1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
اقْتَرَبَ لِلنَّاسِ حِسَابُهُمْ وَهُمْ فِي غَفْلَةٍ مُّعْرِضُونَ
Iqtaraba linnasi hisabuhumwahum fee ghaflatin muAAridoon
Swahili
IMEWAKARIBIA watu hisabu yao, nao wamo katika mghafala wanapuuza.
|
Ayah 21:2 الأية
مَا يَأْتِيهِم مِّن ذِكْرٍ مِّن رَّبِّهِم مُّحْدَثٍ إِلَّا اسْتَمَعُوهُ وَهُمْ
يَلْعَبُونَ
Ma ya/teehim min thikrin minrabbihim muhdathin illa istamaAAoohu wahumyalAAaboon
Swahili
Hayawafikilii mawaidha mapya kutoka kwa Mola wao Mlezi ila huyasikiliza na huku
wanafanya mchezo.
|
Ayah 21:3 الأية
لَاهِيَةً قُلُوبُهُمْ ۗ وَأَسَرُّوا النَّجْوَى الَّذِينَ ظَلَمُوا هَلْ هَٰذَا
إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ ۖ أَفَتَأْتُونَ السِّحْرَ وَأَنتُمْ تُبْصِرُونَ
Lahiyatan quloobuhum waasarroo annajwaallatheena thalamoo hal hatha illabasharun
mithlukum afata/toona assihra waantum tubsiroon
Swahili
Zimeghafilika nyoyo zao. Na wale walio dhulumu hunong'onezana kwa siri: Ni nani
ati huyu isipo kuwa ni binaadamu tu kama nyinyi! Mnauwendea uchawi hali nanyi
mnaona?
|
Ayah 21:4 الأية
قَالَ رَبِّي يَعْلَمُ الْقَوْلَ فِي السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۖ وَهُوَ السَّمِيعُ
الْعَلِيمُ
Qala rabbee yaAAlamu alqawla fee assama-iwal-ardi wahuwa assameeAAu alAAaleem
Swahili
Alisema: Mola wangu Mlezi anayajua yasemwayo mbinguni na katika ardhi. Na Yeye
ni Mwenye kusikia Mwenye kujua.
|
Ayah 21:5 الأية
بَلْ قَالُوا أَضْغَاثُ أَحْلَامٍ بَلِ افْتَرَاهُ بَلْ هُوَ شَاعِرٌ فَلْيَأْتِنَا
بِآيَةٍ كَمَا أُرْسِلَ الْأَوَّلُونَ
Bal qaloo adghathu ahlaminbali iftarahu bal huwa shaAAirun falya/tinabi-ayatin
kama orsila al-awwaloon
Swahili
Lakini wao walisema: Hizo ni ndoto za ovyo ovyo, bali amezizua tu, bali huyo ni
mtunga mashairi. Basi atuletee miujiza kama walivyo tumwa wale wa mwanzo.
|
Ayah 21:6 الأية
مَا آمَنَتْ قَبْلَهُم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا ۖ أَفَهُمْ يُؤْمِنُونَ
Ma amanat qablahum min qaryatinahlaknaha afahum yu/minoon
Swahili
Hawakuamini kabla yao watu wa mji tulio uangamiza. Basi, je, wataamini hawa?
|
Ayah 21:7 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ إِلَّا رِجَالًا نُّوحِي إِلَيْهِمْ ۖ فَاسْأَلُوا
أَهْلَ الذِّكْرِ إِن كُنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ
Wama arsalna qablaka illarijalan noohee ilayhim fas-aloo ahla aththikriin kuntum
la taAAlamoon
Swahili
Na kabla yako hatukuwatuma ila watu wanaume tulio wapa wahyi (ufunuo). Basi
waulizeni wenye ilimu ikiwa nyinyi hamjui.
|
Ayah 21:8 الأية
وَمَا جَعَلْنَاهُمْ جَسَدًا لَّا يَأْكُلُونَ الطَّعَامَ وَمَا كَانُوا خَالِدِينَ
Wama jaAAalnahum jasadan laya/kuloona attaAAama wama kanookhalideen
Swahili
Wala hatukuwafanya miili isiyo kula chakula, wala hawakuwa wenye kuishi milele.
|
Ayah 21:9 الأية
ثُمَّ صَدَقْنَاهُمُ الْوَعْدَ فَأَنجَيْنَاهُمْ وَمَن نَّشَاءُ وَأَهْلَكْنَا
الْمُسْرِفِينَ
Thumma sadaqnahumu alwaAAdafaanjaynahum waman nashao waahlaknaalmusrifeen
Swahili
Kisha tukawatimizia miadi, na tukawaokoa wao na tulio wataka, na tukawateketeza
walio pita mipaka.
|
Ayah 21:10 الأية
لَقَدْ أَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَابًا فِيهِ ذِكْرُكُمْ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Laqad anzalna ilaykum kitabanfeehi thikrukum afala taAAqiloon
Swahili
Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je!
Hamzingatii?
|
Ayah 21:11 الأية
وَكَمْ قَصَمْنَا مِن قَرْيَةٍ كَانَتْ ظَالِمَةً وَأَنشَأْنَا بَعْدَهَا قَوْمًا
آخَرِينَ
Wakam qasamna min qaryatin kanatthalimatan waansha/na baAAdahaqawman akhareen
Swahili
Na mingapi katika miji iliyo kuwa ikidhulumu tumeiteketeza, na tukawasimamisha
baada yao watu wengine.
|
Ayah 21:12 الأية
فَلَمَّا أَحَسُّوا بَأْسَنَا إِذَا هُم مِّنْهَا يَرْكُضُونَ
Falamma ahassoo ba/sanaitha hum minha yarkudoon
Swahili
Basi walipo ihisi adhabu yetu, mara wakaanza kukimbia.
|
Ayah 21:13 الأية
لَا تَرْكُضُوا وَارْجِعُوا إِلَىٰ مَا أُتْرِفْتُمْ فِيهِ وَمَسَاكِنِكُمْ
لَعَلَّكُمْ تُسْأَلُونَ
La tarkudoo warjiAAooila ma otriftum feehi wamasakinikumlaAAallakum tus-aloon
Swahili
Msikimbie! Na rejeeni kwenye zile zile starehe zenu, na maskani zenu, mpate
kusailiwa!
