1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
تَبَارَكَ الَّذِي نَزَّلَ الْفُرْقَانَ عَلَىٰ عَبْدِهِ لِيَكُونَ لِلْعَالَمِينَ
نَذِيرًا
Tabaraka allathee nazzalaalfurqana AAala AAabdihi liyakoona
lilAAalameenanatheera
Swahili
Ametukuka aliye teremsha Furqani kwa mja wake, ili awe mwonyaji kwa walimwengu
wote.
|
Ayah 25:2 الأية
الَّذِي لَهُ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَمْ يَتَّخِذْ وَلَدًا وَلَمْ
يَكُن لَّهُ شَرِيكٌ فِي الْمُلْكِ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ فَقَدَّرَهُ تَقْدِيرًا
Allathee lahu mulku assamawatiwal-ardi walam yattakhith waladan walamyakun lahu
shareekun fee almulki wakhalaqa kulla shay-infaqaddarahu taqdeera
Swahili
Ambaye ni wake ufalme wa mbingu na ardhi, wala hakuwa na mwana, wala hakuwa na
mshirika katika ufalme, na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo.
|
Ayah 25:3 الأية
وَاتَّخَذُوا مِن دُونِهِ آلِهَةً لَّا يَخْلُقُونَ شَيْئًا وَهُمْ يُخْلَقُونَ
وَلَا يَمْلِكُونَ لِأَنفُسِهِمْ ضَرًّا وَلَا نَفْعًا وَلَا يَمْلِكُونَ مَوْتًا
وَلَا حَيَاةً وَلَا نُشُورًا
Wattakhathoo min doonihi alihatanla yakhluqoona shay-an wahum yukhlaqoona
walayamlikoona li-anfusihim darran wala nafAAan walayamlikoona mawtan wala
hayatan walanushoora
Swahili
Na wamechukua badala yake miungu ambayo haiumbi chochote, bali hiyo inaumbwa,
haijimilikii nafsi zao madhara wala manufaa, wala haimiliki mauti, wala uhai,
wala kufufuka.
|
Ayah 25:4 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِنْ هَٰذَا إِلَّا إِفْكٌ افْتَرَاهُ وَأَعَانَهُ
عَلَيْهِ قَوْمٌ آخَرُونَ ۖ فَقَدْ جَاءُوا ظُلْمًا وَزُورًا
Waqala allatheena kafaroo in hathailla ifkun iftarahu waaAAanahu AAalayhiqawmun
akharoona faqad jaoo thulmanwazoora
Swahili
Na wamesema walio kufuru: Haya si chochote ila ni uzushi alio uzua, na
wamemsaidia kwa haya watu wengine! Hakika hawa wamekuja na dhulma na uwongo.
|
Ayah 25:5 الأية
وَقَالُوا أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ اكْتَتَبَهَا فَهِيَ تُمْلَىٰ عَلَيْهِ
بُكْرَةً وَأَصِيلًا
Waqaloo asateeru al-awwaleenaiktatabaha fahiya tumla AAalayhi bukratan waaseela
Swahili
Na wakasema: Hivi ni visa vya watu wa kale alivyo viandikisha, anavyo somewa
asubuhi na jioni.
|
Ayah 25:6 الأية
قُلْ أَنزَلَهُ الَّذِي يَعْلَمُ السِّرَّ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ إِنَّهُ
كَانَ غَفُورًا رَّحِيمًا
Qul anzalahu allathee yaAAlamu assirrafee assamawati wal-ardiinnahu kana
ghafooran raheema
Swahili
Sema: Ameyateremsha haya ajuaye siri za katika mbingu na ardhi. Hakika Yeye ni
Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
|
Ayah 25:7 الأية
وَقَالُوا مَالِ هَٰذَا الرَّسُولِ يَأْكُلُ الطَّعَامَ وَيَمْشِي فِي الْأَسْوَاقِ
ۙ لَوْلَا أُنزِلَ إِلَيْهِ مَلَكٌ فَيَكُونَ مَعَهُ نَذِيرًا
Waqaloo mali hatha arrasooliya/kulu attaAAama wayamshee fee al-aswaqilawla
onzila ilayhi malakun fayakoona maAAahu natheera
Swahili
Na wakasema: Ana nini Mtume huyu? Anakula chakula, na anatembea masokoni! Mbona
hakuteremshiwa Malaika akawa mwonyaji pamoja naye?
|
Ayah 25:8 الأية
أَوْ يُلْقَىٰ إِلَيْهِ كَنزٌ أَوْ تَكُونُ لَهُ جَنَّةٌ يَأْكُلُ مِنْهَا ۚ
وَقَالَ الظَّالِمُونَ إِن تَتَّبِعُونَ إِلَّا رَجُلًا مَّسْحُورًا
Aw yulqa ilayhi kanzun aw takoonu lahujannatun ya/kulu minha waqala
aththalimoonain tattabiAAoona illa rajulan mashoora
Swahili
Au akaangushiwa khazina juu yake, au akawa na bustani ale katika hiyo? Wakasema
madhaalimu: Nyinyi hamumfuati ila mtu aliye rogwa.
