| بِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ | |
|
طسم
Ta-seen-meem
Swahili
T'A SIN MIM, (T'.S.M.)
|
Ayah 28:2 الأية
تِلْكَ آيَاتُ الْكِتَابِ الْمُبِينِ
Tilka ayatu alkitabialmubeen
Swahili
Hizi ni Aya za Kitabu kinacho bainisha.
|
Ayah 28:3 الأية
نَتْلُو عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِالْحَقِّ لِقَوْمٍ
يُؤْمِنُونَ
Natloo AAalayka min naba-i moosawafirAAawna bilhaqqi liqawmin yu/minoon
Swahili
Tunakusomea khabari za Musa na Firauni kwa Haki kwa ajili ya watu wanao amini.
|
Ayah 28:4 الأية
إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِي الْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ
طَائِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَاءَهُمْ وَيَسْتَحْيِي نِسَاءَهُمْ ۚ إِنَّهُ
كَانَ مِنَ الْمُفْسِدِينَ
Inna firAAawna AAala fee al-ardiwajaAAala ahlaha shiyaAAan yastadAAifu
ta-ifatanminhum yuthabbihu abnaahum wayastahyeenisaahum innahu kana mina
almufsideen
Swahili
Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali
mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume
na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi.
|
Ayah 28:5 الأية
وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ
وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ
Wanureedu an namunna AAala allatheenaistudAAifoo fee al-ardi wanajAAalahum
a-immatanwanajAAalahumu alwaritheen
Swahili
Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe
waongozi na kuwafanya ni warithi.
|
Ayah 28:6 الأية
وَنُمَكِّنَ لَهُمْ فِي الْأَرْضِ وَنُرِيَ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا
مِنْهُم مَّا كَانُوا يَحْذَرُونَ
Wanumakkina lahum fee al-ardi wanuriyafirAAawna wahamana wajunoodahuma minhum
makanoo yahtharoon
Swahili
Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na
Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa.
|
Ayah 28:7 الأية
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ
فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ
إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ
Waawhayna ila ommi moosaan ardiAAeehi fa-itha khifti AAalayhi faalqeehi
feealyammi wala takhafee wala tahzaneeinna raddoohu ilayki wajaAAiloohu
minaalmursaleen
Swahili
Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mkhofia basi
mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na
tutamfanya miongoni mwa Mitume.
|
Ayah 28:8 الأية
فَالْتَقَطَهُ آلُ فِرْعَوْنَ لِيَكُونَ لَهُمْ عَدُوًّا وَحَزَنًا ۗ إِنَّ
فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ
Faltaqatahu alufirAAawna liyakoona lahum AAaduwwan wahazanan innafirAAawna
wahamana wajunoodahuma kanookhati-een
Swahili
Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni
na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.
|
Ayah 28:9 الأية
وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ
عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ
Waqalati imraatu firAAawna qurratuAAaynin lee walaka la taqtuloohu AAasa an
yanfaAAanaaw nattakhithahu waladan wahum la yashAAuroon
Swahili
Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako.
Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua.
|
Ayah 28:10 الأية
وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا
أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Waasbaha fu-adu ommimoosa farighan in kadat latubdee bihi lawlaan rabatna AAala
qalbiha litakoonamina almu/mineen
Swahili
Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingeli kuwa
hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.
|
Ayah 28:11 الأية
وَقَالَتْ لِأُخْتِهِ قُصِّيهِ ۖ فَبَصُرَتْ بِهِ عَن جُنُبٍ وَهُمْ لَا
يَشْعُرُونَ
Waqalat li-okhtihi qusseehifabasurat bihi AAan junubin wahum la yashAAuroon
Swahili
Naye akamwambia dada yake Musa: Mfuatie. Basi naye akawa anamuangalia kwa mbali
bila ya wao kujua.
|
Ayah 28:12 الأية
وَحَرَّمْنَا عَلَيْهِ الْمَرَاضِعَ مِن قَبْلُ فَقَالَتْ هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ
أَهْلِ بَيْتٍ يَكْفُلُونَهُ لَكُمْ وَهُمْ لَهُ نَاصِحُونَ
Waharramna AAalayhi almaradiAAamin qablu faqalat hal adullukum AAala ahli
baytinyakfuloonahu lakum wahum lahu nasihoon
Swahili
Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo, mpaka dada yake
akasema: Je! Nikuonyesheni watu wa nyumba watakao mlea kwa ajili yenu, nao pia
watakuwa wema kwake?
|
Ayah 28:13 الأية
فَرَدَدْنَاهُ إِلَىٰ أُمِّهِ كَيْ تَقَرَّ عَيْنُهَا وَلَا تَحْزَنَ وَلِتَعْلَمَ
أَنَّ وَعْدَ اللهِ حَقٌّ وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Faradadnahu ila ommihi kaytaqarra AAaynuha wala tahzana walitaAAlamaanna waAAda
Allahi haqqun walakinnaaktharahum la yaAAlamoon
Swahili
Basi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na
ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui.
|
Ayah 28:14 الأية
وَلَمَّا بَلَغَ أَشُدَّهُ وَاسْتَوَىٰ آتَيْنَاهُ حُكْمًا وَعِلْمًا ۚ وَكَذَٰلِكَ
نَجْزِي الْمُحْسِنِينَ
Walamma balagha ashuddahu wastawaataynahu hukman waAAilman wakathalikanajzee
almuhsineen
Swahili
Na Musa alipo fika utu-uzima baraabara, tulimpa akili na ilimu. Na hivi ndivyo
tunavyo walipa walio wema.