|
Ayah 21:14 الأية
قَالُوا يَا وَيْلَنَا إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ
Qaloo ya waylana innakunna thalimeen
Swahili
Wakasema: Ole wetu! Hakika sisi tulikuwa madhaalimu.
|
Ayah 21:15 الأية
فَمَا زَالَت تِّلْكَ دَعْوَاهُمْ حَتَّىٰ جَعَلْنَاهُمْ حَصِيدًا خَامِدِينَ
Fama zalat tilka daAAwahumhatta jaAAalnahum haseedan khamideen
Swahili
Hakikuacha hicho kuwa kilio chao mpaka tukawafanya kama walio fyekwa,
wamezimika.
|
Ayah 21:16 الأية
وَمَا خَلَقْنَا السَّمَاءَ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا لَاعِبِينَ
Wama khalaqna assamaawal-arda wama baynahuma laAAibeen
Swahili
Na hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yao kwa mchezo.
|
Ayah 21:17 الأية
لَوْ أَرَدْنَا أَن نَّتَّخِذَ لَهْوًا لَّاتَّخَذْنَاهُ مِن لَّدُنَّا إِن كُنَّا
فَاعِلِينَ
Law aradna an nattakhithalahwan lattakhathnahu min ladunna inkunna faAAileen
Swahili
Kama tungeli taka kufanya mchezo tunge jifanyia Sisi wenyewe, lau kwamba tungeli
kuwa ni wafanyao mchezo.
|
Ayah 21:18 الأية
بَلْ نَقْذِفُ بِالْحَقِّ عَلَى الْبَاطِلِ فَيَدْمَغُهُ فَإِذَا هُوَ زَاهِقٌ ۚ
وَلَكُمُ الْوَيْلُ مِمَّا تَصِفُونَ
Bal naqthifu bilhaqqiAAala albatili fayadmaghuhu fa-itha huwa zahiqunwalakumu
alwaylu mimma tasifoon
Swahili
Bali tunaitupa kweli juu ya uwongo ikauvunja na mara ukatoweka. Na ole wenu kwa
mnayo yazua.
|
Ayah 21:19 الأية
وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ
عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ
Walahu man fee assamawatiwal-ardi waman AAindahu la yastakbiroonaAAan
AAibadatihi wala yastahsiroon
Swahili
Na ni vyake Yeye tu Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na katika ardhi. Na
walioko kwake hawafanyi kiburi wakaacha kumuabudu, wala hawachoki.
|
Ayah 21:20 الأية
يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ
Yusabbihoona allayla wannaharala yafturoon
Swahili
Wanamtakasa usiku na mchana, wala hawanyong'onyei.
|
Ayah 21:21 الأية
أَمِ اتَّخَذُوا آلِهَةً مِّنَ الْأَرْضِ هُمْ يُنشِرُونَ
Ami ittakhathoo alihatan minaal-ardi hum yunshiroon
Swahili
Au wamepata miungu katika ardhi inayo fufua?
|
Ayah 21:22 الأية
لَوْ كَانَ فِيهِمَا آلِهَةٌ إِلَّا اللهُ لَفَسَدَتَا ۚ فَسُبْحَانَ اللهِ
رَبِّ الْعَرْشِ عَمَّا يَصِفُونَ
Law kana feehima alihatunilla Allahu lafasadata fasubhana Allahirabbi alAAarshi
AAamma yasifoon
Swahili
Lau wangeli kuwamo humo miungu wengine isipo kuwa Mwenyezi Mungu basi bila ya
shaka hizo mbingu na ardhi zingeli fisidika. Subahana 'Llah Ametakasika Mwenyezi
Mungu, Bwana wa A'rshi (Kiti cha Enzi), na hayo wanayo yazua.
|
Ayah 21:23 الأية
لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ
La yus-alu AAamma yafAAaluwahum yus-aloon
Swahili
Yeye hahojiwi kwa ayatendayo, na wao ndio wanao hojiwa kwa wayatendayo.
|
Ayah 21:24 الأية
أَمِ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً ۖ قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ ۖ هَٰذَا ذِكْرُ
مَن مَّعِيَ وَذِكْرُ مَن قَبْلِي ۗ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ الْحَقَّ ۖ
فَهُم مُّعْرِضُونَ
Ami ittakhathoo min doonihi alihatanqul hatoo burhanakum hatha thikru manmaAAiya
wathikru man qablee bal aktharuhum layaAAlamoona alhaqqa fahum muAAridoon
Swahili
Au wanawaabudu miungu mingine badala yake? Sema: Leteni ushahidi wenu! Haya ni
ukumbusho wa hawa walio nami, na ukumbusho wa walio kabla yangu. Lakini wengi
wao hawaijui kweli, na kwa hivyo wanapuuza.
|
Ayah 21:25 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا مِن قَبْلِكَ مِن رَّسُولٍ إِلَّا نُوحِي إِلَيْهِ أَنَّهُ لَا
إِلَٰهَ إِلَّا أَنَا فَاعْبُدُونِ
Wama arsalna min qablika minrasoolin illa noohee ilayhi annahu la ilahailla ana
faAAbudoon
Swahili
Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu
isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.
|
Ayah 21:26 الأية
وَقَالُوا اتَّخَذَ الرَّحْمَٰنُ وَلَدًا ۗ سُبْحَانَهُ ۚ بَلْ عِبَادٌ
مُّكْرَمُونَ
Waqaloo ittakhatha arrahmanuwaladan subhanahu bal AAibadun mukramoon
Swahili
Na wanasema: Arrahman, Mwingi wa Rehema, ana mwana! Subhanahu, Ametakasika na
hayo! Bali hao (wanao waita wana) ni watumwa walio tukuzwa.
|
Ayah 21:27 الأية
لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ
La yasbiqoonahu bilqawliwahum bi-amrihi yaAAmaloon
Swahili
Hawamtangulii kwa neno, nao wanafanya amri zake.
|
Ayah 21:28 الأية
يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يَشْفَعُونَ إِلَّا لِمَنِ
ارْتَضَىٰ وَهُم مِّنْ خَشْيَتِهِ مُشْفِقُونَ
YaAAlamu ma bayna aydeehim wamakhalfahum wala yashfaAAoona illa limani
irtadawahum min khashyatihi mushfiqoon
Swahili
Anayajua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao. Wala hawamwombei yeyote ila yule
anaye mridhia Yeye, nao kwa ajili ya kumwogopa wananyenyekea.