|
Ayah 25:9 الأية
انظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا لَكَ الْأَمْثَالَ فَضَلُّوا فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا
Onthur kayfa daraboolaka al-amthala fadalloo fala yastateeAAoonasabeela
Swahili
Tazama jinsi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea, wala hawataiweza Njia.
|
Ayah 25:10 الأية
تَبَارَكَ الَّذِي إِن شَاءَ جَعَلَ لَكَ خَيْرًا مِّن ذَٰلِكَ جَنَّاتٍ تَجْرِي
مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ وَيَجْعَل لَّكَ قُصُورًا
Tabaraka allathee in shaajaAAala laka khayran min thalika jannatin tajreemin
tahtiha al-anharu wayajAAal laka qusoora
Swahili
Ametukuka ambaye akitaka atakujaalia yaliyo bora kuliko hayo, nayo ni mabustani
yapitayo mito kati yao, na atakujaalia majumba ya fakhari.
|
Ayah 25:11 الأية
بَلْ كَذَّبُوا بِالسَّاعَةِ ۖ وَأَعْتَدْنَا لِمَن كَذَّبَ بِالسَّاعَةِ سَعِيرًا
Bal kaththaboo bissaAAatiwaaAAtadna liman kaththaba bissaAAatisaAAeera
Swahili
Bali wanaikanusha Saa (ya Kiyama). Na Sisi tumemuandalia Moto mkali kabisa huyo
mwenye kuikanusha Saa..
|
Ayah 25:12 الأية
إِذَا رَأَتْهُم مِّن مَّكَانٍ بَعِيدٍ سَمِعُوا لَهَا تَغَيُّظًا وَزَفِيرًا
Itha raat-hum min makaninbaAAeedin samiAAoo laha taghayyuthanwazafeera
Swahili
Ule Moto ukiwaona tangu mahali mbali wao watasikia hasira yake na mngurumo wake.
|
Ayah 25:13 الأية
وَإِذَا أُلْقُوا مِنْهَا مَكَانًا ضَيِّقًا مُّقَرَّنِينَ دَعَوْا هُنَالِكَ
ثُبُورًا
Wa-itha olqoo minha makanandayyiqan muqarraneena daAAaw hunalika thuboora
Swahili
Na watakapo tupwa humo mahali dhiki, hali wamefungwa, wataomba wafe.
|
Ayah 25:14 الأية
لَّا تَدْعُوا الْيَوْمَ ثُبُورًا وَاحِدًا وَادْعُوا ثُبُورًا كَثِيرًا
La tadAAoo alyawma thubooran wahidanwadAAoo thubooran katheera
Swahili
Msiombe kufa mara moja tu, bali mfe mara nyingi!
|
Ayah 25:15 الأية
قُلْ أَذَٰلِكَ خَيْرٌ أَمْ جَنَّةُ الْخُلْدِ الَّتِي وُعِدَ الْمُتَّقُونَ ۚ
كَانَتْ لَهُمْ جَزَاءً وَمَصِيرًا
Qul athalika khayrun am jannatualkhuldi allatee wuAAida almuttaqoona kanat lahum
jazaanwamaseera
Swahili
Sema: Je! Haya ni bora au Pepo ya milele, ambayo wameahidiwa wachamngu, iwe kwao
malipo na marejeo?
|
Ayah 25:16 الأية
لَّهُمْ فِيهَا مَا يَشَاءُونَ خَالِدِينَ ۚ كَانَ عَلَىٰ رَبِّكَ وَعْدًا
مَّسْئُولًا
Lahum feeha ma yashaoonakhalideena kana AAala rabbika waAAdanmas-oola
Swahili
Watayapata humo wayatakayo daima dawamu. Hii ni ahadi juu ya Mola wako Mlezi,
inayo ombwa.
|
Ayah 25:17 الأية
وَيَوْمَ يَحْشُرُهُمْ وَمَا يَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ فَيَقُولُ أَأَنتُمْ
أَضْلَلْتُمْ عِبَادِي هَٰؤُلَاءِ أَمْ هُمْ ضَلُّوا السَّبِيلَ
Wayawma yahshuruhum wamayaAAbudoona min dooni Allahi fayaqoolu aantum
adlaltumAAibadee haola-i am hum dalloo assabeel
Swahili
Na siku atakapo wakusanya wao na hao wanao waabudu, na akasema: Je! Ni nyinyi
mlio wapoteza waja wangu hawa, au wao wenyewe walipotea njia?
|
Ayah 25:18 الأية
قَالُوا سُبْحَانَكَ مَا كَانَ يَنبَغِي لَنَا أَن نَّتَّخِذَ مِن دُونِكَ مِنْ
أَوْلِيَاءَ وَلَٰكِن مَّتَّعْتَهُمْ وَآبَاءَهُمْ حَتَّىٰ نَسُوا الذِّكْرَ
وَكَانُوا قَوْمًا بُورًا
Qaloo subhanaka ma kanayanbaghee lana an nattakhitha min doonika min
awliyaawalakin mattaAAtahum waabaahum hattanasoo aththikra wakanoo qawman boora
Swahili
Watasema: Subhanak, Umetakasika na upungufu! Haikutupasia sisi kuchukulia
walinzi badala yako, lakini Wewe uliwastarehesha wao na baba zao hata wakasahau
kukumbuka, na wakawa watu walio angamia.