|
Ayah 28:15 الأية
وَدَخَلَ الْمَدِينَةَ عَلَىٰ حِينِ غَفْلَةٍ مِّنْ أَهْلِهَا فَوَجَدَ فِيهَا
رَجُلَيْنِ يَقْتَتِلَانِ هَٰذَا مِن شِيعَتِهِ وَهَٰذَا مِنْ عَدُوِّهِ ۖ
فَاسْتَغَاثَهُ الَّذِي مِن شِيعَتِهِ عَلَى الَّذِي مِنْ عَدُوِّهِ فَوَكَزَهُ
مُوسَىٰ فَقَضَىٰ عَلَيْهِ ۖ قَالَ هَٰذَا مِنْ عَمَلِ الشَّيْطَانِ ۖ إِنَّهُ
عَدُوٌّ مُّضِلٌّ مُّبِينٌ
Wadakhala almadeenata AAala heenighaflatin min ahliha fawajada feeha
rajulayniyaqtatilani hatha min sheeAAatihi wahathamin AAaduwwihi fastaghathahu
allathee minsheeAAatihi AAala allathee min AAaduwwihifawakazahu moosa faqada
AAalayhi qala hathamin AAamali ashshaytani innahu AAaduwwun mudillunmubeen
Swahili
Na akaingia mjini wakati wa kughafilika wenyeji wake, na akakuta humo watu
wawili wanapigana - mmoja ni katika wenzake, na mwengine katika maadui zake.
Yule mwenzake alimtaka msaada kumpiga adui yake. Musa akampiga ngumi, akamuuwa.
Akasema: Hiki ni kitendo cha Shet'ani; hakika yeye ni adui, mpotezaji dhaahiri.
|
Ayah 28:16 الأية
قَالَ رَبِّ إِنِّي ظَلَمْتُ نَفْسِي فَاغْفِرْ لِي فَغَفَرَ لَهُ ۚ إِنَّهُ هُوَ
الْغَفُورُ الرَّحِيمُ
Qala rabbi innee thalamtunafsee faghfir lee faghafara lahu innahu huwa
alghafooruarraheem
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe.
Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu.
|
Ayah 28:17 الأية
قَالَ رَبِّ بِمَا أَنْعَمْتَ عَلَيَّ فَلَنْ أَكُونَ ظَهِيرًا لِّلْمُجْرِمِينَ
Qala rabbi bima anAAamtaAAalayya falan akoona thaheeran lilmujrimeen
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Kwa ulivyo nineemesha, basi mimi sitakuwa kabisa
msaidizi wa wakosefu.
|
Ayah 28:18 الأية
فَأَصْبَحَ فِي الْمَدِينَةِ خَائِفًا يَتَرَقَّبُ فَإِذَا الَّذِي اسْتَنصَرَهُ
بِالْأَمْسِ يَسْتَصْرِخُهُ ۚ قَالَ لَهُ مُوسَىٰ إِنَّكَ لَغَوِيٌّ مُّبِينٌ
Faasbaha fee almadeenati kha-ifanyataraqqabu fa-itha allathee istansarahu
bil-amsiyastasrikhuhu qala lahu moosa innakalaghawiyyun mubeen
Swahili
Akapambazukiwa mjini asubuhi naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Mara yule
yule aliye mtaka msaada jana akawa anampigia kelele amsaidie. Musa akamwambia:
Hakika wewe ni mgomvi kweli kweli.
|
Ayah 28:19 الأية
فَلَمَّا أَنْ أَرَادَ أَن يَبْطِشَ بِالَّذِي هُوَ عَدُوٌّ لَّهُمَا قَالَ يَا
مُوسَىٰ أَتُرِيدُ أَن تَقْتُلَنِي كَمَا قَتَلْتَ نَفْسًا بِالْأَمْسِ ۖ إِن
تُرِيدُ إِلَّا أَن تَكُونَ جَبَّارًا فِي الْأَرْضِ وَمَا تُرِيدُ أَن تَكُونَ
مِنَ الْمُصْلِحِينَ
Falamma an arada an yabtishabillathee huwa AAaduwwun lahuma qalaya moosa
atureedu an taqtulanee kama qataltanafsan bil-amsi in tureedu illa an takoona
jabbaranfee al-ardi wama tureedu an takoona mina almusliheen
Swahili
Basi alipo taka kumshika kwa nguvu yule aliye adui wao wote wawili, akasema: Ewe
Musa! Unataka kuniuwa kama ulivyo muuwa mtu jana? Wewe hutaki ila kuwa jabari
katika nchi, wala hutaki kuwa miongoni mwa wenye maslaha..
|
Ayah 28:20 الأية
وَجَاءَ رَجُلٌ مِّنْ أَقْصَى الْمَدِينَةِ يَسْعَىٰ قَالَ يَا مُوسَىٰ إِنَّ
الْمَلَأَ يَأْتَمِرُونَ بِكَ لِيَقْتُلُوكَ فَاخْرُجْ إِنِّي لَكَ مِنَ
النَّاصِحِينَ
Wajaa rajulun min aqsaalmadeenati yasAAa qala ya moosa innaalmalaa ya/tamiroona
bika liyaqtulooka fakhruj innee lakamina annasiheen
Swahili
Na akaja mtu kutoka mwisho wa mji akipiga mbio, akasema: Ewe Musa! Wakubwa
wanashauriana kukuuwa. Basi toka! Hakika mimi ni katika wanao kupa nasaha.
|
Ayah 28:21 الأية
فَخَرَجَ مِنْهَا خَائِفًا يَتَرَقَّبُ ۖ قَالَ رَبِّ نَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ
الظَّالِمِينَ
Fakharaja minha kha-ifanyataraqqabu qala rabbi najjinee mina alqawmi
aththalimeen
Swahili
Basi akatoka, naye ana khofu, akiangalia huku na huku. Akasema: Mola wangu
Mlezi! Niokoe na watu madhaalimu.