|
Ayah 21:29 الأية
وَمَن يَقُلْ مِنْهُمْ إِنِّي إِلَٰهٌ مِّن دُونِهِ فَذَٰلِكَ نَجْزِيهِ جَهَنَّمَ
ۚ كَذَٰلِكَ نَجْزِي الظَّالِمِينَ
Waman yaqul minhum innee ilahun mindoonihi fathalika najzeehi jahannama
kathalikanajzee aththalimeen
Swahili
Na yeyote kati yao atakaye sema: Mimi ni mungu, badala yake, basi huyo tutamlipa
malipo yake Jahannamu. Hivyo ndivyo tuwalipavyo wenye kudhulumu.
|
Ayah 21:30 الأية
أَوَلَمْ يَرَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ كَانَتَا
رَتْقًا فَفَتَقْنَاهُمَا ۖ وَجَعَلْنَا مِنَ الْمَاءِ كُلَّ شَيْءٍ حَيٍّ ۖ
أَفَلَا يُؤْمِنُونَ
Awa lam yara allatheenakafaroo anna assamawati wal-ardakanata ratqan
fafataqnahuma wajaAAalnamina alma-i kulla shay-in hayyin afalayu/minoon
Swahili
Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana,
kisha Sisi tukazibabandua? Na tukajaalia kwa maji kila kilicho hai? Basi je,
hawaamini?
|
Ayah 21:31 الأية
وَجَعَلْنَا فِي الْأَرْضِ رَوَاسِيَ أَن تَمِيدَ بِهِمْ وَجَعَلْنَا فِيهَا
فِجَاجًا سُبُلًا لَّعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ
WajaAAalna fee al-ardi rawasiyaan tameeda bihim wajaAAalna feeha fijajansubulan
laAAallahum yahtadoon
Swahili
Na tukaweka katika ardhi milima iliyo thibiti ili isiwayumbishe, na tukaweka
humo njia pana ili wapate kuongoka.
|
Ayah 21:32 الأية
وَجَعَلْنَا السَّمَاءَ سَقْفًا مَّحْفُوظًا ۖ وَهُمْ عَنْ آيَاتِهَا مُعْرِضُونَ
WajaAAalna assamaasaqfan mahfoothan wahum AAan ayatihamuAAridoon
Swahili
Na tukaifanya mbingu kuwa dari iliyo hifadhiwa, lakini wanazipuuza Ishara zake.
|
Ayah 21:33 الأية
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ فِي
فَلَكٍ يَسْبَحُونَ
Wahuwa allathee khalaqa allayla wannaharawashshamsa walqamara kullun fee falakin
yasbahoon
Swahili
Na Yeye ndiye aliye umba usiku na mchana na jua na mwezi, vyote katika anga
vinaogelea.
|
Ayah 21:34 الأية
وَمَا جَعَلْنَا لِبَشَرٍ مِّن قَبْلِكَ الْخُلْدَ ۖ أَفَإِن مِّتَّ فَهُمُ
الْخَالِدُونَ
Wama jaAAalna libasharin minqablika alkhulda afa-in mitta fahumu alkhalidoon
Swahili
Nasi hatukumjaalia mwanaadamu yeyote kabla yako kuwa na maisha ya milele. Basi
je! Ukifa wewe, wao wataishi milele?
|
Ayah 21:35 الأية
كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَنَبْلُوكُم بِالشَّرِّ وَالْخَيْرِ فِتْنَةً
ۖ وَإِلَيْنَا تُرْجَعُونَ
Kullu nafsin tha-iqatu almawtiwanablookum bishsharri walkhayri fitnatanwa-ilayna
turjaAAoon
Swahili
Kila nafsi itaonja mauti; na tunakujaribuni kwa mtihani wa shari na kheri. Na
kwetu Sisi mtarejeshwa.
|
Ayah 21:36 الأية
وَإِذَا رَآكَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا
الَّذِي يَذْكُرُ آلِهَتَكُمْ وَهُم بِذِكْرِ الرَّحْمَٰنِ هُمْ كَافِرُونَ
Wa-itha raaka allatheenakafaroo in yattakhithoonaka illa huzuwan ahathaallathee
yathkuru alihatakum wahum bithikriarrahmani hum kafiroon
Swahili
Na wakikuona walio kufuru hawakufanyi wewe ila ni kitu cha maskhara tu,
(wakisema): Je! Ndiye huyu anaye itaja miungu yenu? Na hali wao wanakataa
kumkumbuka Arrahman, Mwingi wa Rehema!
|
Ayah 21:37 الأية
خُلِقَ الْإِنسَانُ مِنْ عَجَلٍ ۚ سَأُرِيكُمْ آيَاتِي فَلَا تَسْتَعْجِلُونِ
Khuliqa al-insanu min AAajalinsaoreekum ayatee fala tastaAAjiloon
Swahili
Mwanaadamu ameumbwa na haraka. Nitakuonyesheni Ishara zangu. Basi msinihimize.
|
Ayah 21:38 الأية
وَيَقُولُونَ مَتَىٰ هَٰذَا الْوَعْدُ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Wayaqooloona mata hathaalwaAAdu in kuntum sadiqeen
Swahili
Na wanasema: Ahadi hii itatokea lini, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
|
Ayah 21:39 الأية
لَوْ يَعْلَمُ الَّذِينَ كَفَرُوا حِينَ لَا يَكُفُّونَ عَن وُجُوهِهِمُ النَّارَ
وَلَا عَن ظُهُورِهِمْ وَلَا هُمْ يُنصَرُونَ
Law yaAAlamu allatheena kafaroo heenala yakuffoona AAan wujoohihimu annara
walaAAan thuhoorihim wala hum yunsaroon
Swahili
Lau wangeli jua wale walio kufuru wakati ambao hawatauzuia Moto kwenye nyuso zao
wala migongo yao, na wala hawatanusuriwa!
|
Ayah 21:40 الأية
بَلْ تَأْتِيهِم بَغْتَةً فَتَبْهَتُهُمْ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ رَدَّهَا وَلَا هُمْ
يُنظَرُونَ
Bal ta/teehim baghtatan fatabhatuhum falayastateeAAoona raddaha wala hum
yuntharoon
Swahili
Bali utawafikia kwa ghafla, na utawashitua na wala hawataweza kuurudisha, wala
hawatapewa muhula!