|
Ayah 25:19 الأية
فَقَدْ كَذَّبُوكُم بِمَا تَقُولُونَ فَمَا تَسْتَطِيعُونَ صَرْفًا وَلَا نَصْرًا ۚ
وَمَن يَظْلِم مِّنكُمْ نُذِقْهُ عَذَابًا كَبِيرًا
Faqad kaththabookum bimataqooloona fama tastateeAAoona sarfan walanasran waman
yathlim minkum nuthiqhuAAathaban kabeera
Swahili
Basi walikukanusheni kwa mliyo yasema. Kwa hivyo hamwezi kujiondolea wala
kujisaidia. Na atakaye dhulumu miongoni mwenu tutamwonjesha adhabu kubwa.
|
Ayah 25:20 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا قَبْلَكَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ إِلَّا إِنَّهُمْ لَيَأْكُلُونَ
الطَّعَامَ وَيَمْشُونَ فِي الْأَسْوَاقِ ۗ وَجَعَلْنَا بَعْضَكُمْ لِبَعْضٍ
فِتْنَةً أَتَصْبِرُونَ ۗ وَكَانَ رَبُّكَ بَصِيرًا
Wama arsalna qablaka minaalmursaleena illa innahum laya/kuloona
attaAAamawayamshoona fee al-aswaqi wajaAAalna baAAdakumlibaAAdin fitnatan
atasbiroona wakanarabbuka baseera
Swahili
Na hatukuwatuma kabla yako Mitume wowote ila kwa hakika na yakini walikuwa
wakila chakula, na wakenda masokoni. Na tumewajaalia baadhi yenu wawe ni
majaribio kwa wengine; je! Mtasubiri? Na Mola wako Mlezi ni Mwenye kuona.
|
Ayah 25:21 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ لَا يَرْجُونَ لِقَاءَنَا لَوْلَا أُنزِلَ عَلَيْنَا
الْمَلَائِكَةُ أَوْ نَرَىٰ رَبَّنَا ۗ لَقَدِ اسْتَكْبَرُوا فِي أَنفُسِهِمْ
وَعَتَوْا عُتُوًّا كَبِيرًا
Waqala allatheena layarjoona liqaana lawla onzila AAalaynaalmala-ikatu aw nara
rabbana laqadiistakbaroo fee anfusihim waAAataw AAutuwwan kabeera
Swahili
NA WALISEMA wale wasio taraji kukutana nasi: Mbona sisi hatuteremshiwi Malaika
au hatumwoni Mola wetu Mlezi? Kwa yakini hawa wamejiona bora nafsi zao, na
wamepanda kichwa vikubwa mno!
|
Ayah 25:22 الأية
يَوْمَ يَرَوْنَ الْمَلَائِكَةَ لَا بُشْرَىٰ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُجْرِمِينَ
وَيَقُولُونَ حِجْرًا مَّحْجُورًا
Yawma yarawna almala-ikata labushra yawma-ithin lilmujrimeena wayaqooloona
hijranmahjoora
Swahili
Siku watakayo waona Malaika haitakuwa furaha siku hiyo kwa wakosefu. Na
watasema: Mungu apishe mbali!
|
Ayah 25:23 الأية
وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا
Waqadimna ila maAAamiloo min AAamalin fajaAAalnahu habaan manthoora
Swahili
Na tutayaendea yale waliyo yatenda katika vitendo vyao, tuvifanye kama mavumbi
yaliyo tawanyika.
|
Ayah 25:24 الأية
أَصْحَابُ الْجَنَّةِ يَوْمَئِذٍ خَيْرٌ مُّسْتَقَرًّا وَأَحْسَنُ مَقِيلًا
As-habu aljannati yawma-ithinkhayrun mustaqarran waahsanu maqeela
Swahili
Watu wa Peponi siku hiyo watakuwa katika makaazi bora na mahali penye starehe
nzuri.
|
Ayah 25:25 الأية
وَيَوْمَ تَشَقَّقُ السَّمَاءُ بِالْغَمَامِ وَنُزِّلَ الْمَلَائِكَةُ تَنزِيلًا
Wayawma tashaqqaqu assamao bilghamamiwanuzzila almala-ikatu tanzeela
Swahili
Na siku zitapo funguka mbingu kwa mawingu, na wateremshwe Malaika kwa wingi,
|
Ayah 25:26 الأية
الْمُلْكُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ لِلرَّحْمَٰنِ ۚ وَكَانَ يَوْمًا عَلَى
الْكَافِرِينَ عَسِيرًا
Almulku yawma-ithin alhaqqu lirrahmaniwakana yawman AAala alkafireena AAaseera
Swahili
Ufalme wa haki siku hiyo utakuwa wa Arrahman, Mwingi wa Rehema, na itakuwa siku
ngumu kwa makafiri.