|
Ayah 28:22 الأية
وَلَمَّا تَوَجَّهَ تِلْقَاءَ مَدْيَنَ قَالَ عَسَىٰ رَبِّي أَن يَهْدِيَنِي
سَوَاءَ السَّبِيلِ
Walamma tawajjaha tilqaamadyana qala AAasa rabbee an yahdiyanee sawaaassabeel
Swahili
Na alipo elekea upande wa Madyana alisema: Asaa Mola wangu Mlezi akaniongoa njia
iliyo sawa.
|
Ayah 28:23 الأية
وَلَمَّا وَرَدَ مَاءَ مَدْيَنَ وَجَدَ عَلَيْهِ أُمَّةً مِّنَ النَّاسِ يَسْقُونَ
وَوَجَدَ مِن دُونِهِمُ امْرَأَتَيْنِ تَذُودَانِ ۖ قَالَ مَا خَطْبُكُمَا ۖ
قَالَتَا لَا نَسْقِي حَتَّىٰ يُصْدِرَ الرِّعَاءُ ۖ وَأَبُونَا شَيْخٌ كَبِيرٌ
Walamma warada maa madyanawajada AAalayhi ommatan mina annasi yasqoonawawajada
min doonihimu imraatayni tathoodani qalama khatbukuma qalata lanasqee hatta
yusdira arriAAaowaaboona shaykhun kabeer
Swahili
Na alipo yafikia maji ya Madyana alikuta umati wa watu wananywesha (wanyama
wao), na akakuta karibu yao wanawake wawili wanawazuia wanyama wao. Akasema: Mna
nini? Wakasema: Hatunyweshi sisi mpaka wamalize hao wachunga. Na baba yetu ni
mzee sana.
|
Ayah 28:24 الأية
فَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰ إِلَى الظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّي لِمَا
أَنزَلْتَ إِلَيَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ
Fasaqa lahuma thumma tawallaila aththilli faqala rabbiinnee lima anzalta ilayya
min khayrin faqeer
Swahili
Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi!
Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia.
|
Ayah 28:25 الأية
فَجَاءَتْهُ إِحْدَاهُمَا تَمْشِي عَلَى اسْتِحْيَاءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِي
يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَاءَهُ وَقَصَّ
عَلَيْهِ الْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Fajaat-hu ihdahumatamshee AAala istihya-in qalat innaabee yadAAooka liyajziyaka
ajra ma saqayta lanafalamma jaahu waqassa AAalayhi alqasasaqala la takhaf
najawta mina alqawmi aththalimeen
Swahili
Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema: Baba
yangu anakwita akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipo mjia na akamsimulia
visa vyake, alisema: Usiogope; umekwisha okoka kwenye watu madhaalimu.
|
Ayah 28:26 الأية
قَالَتْ إِحْدَاهُمَا يَا أَبَتِ اسْتَأْجِرْهُ ۖ إِنَّ خَيْرَ مَنِ اسْتَأْجَرْتَ
الْقَوِيُّ الْأَمِينُ
Qalat ihdahuma yaabati ista/jirhu inna khayra mani ista/jarta alqawiyyu al-ameen
Swahili
Akasema mmoja katika wale wanawake: Ewe baba yetu! Muajiri huyu. Hakika mbora wa
kumuajiri ni mwenye nguvu na muaminifu.
|
Ayah 28:27 الأية
قَالَ إِنِّي أُرِيدُ أَنْ أُنكِحَكَ إِحْدَى ابْنَتَيَّ هَاتَيْنِ عَلَىٰ أَن
تَأْجُرَنِي ثَمَانِيَ حِجَجٍ ۖ فَإِنْ أَتْمَمْتَ عَشْرًا فَمِنْ عِندِكَ ۖ وَمَا
أُرِيدُ أَنْ أَشُقَّ عَلَيْكَ ۚ سَتَجِدُنِي إِن شَاءَ اللهُ مِنَ الصَّالِحِينَ
Qala innee oreedu an onkihakaihda ibnatayya hatayni AAala anta/juranee thamaniya
hijajin fa-in atmamta AAashranfamin AAindika wama oreedu an ashuqqa AAalayka
satajiduneein shaa Allahu mina assaliheen
Swahili
Akasema: Mimi nataka kukuoza mmojawapo katika binti zangu hawa wawili kwa
kunitumikia miaka minane. Ukitimiza kumi, khiari yako; lakini mimi sitaki
kukutaabisha. Inshallah utanikuta miongoni mwa watu wema.
|
Ayah 28:28 الأية
قَالَ ذَٰلِكَ بَيْنِي وَبَيْنَكَ ۖ أَيَّمَا الْأَجَلَيْنِ قَضَيْتُ فَلَا
عُدْوَانَ عَلَيَّ ۖ وَاللهُ عَلَىٰ مَا نَقُولُ وَكِيلٌ
Qala thalika baynee wabaynakaayyama al-ajalayni qadaytu fala AAudwanaAAalayya
wallahu AAala ma naqooluwakeel
Swahili
Musa akasema: Hayo yamekwisha kuwa baina yangu na wewe. Muda mmojapo nikiumaliza
sitiwi ubayani. Na Mwenyezi Mungu ni Mlinzi juu ya haya tunayo yasema.
|
Ayah 28:29 الأية
فَلَمَّا قَضَىٰ مُوسَى الْأَجَلَ وَسَارَ بِأَهْلِهِ آنَسَ مِن جَانِبِ الطُّورِ
نَارًا قَالَ لِأَهْلِهِ امْكُثُوا إِنِّي آنَسْتُ نَارًا لَّعَلِّي آتِيكُم
مِّنْهَا بِخَبَرٍ أَوْ جَذْوَةٍ مِّنَ النَّارِ لَعَلَّكُمْ تَصْطَلُونَ
Falamma qada moosaal-ajala wasara bi-ahlihi anasa min janibi attoorinaran qala
li-ahlihi omkuthoo innee anastu naranlaAAallee ateekum minha bikhabarin aw
jathwatinmina annari laAAallakum tastaloon
Swahili
Basi alipo timiza muda wake na akasafiri na ahali zake, aliona moto upande wa
Mlima T'uri. Akawaambia ahali zake: Ngojeni! Mimi nimeona moto, labda
nitakuleteeni kutoka huko khabari au kijinga cha moto ili mpate kuota moto.