|
Ayah 21:41 الأية
وَلَقَدِ اسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَحَاقَ بِالَّذِينَ سَخِرُوا مِنْهُم
مَّا كَانُوا بِهِ يَسْتَهْزِئُونَ
Walaqadi istuhzi-a birusulin min qablika fahaqabillatheena sakhiroo minhum ma
kanoobihi yastahzi-oon
Swahili
Na Mitume walio kabla yako walikwisha dhihakiwa. Kwa hivyo wale walio wafanyia
maskhara yaliwafika yale waliyo kuwa wakiyafanyia dhihaka.
|
Ayah 21:42 الأية
قُلْ مَن يَكْلَؤُكُم بِاللَّيْلِ وَالنَّهَارِ مِنَ الرَّحْمَٰنِ ۗ بَلْ هُمْ عَن
ذِكْرِ رَبِّهِم مُّعْرِضُونَ
Qul man yaklaokum billayli wannaharimina arrahmani bal hum AAan thikrirabbihim
muAAridoon
Swahili
Sema: Nani anaye kulindeni usiku na mchana na Arrahmani Mwingi wa Rehema? Bali
wao wanapuuza kumkumbuka Mola wao Mlezi.
|
Ayah 21:43 الأية
أَمْ لَهُمْ آلِهَةٌ تَمْنَعُهُم مِّن دُونِنَا ۚ لَا يَسْتَطِيعُونَ نَصْرَ
أَنفُسِهِمْ وَلَا هُم مِّنَّا يُصْحَبُونَ
Am lahum alihatun tamnaAAuhum mindoonina la yastateeAAoona nasraanfusihim wala
hum minna yushaboon
Swahili
Au wao wanao miungu watao weza kuwakinga nasi? Hao hawawezi kujinusuru nafsi
zao, wala hawatalindwa nasi!
|
Ayah 21:44 الأية
بَلْ مَتَّعْنَا هَٰؤُلَاءِ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ طَالَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۗ
أَفَلَا يَرَوْنَ أَنَّا نَأْتِي الْأَرْضَ نَنقُصُهَا مِنْ أَطْرَافِهَا ۚ
أَفَهُمُ الْغَالِبُونَ
Bal mattaAAna haola-iwaabaahum hatta talaAAalayhimu alAAumuru afala yarawna anna
na/teeal-arda nanqusuha min atrafihaafahumu alghaliboon
Swahili
Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka umri ukawa mrefu kwao. Je, hawaoni
ya kwamba Sisi tunaifikia ardhi tukiipunguza ncha zake? Basi je! Hao ni wenye
kushinda?
|
Ayah 21:45 الأية
قُلْ إِنَّمَا أُنذِرُكُم بِالْوَحْيِ ۚ وَلَا يَسْمَعُ الصُّمُّ الدُّعَاءَ إِذَا
مَا يُنذَرُونَ
Qul innama onthirukum bilwahyiwala yasmaAAu assummu adduAAaaitha ma yuntharoon
Swahili
Sema: Mimi nakuonyeni kwa Wahyi. Na viziwi hawasikii wito wanapo onywa.
|
Ayah 21:46 الأية
وَلَئِن مَّسَّتْهُمْ نَفْحَةٌ مِّنْ عَذَابِ رَبِّكَ لَيَقُولُنَّ يَا وَيْلَنَا
إِنَّا كُنَّا ظَالِمِينَ
Wala-in massat-hum nafhatun min AAathabirabbika layaqoolunna ya waylana inna
kunnathalimeen
Swahili
Na wanapo guswa na mpulizo mmoja tu wa adhabu itokayo kwa Mola wako Mlezi, bila
ya shaka wao husema: Ole wetu! Hakika tulikuwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 21:47 الأية
وَنَضَعُ الْمَوَازِينَ الْقِسْطَ لِيَوْمِ الْقِيَامَةِ فَلَا تُظْلَمُ نَفْسٌ
شَيْئًا ۖ وَإِن كَانَ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ أَتَيْنَا بِهَا ۗ
وَكَفَىٰ بِنَا حَاسِبِينَ
WanadaAAu almawazeena alqistaliyawmi alqiyamati fala tuthlamunafsun shay-an
wa-in kana mithqala habbatinmin khardalin atayna biha wakafa binahasibeen
Swahili
Nasi tutaweka mizani za uadilifu kwa Siku ya Kiyama. Basi nafsi haitadhulumiwa
kitu chochote. Hata ikiwa ni uzito wa chembe ya khardali tutaileta. Nasi
tunatosha kuwa washika hisabu.
|
Ayah 21:48 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَىٰ وَهَارُونَ الْفُرْقَانَ وَضِيَاءً وَذِكْرًا
لِّلْمُتَّقِينَ
Walaqad atayna moosawaharoona alfurqana wadiyaan wathikranlilmuttaqeen
Swahili
Na kwa yakini tuliwapa Musa na Haaruni kipambanuzi, na mwangaza, na makumbusho
kwa wachamngu,
|
Ayah 21:49 الأية
الَّذِينَ يَخْشَوْنَ رَبَّهُم بِالْغَيْبِ وَهُم مِّنَ السَّاعَةِ مُشْفِقُونَ
Allatheena yakhshawna rabbahum bilghaybiwahum mina assaAAati mushfiqoon
Swahili
Ambao wanamkhofu Mola wao Mlezi faraghani, na wanaiogopa Saa ya Kiyama.
|
Ayah 21:50 الأية
وَهَٰذَا ذِكْرٌ مُّبَارَكٌ أَنزَلْنَاهُ ۚ أَفَأَنتُمْ لَهُ مُنكِرُونَ
Wahatha thikrun mubarakunanzalnahu afaantum lahu munkiroon
Swahili
Na haya ni makumbusho yaliyo barikiwa, tuliyo yateremsha. Basi je! Mnayakataa?
|
Ayah 21:51 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا إِبْرَاهِيمَ رُشْدَهُ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِ عَالِمِينَ
Walaqad atayna ibraheemarushdahu min qablu wakunna bihi AAalimeen
Swahili
Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wake zamani, na tulikuwa tunamjua.
|
Ayah 21:52 الأية
إِذْ قَالَ لِأَبِيهِ وَقَوْمِهِ مَا هَٰذِهِ التَّمَاثِيلُ الَّتِي أَنتُمْ لَهَا
عَاكِفُونَ
Ith qala li-abeehi waqawmihi mahathihi attamatheelu allatee antum lahaAAakifoon
Swahili
Alipo mwambia baba yake na watu wake: Ni nini haya masanamu mnayo yashughulikia
kuyaabudu?
