliwastarehesha wao na baba zao hata wakasahau
kukumbuka, na wakawa watu walio angamia.
Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa
wakila chakula, na wakenda masokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni
majaribio kwa wengine; je! Mtasubiri? Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuona.
NA WALISEMA wale wasio taraji kukutana nasi: Mbona sisi hatuteremshiwi Malaika
au hatumwoni Mola wetu Mlezi? Kwa yakini hawa wamejiona bora nafsi zao, na
wamepanda kichwa vikubwa mno!
Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiache miungu yetu, ingeli kuwa
hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapo iona adhabu, ni
nani aliye potea njia.
Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha
akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa
wamjuaye.
Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi
aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye
fanya hayo atapata madhara,
Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao
Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kusamehe, Mwenye kurehemu.