|
Ayah 28:30 الأية
فَلَمَّا أَتَاهَا نُودِيَ مِن شَاطِئِ الْوَادِ الْأَيْمَنِ فِي الْبُقْعَةِ
الْمُبَارَكَةِ مِنَ الشَّجَرَةِ أَن يَا مُوسَىٰ إِنِّي أَنَا اللهُ رَبُّ
الْعَالَمِينَ
Falamma ataha noodiyamin shati-i alwadi al-aymani fee albuqAAati
almubarakatimina ashshajarati an ya moosa innee anaAllahu rabbu alAAalameen
Swahili
Basi alipo ufikia aliitwa kutoka ng'ambo ya bonde la kuliani katika eneo lilio
barikiwa kutoka kwenye mti: Ewe Musa! Hakika Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi
wa walimwengu wote.
|
Ayah 28:31 الأية
وَأَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَلَمَّا رَآهَا تَهْتَزُّ كَأَنَّهَا جَانٌّ وَلَّىٰ
مُدْبِرًا وَلَمْ يُعَقِّبْ ۚ يَا مُوسَىٰ أَقْبِلْ وَلَا تَخَفْ ۖ إِنَّكَ مِنَ
الْآمِنِينَ
Waan alqi AAasaka falamma raahatahtazzu kaannaha jannun walla mudbiranwalam
yuAAaqqib ya moosa aqbil wala takhafinnaka mina al-amineen
Swahili
Na tupa chini fimbo yako. Basi alipo iona ikitikisika kama nyoka, akarudi nyuma
wala hakutazama. (Akaambiwa): Ewe Musa! Njoo mbele wala usiogope. Hakika wewe ni
miongoni mwa walio salimika.
|
Ayah 28:32 الأية
اسْلُكْ يَدَكَ فِي جَيْبِكَ تَخْرُجْ بَيْضَاءَ مِنْ غَيْرِ سُوءٍ وَاضْمُمْ
إِلَيْكَ جَنَاحَكَ مِنَ الرَّهْبِ ۖ فَذَانِكَ بُرْهَانَانِ مِن رَّبِّكَ إِلَىٰ
فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ
Osluk yadaka fee jaybika takhruj baydaamin ghayri soo-in wadmum ilayka
janahakamina arrahbi fathanika burhanani minrabbika ila firAAawna wamala-ihi
innahum kanooqawman fasiqeen
Swahili
Ingiza mkono wako kwenye mfuko wako, utatoka mweupe pasipo na ubaya. Na
jiambatishe mkono wako ukihisi khofu. Basi hizi ni dalili mbili zitokazo kwa
Mola wako Mlezi kumpelekea Firauni na wakuu wa umma wake. Hakika hao walikuwa
watu mafaasiki.
|
Ayah 28:33 الأية
قَالَ رَبِّ إِنِّي قَتَلْتُ مِنْهُمْ نَفْسًا فَأَخَافُ أَن يَقْتُلُونِ
Qala rabbi innee qataltu minhumnafsan faakhafu an yaqtuloon
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nilimuuwa mtu katika wao, kwa hivyo
naogopa wataniuwa.
|
Ayah 28:34 الأية
وَأَخِي هَارُونُ هُوَ أَفْصَحُ مِنِّي لِسَانًا فَأَرْسِلْهُ مَعِيَ رِدْءًا
يُصَدِّقُنِي ۖ إِنِّي أَخَافُ أَن يُكَذِّبُونِ
Waakhee haroonu huwa afsahuminnee lisanan faarsilhu maAAiya rid-an
yusaddiquneeinnee akhafu an yukaththiboon
Swahili
Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume ende
nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi nina khofu watanikadhibisha.
|
Ayah 28:35 الأية
قَالَ سَنَشُدُّ عَضُدَكَ بِأَخِيكَ وَنَجْعَلُ لَكُمَا سُلْطَانًا فَلَا يَصِلُونَ
إِلَيْكُمَا ۚ بِآيَاتِنَا أَنتُمَا وَمَنِ اتَّبَعَكُمَا الْغَالِبُونَ
Qala sanashuddu AAadudakabi-akheeka wanajAAalu lakuma sultanan falayasiloona
ilaykuma bi-ayatinaantuma wamani ittabaAAakuma alghaliboon
Swahili
(Mwenyezi Mungu) akasema: Tutautia nguvu mkono wako kwa nduguyo, na tutakupeni
madaraka, hata wasikufikilieni. Kwa sababu ya Ishara zetu nyinyi na watakao
kufuateni mtashinda.
|
Ayah 28:36 الأية
فَلَمَّا جَاءَهُم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا بَيِّنَاتٍ قَالُوا مَا هَٰذَا إِلَّا
سِحْرٌ مُّفْتَرًى وَمَا سَمِعْنَا بِهَٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ
Falamma jaahum moosabi-ayatina bayyinatin qaloo mahatha illa sihrun muftaran
wamasamiAAna bihatha fee aba-inaal-awwaleen
Swahili
Basi alipo wafikia Musa na Ishara zetu, walisema: Haya si chochote ila ni uchawi
ulio zuliwa. Na hatukuyasikia haya kwa baba zetu wa zamani.
|
Ayah 28:37 الأية
وَقَالَ مُوسَىٰ رَبِّي أَعْلَمُ بِمَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ مِنْ عِندِهِ وَمَن
تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدَّارِ ۖ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ
Waqala moosa rabbee aAAlamubiman jaa bilhuda min AAindihi wamantakoonu lahu
AAaqibatu addari innahu layuflihu aththalimoon
Swahili
Na Musa akasema: Mola wangu Mlezi ni Mwenye kujua kabisa nani anaye kuja na
uwongofu unao toka kwake, na nani atakaye kuwa na mwisho mwema wa makaazi.