|
Ayah 21:53 الأية
قَالُوا وَجَدْنَا آبَاءَنَا لَهَا عَابِدِينَ
Qaloo wajadna abaanalaha AAabideen
Swahili
Wakasema: Tumewakuta baba zetu wakiyaabudu.
|
Ayah 21:54 الأية
قَالَ لَقَدْ كُنتُمْ أَنتُمْ وَآبَاؤُكُمْ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Qala laqad kuntum antum waabaokumfee dalalin mubeen
Swahili
Akasema: Bila ya shaka nyinyi na baba zenu mmekuwa katika upotofu ulio dhaahiri.
|
Ayah 21:55 الأية
قَالُوا أَجِئْتَنَا بِالْحَقِّ أَمْ أَنتَ مِنَ اللَّاعِبِينَ
Qaloo aji/tana bilhaqqiam anta mina allaAAibeen
Swahili
Wakasema: Je! Umetujia kwa maneno ya kweli au wewe ni katika wachezao tu?
|
Ayah 21:56 الأية
قَالَ بَل رَّبُّكُمْ رَبُّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ الَّذِي فَطَرَهُنَّ وَأَنَا
عَلَىٰ ذَٰلِكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ
Qala bal rabbukum rabbu assamawatiwal-ardi allathee fatarahunna waanaAAala
thalikum mina ashshahideen
Swahili
Akasema: Bali Mola wenu Mlezi ni Mola Mlezi wa mbingu na ardhi ambaye ndiye
aliye ziumba. Na mimi ni katika wenye kuyashuhudia hayo.
|
Ayah 21:57 الأية
وَتَاللهِ لَأَكِيدَنَّ أَصْنَامَكُم بَعْدَ أَن تُوَلُّوا مُدْبِرِينَ
Watallahi laakeedanna asnamakumbaAAda an tuwalloo mudbireen
Swahili
Na Wallahi! Nitayafanyia vitimbi masanamu yenu haya baada ya mkisha geuka kwenda
zenu.
|
Ayah 21:58 الأية
فَجَعَلَهُمْ جُذَاذًا إِلَّا كَبِيرًا لَّهُمْ لَعَلَّهُمْ إِلَيْهِ يَرْجِعُونَ
FajaAAalahum juthathan illakabeeran lahum laAAallahum ilayhi yarjiAAoon
Swahili
Basi akayavunja vipande vipande, ila kubwa lao, ili wao walirudie.
|
Ayah 21:59 الأية
قَالُوا مَن فَعَلَ هَٰذَا بِآلِهَتِنَا إِنَّهُ لَمِنَ الظَّالِمِينَ
Qaloo man faAAala hatha bi-alihatinainnahu lamina aththalimeen
Swahili
Wakasema: Nani aliye ifanyia haya miungu yetu? Hakika huyu ni katika walio
dhulumu.
|
Ayah 21:60 الأية
قَالُوا سَمِعْنَا فَتًى يَذْكُرُهُمْ يُقَالُ لَهُ إِبْرَاهِيمُ
Qaloo samiAAna fatan yathkuruhumyuqalu lahu ibraheem
Swahili
Wakasema: Tumemsikia kijana mmoja akiwataja. Anaitwa Ibrahim.
|
Ayah 21:61 الأية
قَالُوا فَأْتُوا بِهِ عَلَىٰ أَعْيُنِ النَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَشْهَدُونَ
Qaloo fa/too bihi AAalaaAAyuni annasi laAAallahum yashhadoon
Swahili
Wakasema: Mleteni mbele ya macho ya watu, wapate kumshuhudia!
|
Ayah 21:62 الأية
قَالُوا أَأَنتَ فَعَلْتَ هَٰذَا بِآلِهَتِنَا يَا إِبْرَاهِيمُ
Qaloo aanta faAAalta hatha bi-alihatinaya ibraheem
Swahili
Wakasema: Je! Wewe umeifanyia haya miungu yetu, ewe Ibrahim?
|
Ayah 21:63 الأية
قَالَ بَلْ فَعَلَهُ كَبِيرُهُمْ هَٰذَا فَاسْأَلُوهُمْ إِن كَانُوا يَنطِقُونَ
Qala bal faAAalahu kabeeruhum hathafas-aloohum in kanoo yantiqoon
Swahili
Akasema: Bali amefanya hayo huyu mkubwa wao. Basi waulizeni ikiwa wanaweza
kutamka.
|
Ayah 21:64 الأية
فَرَجَعُوا إِلَىٰ أَنفُسِهِمْ فَقَالُوا إِنَّكُمْ أَنتُمُ الظَّالِمُونَ
FarajaAAoo ila anfusihim faqalooinnakum antumu aththalimoon
Swahili
Basi wakajirudi nafsi zao, wakasema: Hakika nyinyi mlikuwa madhaalimu!
|
Ayah 21:65 الأية
ثُمَّ نُكِسُوا عَلَىٰ رُءُوسِهِمْ لَقَدْ عَلِمْتَ مَا هَٰؤُلَاءِ يَنطِقُونَ
Thumma nukisoo AAala ruoosihim laqadAAalimta ma haola-i yantiqoon
Swahili
Kisha wakarejea kwenye ule ule upotovu wao wakasema: Wewe unajua kwamba hawa
hawesemi.
|
Ayah 21:66 الأية
قَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْئًا وَلَا
يَضُرُّكُمْ
Qala afataAAbudoona min dooni Allahima la yanfaAAukum shay-an wala yadurrukum
Swahili
Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu
wala kukudhuruni?
|
Ayah 21:67 الأية
أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Offin lakum walima taAAbudoona mindooni Allahi afala taAAqiloon
Swahili
Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi
hamtii akilini?
|
Ayah 21:68 الأية
قَالُوا حَرِّقُوهُ وَانصُرُوا آلِهَتَكُمْ إِن كُنتُمْ فَاعِلِينَ
Qaloo harriqoohu wansurooalihatakum in kuntum faAAileen
Swahili
Wakasema: Mchomeni moto, na muinusuru miungu yenu, ikiwa nyinyi ni watendao
jambo!
|
Ayah 21:69 الأية
قُلْنَا يَا نَارُ كُونِي بَرْدًا وَسَلَامًا عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ
Qulna ya naru kooneebardan wasalaman AAala ibraheem
Swahili
Sisi tukasema: Ewe moto! Kuwa baridi na salama kwa Ibrahim!