|
Ayah 25:27 الأية
وَيَوْمَ يَعَضُّ الظَّالِمُ عَلَىٰ يَدَيْهِ يَقُولُ يَا لَيْتَنِي اتَّخَذْتُ
مَعَ الرَّسُولِ سَبِيلًا
Wayawma yaAAaddu aththalimuAAala yadayhi yaqoolu ya laytanee ittakhathtumaAAa
arrasooli sabeela
Swahili
Na siku ambayo mwenye kudhulumu atajiuma mikono yake, na huku anasema: Laiti
ningeli shika njia pamoja na Mtume!
|
Ayah 25:28 الأية
يَا وَيْلَتَىٰ لَيْتَنِي لَمْ أَتَّخِذْ فُلَانًا خَلِيلًا
Ya waylata laytanee lamattakhith fulanan khaleela
Swahili
Ee Ole wangu! Laiti nisingeli mfanya fulani kuwa rafiki!
|
Ayah 25:29 الأية
لَّقَدْ أَضَلَّنِي عَنِ الذِّكْرِ بَعْدَ إِذْ جَاءَنِي ۗ وَكَانَ الشَّيْطَانُ
لِلْإِنسَانِ خَذُولًا
Laqad adallanee AAani aththikribaAAda ith jaanee wakana ashshaytanulil-insani
khathoola
Swahili
Amenipoteza, nikaacha Ukumbusho, baada ya kwisha nijia, na kweli Shet'ani ni
khaini kwa mwanaadamu.
|
Ayah 25:30 الأية
وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَٰذَا الْقُرْآنَ
مَهْجُورًا
Waqala arrasoolu yarabbi inna qawmee ittakhathoo hatha alqur-anamahjoora
Swahili
Na Mtume alikuwa akisema: Ee Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wameifanya hii
Qur'ani ni kihame.
|
Ayah 25:31 الأية
وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَا لِكُلِّ نَبِيٍّ عَدُوًّا مِّنَ الْمُجْرِمِينَ ۗ وَكَفَىٰ
بِرَبِّكَ هَادِيًا وَنَصِيرًا
Wakathalika jaAAalna likullinabiyyin AAaduwwan mina almujrimeena wakafa
birabbika hadiyanwanaseera
Swahili
Na vivi hivi tumemfanyia kila Nabii adui miongoni mwa wakosefu, na Mola wako
Mlezi anatosha kuwa Mwenye kuongoa na Mwenye kunusuru.
|
Ayah 25:32 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لَوْلَا نُزِّلَ عَلَيْهِ الْقُرْآنُ جُمْلَةً
وَاحِدَةً ۚ كَذَٰلِكَ لِنُثَبِّتَ بِهِ فُؤَادَكَ ۖ وَرَتَّلْنَاهُ تَرْتِيلًا
Waqala allatheena kafaroo lawlanuzzila AAalayhi alqur-anu jumlatan wahidatan
kathalikalinuthabbita bihi fu-adaka warattalnahu tarteela
Swahili
Na wakasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa Qur'ani kwa jumla moja? Hayo
ni hivyo ili tuuthibitishe moyo wako, na ndio tumeisoma kwa mafungu.
|
Ayah 25:33 الأية
وَلَا يَأْتُونَكَ بِمَثَلٍ إِلَّا جِئْنَاكَ بِالْحَقِّ وَأَحْسَنَ تَفْسِيرًا
Wala ya/toonaka bimathalin illaji/naka bilhaqqi waahsana tafseera
Swahili
Wala hawatakuletea mfano wowote, ila na Sisi tutakuletea (jawabu) kwa haki, na
tafsiri iliyo bora.
|
Ayah 25:34 الأية
الَّذِينَ يُحْشَرُونَ عَلَىٰ وُجُوهِهِمْ إِلَىٰ جَهَنَّمَ أُولَٰئِكَ شَرٌّ
مَّكَانًا وَأَضَلُّ سَبِيلًا
Allatheena yuhsharoona AAalawujoohihim ila jahannama ola-ika sharrun
makananwaadallu sabeela
Swahili
Wale ambao watakao kusanywa na kubururwa kifudifudi mpaka kwenye Jahannamu, hao
watakuwa na mahali pabaya, ndio wenye kuipotea sana njia.
|
Ayah 25:35 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ وَجَعَلْنَا مَعَهُ أَخَاهُ هَارُونَ وَزِيرًا
Walaqad atayna moosaalkitaba wajaAAalna maAAahu akhahu haroonawazeera
Swahili
Na hakika tulimpa Musa Kitabu na tukamweka pamoja naye nduguye, Harun, kuwa
waziri.
|
Ayah 25:36 الأية
فَقُلْنَا اذْهَبَا إِلَى الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا
فَدَمَّرْنَاهُمْ تَدْمِيرًا
Faqulna ithhaba ilaalqawmi allatheena kaththaboo bi-ayatinafadammarnahum
tadmeera
Swahili
Tukawaambia: Nendeni kwa watu walio kanusha Ishara zetu. Basi tukawateketeza
kabisa.