Hakika wenye kudhulumu hawatafanikiwa.
|
Ayah 28:38 الأية
وَقَالَ فِرْعَوْنُ يَا أَيُّهَا الْمَلَأُ مَا عَلِمْتُ لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ
غَيْرِي فَأَوْقِدْ لِي يَا هَامَانُ عَلَى الطِّينِ فَاجْعَل لِّي صَرْحًا
لَّعَلِّي أَطَّلِعُ إِلَىٰ إِلَٰهِ مُوسَىٰ وَإِنِّي لَأَظُنُّهُ مِنَ
الْكَاذِبِينَ
Waqala firAAawnu ya ayyuhaalmalao ma AAalimtu lakum min ilahin ghayreefaawqid
lee ya hamanu AAala atteenifajAAal lee sarhan laAAallee attaliAAuila ilahi moosa
wa-innee laathunnuhumina alkathibeen
Swahili
Na Firauni akasema: Enyi waheshimiwa! Sijui kama mnaye mungu asiye kuwa mimi.
Ewe Haman! Niwashie moto unichomee udongo, unijengee mnara nipate kumchungulia
mungu wa Musa. Na hakika mimi namwona yeye ni katika waongo.
|
Ayah 28:39 الأية
وَاسْتَكْبَرَ هُوَ وَجُنُودُهُ فِي الْأَرْضِ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَظَنُّوا
أَنَّهُمْ إِلَيْنَا لَا يُرْجَعُونَ
Wastakbara huwa wajunooduhu feeal-ardi bighayri alhaqqi wathannooannahum ilayna
la yurjaAAoon
Swahili
Na alipanda kiburi yeye na majeshi yake katika nchi bila ya haki, na wakadhania
kuwa hawatarudishwa kwetu.
|
Ayah 28:40 الأية
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ
عَاقِبَةُ الظَّالِمِينَ
Faakhathnahu wajunoodahufanabathnahum fee alyammi fanthurkayfa kana AAaqibatu
aththalimeen
Swahili
Basi tukamshika yeye na majeshi yake, na tukawatupa baharini. Basi hebu angalia
ulikuwaje mwisho wa wenye kudhulumu?
|
Ayah 28:41 الأية
وَجَعَلْنَاهُمْ أَئِمَّةً يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ لَا
يُنصَرُونَ
WajaAAalnahum a-immatan yadAAoona ilaannari wayawma alqiyamati la yunsaroon
Swahili
Na tuliwafanya ni waongozi waitao kwenye Moto. Na Siku ya Kiyama hawatanusuriwa.
|
Ayah 28:42 الأية
وَأَتْبَعْنَاهُمْ فِي هَٰذِهِ الدُّنْيَا لَعْنَةً ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ هُم
مِّنَ الْمَقْبُوحِينَ
WaatbaAAnahum fee hathihi addunyalaAAnatan wayawma alqiyamati hum mina
almaqbooheen
Swahili
Na tukawafuatishia laana katika dunia hii, na Siku ya Kiyama watakuwa miongoni
mwa wanao chusha.
|
Ayah 28:43 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ مِن بَعْدِ مَا أَهْلَكْنَا الْقُرُونَ
الْأُولَىٰ بَصَائِرَ لِلنَّاسِ وَهُدًى وَرَحْمَةً لَّعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Walaqad atayna moosaalkitaba min baAAdi ma ahlakna alquroonaal-oola basa-ira
linnasi wahudanwarahmatan laAAallahum yatathakkaroon
Swahili
Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha ziangamiza kaumu za
mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uwongofu, na rehema, ili wapate
kukumbuka.
|
Ayah 28:44 الأية
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الْغَرْبِيِّ إِذْ قَضَيْنَا إِلَىٰ مُوسَى الْأَمْرَ وَمَا
كُنتَ مِنَ الشَّاهِدِينَ
Wama kunta bijanibialgharbiyyi ith qadayna ila moosaal-amra wama kunta mina
ashshahideen
Swahili
Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipo mpa Musa amri, wala hukuwa katika
walio hudhuria.
|
Ayah 28:45 الأية
وَلَٰكِنَّا أَنشَأْنَا قُرُونًا فَتَطَاوَلَ عَلَيْهِمُ الْعُمُرُ ۚ وَمَا كُنتَ
ثَاوِيًا فِي أَهْلِ مَدْيَنَ تَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا وَلَٰكِنَّا كُنَّا
مُرْسِلِينَ
Walakinna ansha-naquroonan fatatawala AAalayhimu alAAumuru wama kuntathawiyan
fee ahli madyana tatloo AAalayhim ayatinawalakinna kunna mursileen
Swahili
Lakini Sisi tuliziumba kaumu, na ukawa mrefu umri juu yao. Wala hukuwa mkaazi na
watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu. Lakini ni Sisi tulio kuwa tukiwatuma
Mitume.
|
Ayah 28:46 الأية
وَمَا كُنتَ بِجَانِبِ الطُّورِ إِذْ نَادَيْنَا وَلَٰكِن رَّحْمَةً مِّن رَّبِّكَ
لِتُنذِرَ قَوْمًا مَّا أَتَاهُم مِّن نَّذِيرٍ مِّن قَبْلِكَ لَعَلَّهُمْ
يَتَذَكَّرُونَ
Wama kunta bijanibi attooriith nadayna walakin rahmatanmin rabbika litunthira
qawman ma atahum minnatheerin min qablika laAAallahum yatathakkaroon
Swahili
Wala hukuwa kando ya mlima tulipo nadi. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako
Mlezi ili uwaonye watu wasio pata kufikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda
wakakumbuka.