|
Ayah 21:70 الأية
وَأَرَادُوا بِهِ كَيْدًا فَجَعَلْنَاهُمُ الْأَخْسَرِينَ
Waaradoo bihi kaydan fajaAAalnahumual-akhsareen
Swahili
Wao walimkusudia maovu, lakini Sisi tukawafanya wao ndio walio khasiri.
|
Ayah 21:71 الأية
وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ
Wanajjaynahu walootan ilaal-ardi allatee barakna feeha lilAAalameen
Swahili
Na tukamwokoa yeye na Luut'i tukawapeleka kwenye nchi tulio ibariki kwa ajili ya
walimwengu wote.
|
Ayah 21:72 الأية
وَوَهَبْنَا لَهُ إِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ نَافِلَةً ۖ وَكُلًّا جَعَلْنَا صَالِحِينَ
Wawahabna lahu ishaqawayaAAqooba nafilatan wakullan jaAAalna saliheen
Swahili
Naye tukampa Is-haq, na Yaaqub kuwa ni ziada. Na wote tukawajaalia wawe watu
wema.
|
Ayah 21:73 الأية
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَهْدُونَ بِأَمْرِنَا وَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِمْ فِعْلَ
الْخَيْرَاتِ وَإِقَامَ الصَّلَاةِ وَإِيتَاءَ الزَّكَاةِ ۖ وَكَانُوا لَنَا
عَابِدِينَ
WajaAAalnahum a-immatan yahdoonabi-amrina waawhayna ilayhim fiAAla
alkhayratiwa-iqama assalati wa-eetaa azzakatiwakanoo lana AAabideen
Swahili
Na tukawafanya maimamu wakiongoa watu kwa amri yetu. Na tukawafunulia watende
kheri, na washike Sala, na watoe Zaka; na walikuwa wanatuabudu Sisi tu.
|
Ayah 21:74 الأية
وَلُوطًا آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْقَرْيَةِ الَّتِي
كَانَت تَّعْمَلُ الْخَبَائِثَ ۗ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَاسِقِينَ
Walootan ataynahu hukmanwaAAilman wanajjaynahu mina alqaryati allatee
kanattaAAmalu alkhaba-itha innahum kanoo qawma saw-in fasiqeen
Swahili
Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa na ule mji ulio kuwa ukifanya
maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu.
|
Ayah 21:75 الأية
وَأَدْخَلْنَاهُ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُ مِنَ الصَّالِحِينَ
Waadkhalnahu fee rahmatinainnahu mina assaliheen
Swahili
Na tukamuingiza katika rehema yetu. Hakika yeye ni miongoni mwa watenda mema.
|
Ayah 21:76 الأية
وَنُوحًا إِذْ نَادَىٰ مِن قَبْلُ فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَنَجَّيْنَاهُ وَأَهْلَهُ
مِنَ الْكَرْبِ الْعَظِيمِ
Wanoohan ith nadamin qablu fastajabna lahu fanajjaynahuwaahlahu mina alkarbi
alAAatheem
Swahili
Na Nuhu alipo ita zamani, nasi tukamuitikia, na tukamwokoa yeye na watu wake
kutokana na shida kubwa.
|
Ayah 21:77 الأية
وَنَصَرْنَاهُ مِنَ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا
قَوْمَ سَوْءٍ فَأَغْرَقْنَاهُمْ أَجْمَعِينَ
Wanasarnahu mina alqawmi allatheenakaththaboo bi-ayatina innahum kanooqawma
saw-in faaghraqnahum ajmaAAeen
Swahili
Na tukamnusuru na watu walio zikanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu
wabaya. Basi tukawazamisha wote.
|
Ayah 21:78 الأية
وَدَاوُودَ وَسُلَيْمَانَ إِذْ يَحْكُمَانِ فِي الْحَرْثِ إِذْ نَفَشَتْ فِيهِ
غَنَمُ الْقَوْمِ وَكُنَّا لِحُكْمِهِمْ شَاهِدِينَ
Wadawooda wasulaymana ithyahkumani fee alharthi ith nafashatfeehi ghanamu
alqawmi wakunna lihukmihim shahideen
Swahili
Na Daud na Suleiman walipo kata hukumu katika kadhiya ya konde walipo lisha humo
mbuzi wa watu usiku. Na Sisi tulikuwa wenye kushuhudia hukumu yao hiyo.
|
Ayah 21:79 الأية
فَفَهَّمْنَاهَا سُلَيْمَانَ ۚ وَكُلًّا آتَيْنَا حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَسَخَّرْنَا
مَعَ دَاوُودَ الْجِبَالَ يُسَبِّحْنَ وَالطَّيْرَ ۚ وَكُنَّا فَاعِلِينَ
Fafahhamnaha sulaymanawakullan atayna hukman waAAilman wasakhkharnamaAAa dawooda
aljibala yusabbihna wattayrawakunna faAAileen
Swahili
Tukamfahamisha Suleiman. Na kila mmoja wao tulimpa hukumu na ilimu. Na
tuliifanya milima na ndege kuwa pamoja na Daud imnyenyekee na imtakase Mwenyezi
Mungu. Na Sisi ndio tulio fanya hayo.
|
Ayah 21:80 الأية
وَعَلَّمْنَاهُ صَنْعَةَ لَبُوسٍ لَّكُمْ لِتُحْصِنَكُم مِّن بَأْسِكُمْ ۖ فَهَلْ
أَنتُمْ شَاكِرُونَ
WaAAallamnahu sanAAatalaboosin lakum lituhsinakum min ba/sikum fahal antum
shakiroon
Swahili
Na tukamfundisha kuunda mavazi ya vita kwa ajili yenu ili yakuhifadhini katika
kupigana kwenu. Je! Mtakuwa wenye kushukuru?
|
Ayah 21:81 الأية
وَلِسُلَيْمَانَ الرِّيحَ عَاصِفَةً تَجْرِي بِأَمْرِهِ إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي
بَارَكْنَا فِيهَا ۚ وَكُنَّا بِكُلِّ شَيْءٍ عَالِمِينَ
Walisulaymana arreehaAAasifatan tajree bi-amrihi ila al-ardiallatee barakna
feeha wakunna bikullishay-in AAalimeen
Swahili
Na tukamsahilishia Suleiman upepo wa kimbunga wendao kwa amri yake kwenye ardhi
tuliyo ibarikia. Na Sisi ndio tunao jua kila kitu.