|
Ayah 25:37 الأية
وَقَوْمَ نُوحٍ لَّمَّا كَذَّبُوا الرُّسُلَ أَغْرَقْنَاهُمْ وَجَعَلْنَاهُمْ
لِلنَّاسِ آيَةً ۖ وَأَعْتَدْنَا لِلظَّالِمِينَ عَذَابًا أَلِيمًا
Waqawma noohin lamma kaththabooarrusula aghraqnahum wajaAAalnahum linnasiayatan
waaAAtadna liththalimeenaAAathaban aleema
Swahili
Na watu wa Nuhu, walipo wakanusha Mitume, tuliwazamisha, na tukawafanya ni
Ishara kwa watu. Na tumewaandalia wenye kudhulumu adhabu chungu.
|
Ayah 25:38 الأية
وَعَادًا وَثَمُودَ وَأَصْحَابَ الرَّسِّ وَقُرُونًا بَيْنَ ذَٰلِكَ كَثِيرًا
WaAAadan wathamooda waas-habaarrassi waquroonan bayna thalika katheera
Swahili
Na tuliwaangamiza kina A'di na Thamudi na watu wa Rass na vizazi vingi vilivyo
kuwa kati yao.
|
Ayah 25:39 الأية
وَكُلًّا ضَرَبْنَا لَهُ الْأَمْثَالَ ۖ وَكُلًّا تَبَّرْنَا تَتْبِيرًا
Wakullan darabna lahu al-amthalawakullan tabbarna tatbeera
Swahili
Na wote tuliwapigia mifano, na wote tuliwaangamiza kabisa kabisa.
|
Ayah 25:40 الأية
وَلَقَدْ أَتَوْا عَلَى الْقَرْيَةِ الَّتِي أُمْطِرَتْ مَطَرَ السَّوْءِ ۚ
أَفَلَمْ يَكُونُوا يَرَوْنَهَا ۚ بَلْ كَانُوا لَا يَرْجُونَ نُشُورًا
Walaqad ataw AAala alqaryati allateeomtirat matara assaw-i afalam
yakoonooyarawnaha bal kanoo la yarjoona nushoora
Swahili
Na kwa yakini wao wanafika kwenye nchi ilio teremshiwa mvua mbaya. Basi, je,
hawakuwa wakiiona? Bali walikuwa hawataraji kufufuliwa.
|
Ayah 25:41 الأية
وَإِذَا رَأَوْكَ إِن يَتَّخِذُونَكَ إِلَّا هُزُوًا أَهَٰذَا الَّذِي بَعَثَ
اللهُ رَسُولًا
Wa-itha raawka in yattakhithoonakailla huzuwan ahatha allathee baAAatha
Allahurasoola
Swahili
Na wanapo kuona hawakuchukulii ila ni mzaha tu, na (wanasema): Ati ndiye huyu
Mwenyezi Mungu aliye mtuma kuwa Mtume?
|
Ayah 25:42 الأية
إِن كَادَ لَيُضِلُّنَا عَنْ آلِهَتِنَا لَوْلَا أَن صَبَرْنَا عَلَيْهَا ۚ
وَسَوْفَ يَعْلَمُونَ حِينَ يَرَوْنَ الْعَذَابَ مَنْ أَضَلُّ سَبِيلًا
In kada layudillunaAAan alihatina lawla an sabarnaAAalayha wasawfa yaAAlamoona
heena yarawna alAAathabaman adallu sabeela
Swahili
Kwa hakika alikuwa karibu kutupoteza tuiache miungu yetu, ingeli kuwa
hatukushikamana nayo kwa kuvumilia. Bado watakuja jua, watakapo iona adhabu, ni
nani aliye potea njia.
|
Ayah 25:43 الأية
أَرَأَيْتَ مَنِ اتَّخَذَ إِلَٰهَهُ هَوَاهُ أَفَأَنتَ تَكُونُ عَلَيْهِ وَكِيلًا
Araayta mani ittakhatha ilahahuhawahu afaanta takoonu AAalayhi wakeela
Swahili
Je! Umemwona aliye yafanya matamanio yake kuwa ndio mungu wake? Basi je, wewe
utakuwa ni wakili wake?
|
Ayah 25:44 الأية
أَمْ تَحْسَبُ أَنَّ أَكْثَرَهُمْ يَسْمَعُونَ أَوْ يَعْقِلُونَ ۚ إِنْ هُمْ إِلَّا
كَالْأَنْعَامِ ۖ بَلْ هُمْ أَضَلُّ سَبِيلًا
Am tahsabu anna aktharahumyasmaAAoona aw yaAAqiloona in hum illa kal-anAAamibal
hum adallu sabeela
Swahili
Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni
kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia.
|
Ayah 25:45 الأية
أَلَمْ تَرَ إِلَىٰ رَبِّكَ كَيْفَ مَدَّ الظِّلَّ وَلَوْ شَاءَ لَجَعَلَهُ
سَاكِنًا ثُمَّ جَعَلْنَا الشَّمْسَ عَلَيْهِ دَلِيلًا
Alam tara ila rabbika kayfa madda aththillawalaw shaa lajaAAalahu sakinan thumma
jaAAalnaashshamsa AAalayhi daleela
Swahili
Je! Huoni jinsi Mola wako Mlezi anavyo kitandaza kivuli. Na angeli taka angeli
kifanya kikatulia tu. Kisha tumelifanya jua kuwa ni kiongozi wake.