|
Ayah 28:47 الأية
وَلَوْلَا أَن تُصِيبَهُم مُّصِيبَةٌ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ فَيَقُولُوا
رَبَّنَا لَوْلَا أَرْسَلْتَ إِلَيْنَا رَسُولًا فَنَتَّبِعَ آيَاتِكَ وَنَكُونَ
مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Walawla an tuseebahum museebatunbima qaddamat aydeehim fayaqooloo rabbana
lawlaarsalta ilayna rasoolan fanattabiAAa ayatikawanakoona mina almu/mineen
Swahili
Na usije kuwasibu msiba kwa iliyo yatanguliza mikono yao, wakasema: Ewe Mola
wetu Mlezi! Mbona hukututumia Mtume nasi, tukafuata Ishara zako, na tukawa
miongoni mwa Waumini?
|
Ayah 28:48 الأية
فَلَمَّا جَاءَهُمُ الْحَقُّ مِنْ عِندِنَا قَالُوا لَوْلَا أُوتِيَ مِثْلَ مَا
أُوتِيَ مُوسَىٰ ۚ أَوَلَمْ يَكْفُرُوا بِمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ مِن قَبْلُ ۖ قَالُوا
سِحْرَانِ تَظَاهَرَا وَقَالُوا إِنَّا بِكُلٍّ كَافِرُونَ
Falamma jaahumu alhaqqumin AAindina qaloo lawla ootiya mithla maootiya moosa awa
lam yakfuroo bima ootiya moosamin qablu qaloo sihrani tathaharawaqaloo inna
bikullin kafiroon
Swahili
Ilipo wajia Haki kutoka kwetu walisema: Mbona hakupewa kama aliyo pewa Musa? Je!
Kwani wao hawakuyakataa aliyo pewa Musa zamani? Walisema: Ni wachawi wawili
wanasaidiana. Na wakasema: Hakika sisi tunawakataa wote.
|
Ayah 28:49 الأية
قُلْ فَأْتُوا بِكِتَابٍ مِّنْ عِندِ اللهِ هُوَ أَهْدَىٰ مِنْهُمَا أَتَّبِعْهُ
إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Qul fa/too bikitabin min AAindi Allahihuwa ahda minhuma attabiAAhu in kuntum
sadiqeen
Swahili
Sema: Basi leteni Kitabu kinacho toka kwa Mwenyezi Mungu chenye kuongoka zaidi
kuliko hivi viwili tukifuate, kama nyinyi mnasema kweli.
|
Ayah 28:50 الأية
فَإِن لَّمْ يَسْتَجِيبُوا لَكَ فَاعْلَمْ أَنَّمَا يَتَّبِعُونَ أَهْوَاءَهُمْ ۚ
وَمَنْ أَضَلُّ مِمَّنِ اتَّبَعَ هَوَاهُ بِغَيْرِ هُدًى مِّنَ اللهِ ۚ إِنَّ
اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ
Fa-in lam yastajeeboo laka faAAlamannama yattabiAAoona ahwaahum waman
adallumimmani ittabaAAa hawahu bighayri hudan mina Allahiinna Allaha la yahdee
alqawma aththalimeen
Swahili
Na ikiwa hawakuitikii, basi jua kuwa wanafuata pumbao lao tu. Na nani aliye
potea zaidi kumshinda anaye fuata pumbao lake bila ya uwongofu utokao kwa
Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wenye kudhulumu.
|
Ayah 28:51 الأية
وَلَقَدْ وَصَّلْنَا لَهُمُ الْقَوْلَ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Walaqad wassalna lahumualqawla laAAallahum yatathakkaroon
Swahili
Na sasa kwa yakini tumewafikishia Neno ili wapate kukumbuka.
|
Ayah 28:52 الأية
الَّذِينَ آتَيْنَاهُمُ الْكِتَابَ مِن قَبْلِهِ هُم بِهِ يُؤْمِنُونَ
Allatheena ataynahumualkitaba min qablihi hum bihi yu/minoon
Swahili
Wale tulio wapa Kitabu kabla yake wanakiamini hiki.
|
Ayah 28:53 الأية
وَإِذَا يُتْلَىٰ عَلَيْهِمْ قَالُوا آمَنَّا بِهِ إِنَّهُ الْحَقُّ مِن رَّبِّنَا
إِنَّا كُنَّا مِن قَبْلِهِ مُسْلِمِينَ
Wa-itha yutla AAalayhim qalooamanna bihi innahu alhaqqu min rabbinainna kunna
min qablihi muslimeen
Swahili
Na wanapo somewa wanasema: Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayo toka kwa Mola
wetu Mlezi. Hakika sisi kabla yake tulikuwa ni Waislamu, tulio nyenyekea.
|
Ayah 28:54 الأية
أُولَٰئِكَ يُؤْتَوْنَ أَجْرَهُم مَّرَّتَيْنِ بِمَا صَبَرُوا وَيَدْرَءُونَ
بِالْحَسَنَةِ السَّيِّئَةَ وَمِمَّا رَزَقْنَاهُمْ يُنفِقُونَ
Ola-ika yu/tawna ajrahum marrataynibima sabaroo wayadraoona
bilhasanatiassayyi-ata wamimma razaqnahum yunfiqoon
Swahili
Basi hao watapewa ujira wao mara mbili kwa walivyo vumilia, na wakaondoa ubaya
kwa wema, na wakatoa katika tuliyo waruzuku.