|
Ayah 21:82 الأية
وَمِنَ الشَّيَاطِينِ مَن يَغُوصُونَ لَهُ وَيَعْمَلُونَ عَمَلًا دُونَ ذَٰلِكَ ۖ
وَكُنَّا لَهُمْ حَافِظِينَ
Wamina ashshayateeni manyaghoosoona lahu wayaAAmaloona AAamalan doona
thalikawakunna lahum hafitheen
Swahili
Na pia mashet'ani wanao mpigia mbizi na kufanya kazi nyenginezo. Na Sisi
tulikuwa walinzi wao.
|
Ayah 21:83 الأية
وَأَيُّوبَ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ أَنِّي مَسَّنِيَ الضُّرُّ وَأَنتَ أَرْحَمُ
الرَّاحِمِينَ
Waayyooba ith nadarabbahu annee massaniya addurru waanta arhamuarrahimeen
Swahili
Na Ayyubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: Mimi yamenipata madhara. Na
Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu.
|
Ayah 21:84 الأية
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ فَكَشَفْنَا مَا بِهِ مِن ضُرٍّ ۖ وَآتَيْنَاهُ أَهْلَهُ
وَمِثْلَهُم مَّعَهُمْ رَحْمَةً مِّنْ عِندِنَا وَذِكْرَىٰ لِلْعَابِدِينَ
Fastajabna lahu fakashafnama bihi min durrin waataynahu ahlahuwamithlahum
maAAahum rahmatan min AAindina wathikralilAAabideen
Swahili
Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu
wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa
wafanyao ibada.
|
Ayah 21:85 الأية
وَإِسْمَاعِيلَ وَإِدْرِيسَ وَذَا الْكِفْلِ ۖ كُلٌّ مِّنَ الصَّابِرِينَ
Wa-ismaAAeela wa-idreesa wathaalkifli kullun mina assabireen
Swahili
Na Ismail, na Idris, na Dhulkifli - wote walikuwa miongoni mwa wanao subiri.
|
Ayah 21:86 الأية
وَأَدْخَلْنَاهُمْ فِي رَحْمَتِنَا ۖ إِنَّهُم مِّنَ الصَّالِحِينَ
Waadkhalnahum fee rahmatinainnahum mina assaliheen
Swahili
Na tukawaingiza katika rehema yetu. Hakika wao walikuwa katika watu wema.
|
Ayah 21:87 الأية
وَذَا النُّونِ إِذ ذَّهَبَ مُغَاضِبًا فَظَنَّ أَن لَّن نَّقْدِرَ عَلَيْهِ
فَنَادَىٰ فِي الظُّلُمَاتِ أَن لَّا إِلَٰهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي
كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ
Watha annooni ith thahabamughadiban fathanna an lan naqdira AAalayhifanada fee
aththulumatian la ilaha illa anta subhanaka inneekuntu mina aththalimeen
Swahili
Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na
uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka
Uliye takasika. Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 21:88 الأية
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي
الْمُؤْمِنِينَ
Fastajabna lahu wanajjaynahumina alghammi wakathalika nunjee almu/mineen
Swahili
Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo
waokoa Waumini.
|
Ayah 21:89 الأية
وَزَكَرِيَّا إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُ رَبِّ لَا تَذَرْنِي فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ
الْوَارِثِينَ
Wazakariyya ith nadarabbahu rabbi la tatharnee fardan waanta khayru alwaritheen
Swahili
Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu,
na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi.
|
Ayah 21:90 الأية
فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَوَهَبْنَا لَهُ يَحْيَىٰ وَأَصْلَحْنَا لَهُ زَوْجَهُ ۚ
إِنَّهُمْ كَانُوا يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَيَدْعُونَنَا رَغَبًا وَرَهَبًا
ۖ وَكَانُوا لَنَا خَاشِعِينَ
Fastajabna lahu wawahabnalahu yahya waaslahna lahuzawjahu innahum kanoo
yusariAAoona fee alkhayratiwayadAAoonana raghaban warahaban wakanoo
lanakhashiAAeen
Swahili
Basi tukamwitikia, na tukampa Yahya na tukamponyeshea mkewe. Hakika wao walikuwa
wepesi wa kutenda mema, na wakituomba kwa shauku na khofu. Nao walikuwa
wakitunyenyekea.
|
Ayah 21:91 الأية
وَالَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهَا مِن رُّوحِنَا وَجَعَلْنَاهَا
وَابْنَهَا آيَةً لِّلْعَالَمِينَ
Wallatee ahsanat farjahafanafakhna feeha min roohinawajaAAalnaha wabnaha
ayatanlilAAalameen
Swahili
Na mwanamke aliye linda uke wake, na tukampulizia katika roho yetu, na
tukamfanya yeye na mwanawe kuwa ni Ishara kwa walimwengu.
|
Ayah 21:92 الأية
إِنَّ هَٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ
Inna hathihi ommatukum ommatan wahidatanwaana rabbukum faoAAbudoon
Swahili
Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo
niabuduni Mimi.
|
Ayah 21:93 الأية
وَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ ۖ كُلٌّ إِلَيْنَا رَاجِعُونَ
WataqattaAAoo amrahum baynahum kullunilayna rajiAAoon
Swahili
Nao wakalikata jambo lao hili mapande mapande baina yao. Wote watarudi kwetu.
|
Ayah 21:94 الأية
فَمَن يَعْمَلْ مِنَ الصَّالِحَاتِ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَا كُفْرَانَ لِسَعْيِهِ
وَإِنَّا لَهُ كَاتِبُونَ
Faman yaAAmal mina assalihatiwahuwa mu/minun fala kufrana lisaAAyihi wa-innalahu
katiboon
Swahili
Na atendaye mema naye ni Muumini basi haitakataliwa juhudi yake. Na hakika Sisi
tunamwandikia.