|
Ayah 25:46 الأية
ثُمَّ قَبَضْنَاهُ إِلَيْنَا قَبْضًا يَسِيرًا
Thumma qabadnahu ilaynaqabdan yaseera
Swahili
Kisha tunakivutia kwetu kidogo kidogo.
|
Ayah 25:47 الأية
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ لِبَاسًا وَالنَّوْمَ سُبَاتًا وَجَعَلَ
النَّهَارَ نُشُورًا
Wahuwa allathee jaAAala lakumuallayla libasan wannawma subatan wajaAAalaannahara
nushoora
Swahili
Naye ndiye aliye kufanyieni usiku kuwa ni vazi, na usingizi kuwa mapumziko, na
akakufanyieni mchana ni kufufuka.
|
Ayah 25:48 الأية
وَهُوَ الَّذِي أَرْسَلَ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۚ
وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً طَهُورًا
Wahuwa allathee arsala arriyahabushran bayna yaday rahmatihi waanzalna mina
assama-imaan tahoora
Swahili
Naye ndiye anaye zituma pepo kuwa bishara njema kabla ya rehema yake, na
tunayateremsha kutoka mbinguni maji safi.
|
Ayah 25:49 الأية
لِّنُحْيِيَ بِهِ بَلْدَةً مَّيْتًا وَنُسْقِيَهُ مِمَّا خَلَقْنَا أَنْعَامًا
وَأَنَاسِيَّ كَثِيرًا
Linuhyiya bihi baldatan maytanwanusqiyahu mimma khalaqna anAAaman
waanasiyyakatheera
Swahili
Ili kwa hayo tuihuishe nchi iliyo kufa, na tuwanyweshe wanyama na watu wengi
tulio waumba.
|
Ayah 25:50 الأية
وَلَقَدْ صَرَّفْنَاهُ بَيْنَهُمْ لِيَذَّكَّرُوا فَأَبَىٰ أَكْثَرُ النَّاسِ
إِلَّا كُفُورًا
Walaqad sarrafnahu baynahumliyaththakkaroo faaba aktharu annasiilla kufoora
Swahili
Na kwa yakini tumeisarifu kati yao wapate kukumbuka. Lakini watu wengi wanakataa
ila kukufuru.
|
Ayah 25:51 الأية
وَلَوْ شِئْنَا لَبَعَثْنَا فِي كُلِّ قَرْيَةٍ نَّذِيرًا
Walaw shi/na labaAAathna feekulli qaryatin natheera
Swahili
Na tungeli taka tungeli peleka katika kila mji Mwonyaji.
|
Ayah 25:52 الأية
فَلَا تُطِعِ الْكَافِرِينَ وَجَاهِدْهُم بِهِ جِهَادًا كَبِيرًا
Fala tutiAAi alkafireenawajahidhum bihi jihadan kabeera
Swahili
Basi usiwat'ii makafiri. Na pambana nao kwayo kwa Jihadi kubwa.
|
Ayah 25:53 الأية
وَهُوَ الَّذِي مَرَجَ الْبَحْرَيْنِ هَٰذَا عَذْبٌ فُرَاتٌ وَهَٰذَا مِلْحٌ
أُجَاجٌ وَجَعَلَ بَيْنَهُمَا بَرْزَخًا وَحِجْرًا مَّحْجُورًا
Wahuwa allathee maraja albahraynihatha AAathbun furatun wahatha milhunojajun
wajaAAala baynahuma barzakhan wahijranmahjoora
Swahili
Naye ndiye aliye zipeleka bahari mbili, hii tamu mno, na hii ya chumvi chungu.
Na akaweka baina yao kinga na kizuizi kizuiacho.
|
Ayah 25:54 الأية
وَهُوَ الَّذِي خَلَقَ مِنَ الْمَاءِ بَشَرًا فَجَعَلَهُ نَسَبًا وَصِهْرًا ۗ
وَكَانَ رَبُّكَ قَدِيرًا
Wahuwa allathee khalaqa mina alma-ibasharan fajaAAalahu nasaban wasihran
wakanarabbuka qadeera
Swahili
Naye ndiye aliye muumba mwanaadamu kutokana na maji, akamjaalia kuwa na nasaba
na ushemeji. Na Mola wako Mlezi ni Muweza.
|
Ayah 25:55 الأية
وَيَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللهِ مَا لَا يَنفَعُهُمْ وَلَا يَضُرُّهُمْ ۗ وَكَانَ
الْكَافِرُ عَلَىٰ رَبِّهِ ظَهِيرًا
WayaAAbudoona min dooni Allahi mala yanfaAAuhum wala yadurruhum wakanaalkafiru
AAala rabbihi thaheera
Swahili
Na wanayaabudu badala ya Mwenyezi Mungu yasiyo wafaa wala yasiyo wadhuru. Na
kafiri daima ni msaidizi wa kumpinga Mola wake Mlezi.