|
Ayah 28:55 الأية
وَإِذَا سَمِعُوا اللَّغْوَ أَعْرَضُوا عَنْهُ وَقَالُوا لَنَا أَعْمَالُنَا
وَلَكُمْ أَعْمَالُكُمْ سَلَامٌ عَلَيْكُمْ لَا نَبْتَغِي الْجَاهِلِينَ
Wa-itha samiAAoo allaghwa aAAradooAAanhu waqaloo lana aAAmaluna
walakumaAAmalukum salamun AAalaykum la nabtagheealjahileen
Swahili
Na wanapo sikia upuuzi hujitenga nao na husema: Sisi tuna vitendo vyetu, na
nyinyi mna vitendo vyenu. Salamun Alaikum, Amani juu yenu! Sisi hatutaki
kujibizana na wajinga.
|
Ayah 28:56 الأية
إِنَّكَ لَا تَهْدِي مَنْ أَحْبَبْتَ وَلَٰكِنَّ اللهَ يَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ
وَهُوَ أَعْلَمُ بِالْمُهْتَدِينَ
Innaka la tahdee man ahbabtawalakinna Allaha yahdee man yashao wahuwaaAAlamu
bilmuhtadeen
Swahili
Kwa hakika wewe humwongoi umpendaye, lakini Mwenyezi Mungu humwongoa amtakaye.
Na Yeye ndiye anawajua zaidi waongokao.
|
Ayah 28:57 الأية
وَقَالُوا إِن نَّتَّبِعِ الْهُدَىٰ مَعَكَ نُتَخَطَّفْ مِنْ أَرْضِنَا ۚ أَوَلَمْ
نُمَكِّن لَّهُمْ حَرَمًا آمِنًا يُجْبَىٰ إِلَيْهِ ثَمَرَاتُ كُلِّ شَيْءٍ
رِّزْقًا مِّن لَّدُنَّا وَلَٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ
Waqaloo in nattabiAAi alhudamaAAaka nutakhattaf min ardina awa lamnumakkin lahum
haraman aminan yujba ilayhithamaratu kulli shay-in rizqan min ladunna
walakinnaaktharahum la yaAAlamoon
Swahili
Na wakasema: Tukiufuata uwongofu huu pamoja nawe tutanyakuliwa kutoka nchi yetu.
Je! Kwani Sisi hatukuwaweka imara katika pahala patakatifu, penye amani, ambapo
huletewa matunda ya kila aina kuwa ni riziki itokayo kwetu? Lakini wengi wao
hawajui.
|
Ayah 28:58 الأية
وَكَمْ أَهْلَكْنَا مِن قَرْيَةٍ بَطِرَتْ مَعِيشَتَهَا ۖ فَتِلْكَ مَسَاكِنُهُمْ
لَمْ تُسْكَن مِّن بَعْدِهِمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ وَكُنَّا نَحْنُ الْوَارِثِينَ
Wakam ahlakna min qaryatin batiratmaAAeeshataha fatilka masakinuhum lam tuskan
minbaAAdihim illa qaleelan wakunna nahnu alwaritheen
Swahili
Na miji mingapi iliyo jifakharisha tumeiangamiza! Na hayo maskani yao
hayakukaliwa tena baada yao, ila kwa uchache tu. Na Sisi ndio tumekuwa warithi
wao.
|
Ayah 28:59 الأية
وَمَا كَانَ رَبُّكَ مُهْلِكَ الْقُرَىٰ حَتَّىٰ يَبْعَثَ فِي أُمِّهَا رَسُولًا
يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِنَا ۚ وَمَا كُنَّا مُهْلِكِي الْقُرَىٰ إِلَّا
وَأَهْلُهَا ظَالِمُونَ
Wama kana rabbuka muhlikaalqura hatta yabAAatha fee ommiharasoolan yatloo
AAalayhim ayatina wamakunna muhlikee alqura illa waahluha thalimoon
Swahili
Na Mola wako Mlezi haangamizi miji mpaka ampeleke Mtume katika miji yake mikuu
awasomee Ishara zetu. Wala hatuiangamizi miji mpaka watu wake wawe madhaalimu.
|
Ayah 28:60 الأية
وَمَا أُوتِيتُم مِّن شَيْءٍ فَمَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَزِينَتُهَا ۚ وَمَا
عِندَ اللهِ خَيْرٌ وَأَبْقَىٰ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Wama ooteetum min shay-in famataAAualhayati addunya wazeenatuhawama AAinda
Allahi khayrun waabqa afalataAAqiloon
Swahili
Na chochote mlicho pewa ni matumizi ya maisha ya dunia na pambo lake. Na
yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ndio bora na yatakayo baki zaidi. Basi je,
hamfahamu?
|
Ayah 28:61 الأية
أَفَمَن وَعَدْنَاهُ وَعْدًا حَسَنًا فَهُوَ لَاقِيهِ كَمَن مَّتَّعْنَاهُ مَتَاعَ
الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ثُمَّ هُوَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ مِنَ الْمُحْضَرِينَ
Afaman waAAadnahu waAAdan hasananfahuwa laqeehi kaman mattaAAnahu mataAAa
alhayatiaddunya thumma huwa yawma alqiyamati minaalmuhdareen
Swahili
Je! Yule tuliye muahidi ahadi nzuri, tena naye akayapata, ni kama tuliye
mstarehesha kwa starehe za maisha ya duniani, na kisha Siku ya Kiyama akawa
miongoni mwa wanao hudhurishwa?
|
Ayah 28:62 الأية
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
Wayawma yunadeehim fayaqoolu aynashuraka-iya allatheena kuntum tazAAumoon
Swahili
Na siku atakapo waita na akasema: Wako wapi mlio kuwa mkidai kuwa ni washirika
wangu?
|
Ayah 28:63 الأية
قَالَ الَّذِينَ حَقَّ عَلَيْهِمُ الْقَوْلُ رَبَّنَا هَٰؤُلَاءِ الَّذِينَ
أَغْوَيْنَا أَغْوَيْنَاهُمْ كَمَا غَوَيْنَا ۖ تَبَرَّأْنَا إِلَيْكَ ۖ مَا
كَانُوا إِيَّانَا يَعْبُدُونَ
Qala allatheena haqqaAAalayhimu alqawlu rabbana haola-i allatheenaaghwayna
aghwaynahum kama ghawaynatabarra/na ilayka ma kanoo iyyanayaAAbudoon
Swahili
Watasema wale iliyo thibiti juu yao kauli: Mola wetu Mlezi! Hawa ndio tulio
wapoteza. Tuliwapoteza kama tulivyo potea sisi. Tunajitenga nao mbele yako.