|
Ayah 21:95 الأية
وَحَرَامٌ عَلَىٰ قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا أَنَّهُمْ لَا يَرْجِعُونَ
Waharamun AAalaqaryatin ahlaknaha annahum la yarjiAAoon
Swahili
Na haiwi kwa wana-mji tulio uangamiza, ya kwamba hawatarejea,
|
Ayah 21:96 الأية
حَتَّىٰ إِذَا فُتِحَتْ يَأْجُوجُ وَمَأْجُوجُ وَهُم مِّن كُلِّ حَدَبٍ يَنسِلُونَ
Hatta itha futihatya/jooju wama/jooju wahum min kulli hadabin yansiloon
Swahili
Mpaka watapo funguliwa Juju na Maajuju wakawa wanateremka kutoka kila mlima;
|
Ayah 21:97 الأية
وَاقْتَرَبَ الْوَعْدُ الْحَقُّ فَإِذَا هِيَ شَاخِصَةٌ أَبْصَارُ الَّذِينَ
كَفَرُوا يَا وَيْلَنَا قَدْ كُنَّا فِي غَفْلَةٍ مِّنْ هَٰذَا بَلْ كُنَّا
ظَالِمِينَ
Waqtaraba alwaAAdu alhaqqufa-itha hiya shakhisatun absaru allatheenakafaroo ya
waylana qad kunna fee ghaflatinmin hatha bal kunna thalimeen
Swahili
Na miadi ya haki ikakaribia. Hapo ndipo yatapo kodoka macho ya walio kufuru (na
watasema:) Ole wetu! Bila ya shaka tulikuwa tumeghafilika na haya, bali tulikuwa
wenye kudhulumu.
|
Ayah 21:98 الأية
إِنَّكُمْ وَمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ حَصَبُ جَهَنَّمَ أَنتُمْ لَهَا
وَارِدُونَ
Innakum wama taAAbudoona min dooniAllahi hasabu jahannama antum laha waridoon
Swahili
Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu;
huko mtaingia tu.
|
Ayah 21:99 الأية
لَوْ كَانَ هَٰؤُلَاءِ آلِهَةً مَّا وَرَدُوهَا ۖ وَكُلٌّ فِيهَا خَالِدُونَ
Law kana haola-i alihatanma waradooha wakullun feeha khalidoon
Swahili
Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo.
|
Ayah 21:100 الأية
لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَهُمْ فِيهَا لَا يَسْمَعُونَ
Lahum feeha zafeerun wahum feehala yasmaAAoon
Swahili
Lao wao humo ni kupiga mayowe, na wala hawatasikia (jenginelo).
|
Ayah 21:101 الأية
إِنَّ الَّذِينَ سَبَقَتْ لَهُم مِّنَّا الْحُسْنَىٰ أُولَٰئِكَ عَنْهَا
مُبْعَدُونَ
Inna allatheena sabaqat lahum minnaalhusna ola-ika AAanha mubAAadoon
Swahili
Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao watatenganishwa na hayo.
|
Ayah 21:102 الأية
لَا يَسْمَعُونَ حَسِيسَهَا ۖ وَهُمْ فِي مَا اشْتَهَتْ أَنفُسُهُمْ خَالِدُونَ
La yasmaAAoona haseesahawahum fee ma ishtahat anfusuhum khalidoon
Swahili
Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale zinayo yatamani nafsi zao.
|
Ayah 21:103 الأية
لَا يَحْزُنُهُمُ الْفَزَعُ الْأَكْبَرُ وَتَتَلَقَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ هَٰذَا
يَوْمُكُمُ الَّذِي كُنتُمْ تُوعَدُونَ
La yahzunuhumu alfazaAAual-akbaru watatalaqqahumu almala-ikatu hathayawmukumu
allathee kuntum tooAAadoon
Swahili
Hicho Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. Na Malaika watawapokea (kwa
kuwaambia): Hii ndiyo Siku yenu mliyo kuwa mkiahidiwa!
|
Ayah 21:104 الأية
يَوْمَ نَطْوِي السَّمَاءَ كَطَيِّ السِّجِلِّ لِلْكُتُبِ ۚ كَمَا بَدَأْنَا
أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ ۚ وَعْدًا عَلَيْنَا ۚ إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ
Yawma natwee assamaakatayyi assijlli lilkutubi kama bada/naawwala khalqin
nuAAeeduhu waAAdan AAalayna innakunna faAAileen
Swahili
Siku tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo
anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni
watendao.
|
Ayah 21:105 الأية
وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الْأَرْضَ يَرِثُهَا
عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ
Walaqad katabna fee azzaboorimin baAAdi aththikri anna al-arda
yarithuhaAAibadiya assalihoon
Swahili
Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi
watairithi waja wangu walio wema.
|
Ayah 21:106 الأية
إِنَّ فِي هَٰذَا لَبَلَاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ
Inna fee hatha labalaghanliqawmin AAabideen
Swahili
Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao ibada.
|
Ayah 21:107 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ
Wama arsalnaka illa rahmatanlilAAalameen
Swahili
Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu wote.
|
Ayah 21:108 الأية
قُلْ إِنَّمَا يُوحَىٰ إِلَيَّ أَنَّمَا إِلَٰهُكُمْ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ فَهَلْ
أَنتُم مُّسْلِمُونَ
Qul innama yooha ilayya annamailahukum ilahun wahidun fahal antummuslimoon
Swahili
Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu.
Je! Mmesilimu?
|
Ayah 21:109 الأية
فَإِن تَوَلَّوْا فَقُلْ آذَنتُكُمْ عَلَىٰ سَوَاءٍ ۖ وَإِنْ أَدْرِي أَقَرِيبٌ أَم
بَعِيدٌ مَّا تُوعَدُونَ
Fa-in tawallaw faqul athantukum AAalasawa-in wa-in adree aqareebun am baAAeedun
matooAAadoon
Swahili
Na kama wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu
au mbali hayo mliyo ahidiwa.
|
Ayah 21:110 الأية
إِنَّهُ يَعْلَمُ الْجَهْرَ مِنَ الْقَوْلِ وَيَعْلَمُ مَا تَكْتُمُونَ
Innahu yaAAlamu aljahra mina alqawliwayaAAlamu ma taktumoon
Swahili
Hakika Yeye anajua kauli ya dhaahiri na anajua myafichayo.
|
Ayah 21:111 الأية
وَإِنْ أَدْرِي لَعَلَّهُ فِتْنَةٌ لَّكُمْ وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ
Wa-in adree laAAallahu fitnatun lakum wamataAAunila heen
Swahili
Wala sijui pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka muda kidogo.
|
Ayah 21:112 الأية
قَالَ رَبِّ احْكُم بِالْحَقِّ ۗ وَرَبُّنَا الرَّحْمَٰنُ الْمُسْتَعَانُ عَلَىٰ
مَا تَصِفُونَ
Qala rabbi ohkum bilhaqqiwarabbuna arrahmanu almustaAAanuAAala ma tasifoon
Swahili
Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa Rehema,
aombwaye msaada juu ya mnayo yazua.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|