|
Ayah 25:56 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا مُبَشِّرًا وَنَذِيرًا
Wama arsalnaka illamubashshiran wanatheera
Swahili
Nasi hatukukutuma ila kuwa ni Mbashiri na Mwonyaji.
|
Ayah 25:57 الأية
قُلْ مَا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ مِنْ أَجْرٍ إِلَّا مَن شَاءَ أَن يَتَّخِذَ إِلَىٰ
رَبِّهِ سَبِيلًا
Qul ma as-alukum AAalayhi min ajrinilla man shaa an yattakhitha ilarabbihi
sabeela
Swahili
Sema: Sikukuombeni ujira juu yake; ila atakaye na ashike njia iendayo kwa Mola
wake Mlezi.
|
Ayah 25:58 الأية
وَتَوَكَّلْ عَلَى الْحَيِّ الَّذِي لَا يَمُوتُ وَسَبِّحْ بِحَمْدِهِ ۚ وَكَفَىٰ
بِهِ بِذُنُوبِ عِبَادِهِ خَبِيرًا
Watawakkal AAala alhayyi allatheela yamootu wasabbih bihamdihi wakafabihi
bithunoobi AAibadihi khabeera
Swahili
Na mtegemee Aliye Hai, ambaye hafi. Na umtukuze kwa sifa zake. Na yatosha kwake
kuwa yeye ni Mwenye khabari za dhambi za waja wake.
|
Ayah 25:59 الأية
الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ
ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا
Allathee khalaqa assamawatiwal-arda wama baynahuma fee sittatiayyamin thumma
istawa AAala alAAarshi arrahmanufas-al bihi khabeera
Swahili
Ambaye ameziumba mbingu na ardhi, na viliomo ndani yake kwa siku sita. Kisha
akatawala juu ya A'rshi, Arrahman, Mwingi wa Rehema! Uliza khabari zake kwa
wamjuaye.
|
Ayah 25:60 الأية
وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَٰنُ
أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩
Wa-itha qeela lahumu osjudoo lirrahmaniqaloo wama arrahmanu anasjudulima
ta/muruna wazadahum nufoora
Swahili
Na wanapo ambiwa: Msujudieni Arrahman! Wao husema: Ni nani Arrahman? Je!
Tumsujudie unaye tuamrisha wewe tu? Na huwazidishia chuki.
|
Ayah 25:61 الأية
تَبَارَكَ الَّذِي جَعَلَ فِي السَّمَاءِ بُرُوجًا وَجَعَلَ فِيهَا سِرَاجًا
وَقَمَرًا مُّنِيرًا
Tabaraka allathee jaAAala feeassama-i buroojan wajaAAala feeha sirajanwaqamaran
muneera
Swahili
Ametukuka aliye zijaalia nyota mbinguni, na akajaalia humo taa na mwezi unao
ng'ara.
|
Ayah 25:62 الأية
وَهُوَ الَّذِي جَعَلَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ خِلْفَةً لِّمَنْ أَرَادَ أَن
يَذَّكَّرَ أَوْ أَرَادَ شُكُورًا
Wahuwa allathee jaAAala allayla wannaharakhilfatan liman arada an yaththakkara
aw aradashukoora
Swahili
Naye ndiye aliye fanya usiku na mchana kufuatana kwa nafuu ya anaye taka
kukumbuka, au anaye taka kushukuru.
|
Ayah 25:63 الأية
وَعِبَادُ الرَّحْمَٰنِ الَّذِينَ يَمْشُونَ عَلَى الْأَرْضِ هَوْنًا وَإِذَا
خَاطَبَهُمُ الْجَاهِلُونَ قَالُوا سَلَامًا
WaAAibadu arrahmaniallatheena yamshoona AAala al-ardi hawnanwa-itha khatabahumu
aljahiloona qaloosalama
Swahili
Na waja wa Arrahman Mwingi wa Rehema ni wale wanao tembea ulimwenguni kwa staha,
na wajinga wakiwasemeza hujibu: Salama!
|
Ayah 25:64 الأية
وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا
Wallatheena yabeetoonalirabbihim sujjadan waqiyama
Swahili
Na wale wanao kesha kwa ajili ya Mola wao Mlezi kwa kusujudu na kusimama.
|
Ayah 25:65 الأية
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا اصْرِفْ عَنَّا عَذَابَ جَهَنَّمَ ۖ إِنَّ
عَذَابَهَا كَانَ غَرَامًا
Wallatheena yaqooloona rabbanaisrif AAanna AAathaba jahannama inna
AAathabahakana gharama
Swahili
Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tuondolee adhabu ya Jahannamu. Hakika
adhabu yake ikimpata mtu haimwachi.
|
Ayah 25:66 الأية
إِنَّهَا سَاءَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا
Innaha saat mustaqarran wamuqama
Swahili
Hakika hiyo ni kituo na makao mabaya.
|
Ayah 25:67 الأية
وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ
ذَٰلِكَ قَوَامًا
Wallatheena ithaanfaqoo lam yusrifoo walam yaqturoo wakana bayna thalikaqawama
Swahili
Na wale ambao wanapo tumia hawatumii kwa fujo wala hawafanyi ubakhili, bali
wanakuwa katikati baina ya hayo.
|
Ayah 25:68 الأية
وَالَّذِينَ لَا يَدْعُونَ مَعَ اللهِ إِلَٰهًا آخَرَ وَلَا يَقْتُلُونَ
النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلَّا بِالْحَقِّ وَلَا يَزْنُونَ ۚ وَمَن
يَفْعَلْ ذَٰلِكَ يَلْقَ أَثَامًا
Wallatheena layadAAoona maAAa Allahi ilahan akharawala yaqtuloona annafsa
allatee harrama Allahuilla bilhaqqi wala yaznoona wamanyafAAal thalika yalqa
athama
Swahili
Na wale wasio mwomba mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu, wala hawaui nafsi
aliyo iharimisha Mwenyezi Mungu isipo kuwa kwa haki, wala hawazini - na atakaye
fanya hayo atapata madhara,
|
Ayah 25:69 الأية
يُضَاعَفْ لَهُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَيَخْلُدْ فِيهِ مُهَانًا
YudaAAaf lahu alAAathabu yawmaalqiyamati wayakhlud feehi muhana
Swahili
Atazidishiwa adhabu Siku ya Kiyama, na atadumu humo kwa kufedheheka.
|
Ayah 25:70 الأية
إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ عَمَلًا صَالِحًا فَأُولَٰئِكَ يُبَدِّلُ
اللهُ سَيِّئَاتِهِمْ حَسَنَاتٍ ۗ وَكَانَ اللهُ غَفُورًا رَّحِيمًا
Illa man taba waamanawaAAamila AAamalan salihan faola-ikayubaddilu Allahu
sayyi-atihim hasanatinwakana Allahu ghafooran raheema
Swahili
Isipo kuwa atakaye tubu, na akaamini, na akatenda vitendo vyema. Basi hao
Mwenyezi Mungu atayabadilisha maovu yao yawe mema. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye
kusamehe, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 25:71 الأية
وَمَن تَابَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَإِنَّهُ يَتُوبُ إِلَى اللهِ مَتَابًا
Waman taba waAAamila salihanfa-innahu yatoobu ila Allahi mataba
Swahili
Na aliye tubu na akafanya mema, basi hakika huyo ametubu kweli kweli kwa
Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 25:72 الأية
وَالَّذِينَ لَا يَشْهَدُونَ الزُّورَ وَإِذَا مَرُّوا بِاللَّغْوِ مَرُّوا
كِرَامًا
Wallatheena layashhadoona azzoora wa-itha marroo billaghwimarroo kirama
Swahili
Na wale ambao hawatoi ushahidi wa uwongo, na pindi wapitapo penye upuuzi, hupita
kwa hishima yao.
|
Ayah 25:73 الأية
وَالَّذِينَ إِذَا ذُكِّرُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ لَمْ يَخِرُّوا عَلَيْهَا صُمًّا
وَعُمْيَانًا
Wallatheena itha thukkiroobi-ayati rabbihim lam yakhirroo AAalayha
summanwaAAumyana
Swahili
Na wale ambao wanapo kumbushwa Ishara za Mola wao Mlezi hawajifanyi viziwi nazo,
na vipofu.
|
Ayah 25:74 الأية
وَالَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا هَبْ لَنَا مِنْ أَزْوَاجِنَا وَذُرِّيَّاتِنَا
قُرَّةَ أَعْيُنٍ وَاجْعَلْنَا لِلْمُتَّقِينَ إِمَامًا
Wallatheena yaqooloona rabbanahab lana min azwajina wathurriyyatinaqurrata
aAAyunin wajAAalna lilmuttaqeena imama
Swahili
Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu
yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu.
|
Ayah 25:75 الأية
أُولَٰئِكَ يُجْزَوْنَ الْغُرْفَةَ بِمَا صَبَرُوا وَيُلَقَّوْنَ فِيهَا تَحِيَّةً
وَسَلَامًا
Ola-ika yujzawna alghurfata bimasabaroo wayulaqqawna feeha tahiyyatan wasalama
Swahili
Hao ndio watakao lipwa makao ya juu kwa kuwa walisubiri, na watakuta humo
maamkio na salamu.
|
Ayah 25:76 الأية
خَالِدِينَ فِيهَا ۚ حَسُنَتْ مُسْتَقَرًّا وَمُقَامًا
Khalideena feeha hasunatmustaqarran wamuqama
Swahili
Wadumu humo - kituo na makao mazuri kabisa.
|
Ayah 25:77 الأية
قُلْ مَا يَعْبَأُ بِكُمْ رَبِّي لَوْلَا دُعَاؤُكُمْ ۖ فَقَدْ كَذَّبْتُمْ
فَسَوْفَ يَكُونُ لِزَامًا
Qul ma yaAAbao bikum rabbee lawladuAAaokum faqad kaththabtum fasawfa yakoonu
lizama
Swahili
Sema: Mola wangu Mlezi asinge kujalini lau kuwa si kuomba kwenu. Lakini nyinyi
mmemkadhibisha. Basi adhabu lazima iwe.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|