Hawakuwa wakituabudu sisi.
|
Ayah 28:64 الأية
وَقِيلَ ادْعُوا شُرَكَاءَكُمْ فَدَعَوْهُمْ فَلَمْ يَسْتَجِيبُوا لَهُمْ وَرَأَوُا
الْعَذَابَ ۚ لَوْ أَنَّهُمْ كَانُوا يَهْتَدُونَ
Waqeela odAAoo shurakaakumfadaAAawhum falam yastajeeboo lahum waraawoo
alAAathabalaw annahum kanoo yahtadoon
Swahili
Na itasemwa: Waiteni hao miungu wa kishirikina wenu! Basi watawaita, lakini
hawatawaitikia, na wataiona adhabu; laiti wangeli kuwa wameongoka!
|
Ayah 28:65 الأية
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ مَاذَا أَجَبْتُمُ الْمُرْسَلِينَ
Wayawma yunadeehim fayaqoolu mathaajabtumu almursaleen
Swahili
Na siku atapo waita na akasema: Mliwajibu nini Mitume?
|
Ayah 28:66 الأية
فَعَمِيَتْ عَلَيْهِمُ الْأَنبَاءُ يَوْمَئِذٍ فَهُمْ لَا يَتَسَاءَلُونَ
FaAAamiyat AAalayhimu al-anbaoyawma-ithin fahum la yatasaaloon
Swahili
Basi zitawapotea khabari siku hiyo, nao hawataulizana.
|
Ayah 28:67 الأية
فَأَمَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا فَعَسَىٰ أَن يَكُونَ مِنَ
الْمُفْلِحِينَ
Faamma man taba waamanawaAAamila salihan faAAasa an yakoona minaalmufliheen
Swahili
Ama mwenye kutubu na akaamini na akatenda mema, huyo atakuwa miongoni mwa wenye
kufanikiwa.
|
Ayah 28:68 الأية
وَرَبُّكَ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ وَيَخْتَارُ ۗ مَا كَانَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ ۚ
سُبْحَانَ اللهِ وَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
Warabbuka yakhluqu ma yashaowayakhtaru ma kana lahumu alkhiyaratu subhanaAllahi
wataAAala AAamma yushrikoon
Swahili
Na Mola wako Mlezi huumba na huteuwa atakavyo. Viumbe hawana khiari. Mwenyezi
Mungu ametukuka na ametakasika na hao wanao washirikisha naye.
|
Ayah 28:69 الأية
وَرَبُّكَ يَعْلَمُ مَا تُكِنُّ صُدُورُهُمْ وَمَا يُعْلِنُونَ
Warabbuka yaAAlamu ma tukinnu sudooruhumwama yuAAlinoon
Swahili
Na Mola wako Mlezi anayajua yaliyo ficha vifua vyao, na wanayo yatangaza.
|
Ayah 28:70 الأية
وَهُوَ اللهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْحَمْدُ فِي الْأُولَىٰ
وَالْآخِرَةِ ۖ وَلَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Wahuwa Allahu la ilahailla huwa lahu alhamdu fee al-oola wal-akhiratiwalahu
alhukmu wa-ilayhi turjaAAoon
Swahili
Naye ni Mwenyezi Mungu ambaye hapana mungu isipo kuwa Yeye. Sifa zote njema ni
zake Yeye, mwanzo na mwisho. Na hukumu ni yake Yeye. Na kwake Yeye mtarejeshwa.
|
Ayah 28:71 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللهُ عَلَيْكُمُ اللَّيْلَ سَرْمَدًا إِلَىٰ
يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ اللهِ يَأْتِيكُم بِضِيَاءٍ ۖ أَفَلَا
تَسْمَعُونَ
Qul araaytum in jaAAala AllahuAAalaykumu allayla sarmadan ila yawmi
alqiyamatiman ilahun ghayru Allahi ya/teekum bidiya-inafala tasmaAAoon
Swahili
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya usiku umekukalieni moja kwa moja
mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu atakaye kuleteeni
mwangaza? Basi je, hamsikii?
|
Ayah 28:72 الأية
قُلْ أَرَأَيْتُمْ إِن جَعَلَ اللهُ عَلَيْكُمُ النَّهَارَ سَرْمَدًا إِلَىٰ
يَوْمِ الْقِيَامَةِ مَنْ إِلَٰهٌ غَيْرُ اللهِ يَأْتِيكُم بِلَيْلٍ تَسْكُنُونَ
فِيهِ ۖ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Qul araaytum in jaAAala AllahuAAalaykumu annahara sarmadan ila yawmialqiyamati
man ilahun ghayru Allahiya/teekum bilaylin taskunoona feehi afala tubsiroon
Swahili
Sema: Mwaonaje, Mwenyezi Mungu angeli ufanya mchana umekukalieni moja kwa moja
mpaka Siku ya Kiyama, mungu gani asiye kuwa Mwenyezi Mungu ataye kuleteeni usiku
mkapumzika humo? Basi je, hamwoni?
|
Ayah 28:73 الأية
وَمِن رَّحْمَتِهِ جَعَلَ لَكُمُ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لِتَسْكُنُوا فِيهِ
وَلِتَبْتَغُوا مِن فَضْلِهِ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ
Wamin rahmatihi jaAAala lakumuallayla wannahara litaskunoo feehi
walitabtaghoomin fadlihi walaAAallakum tashkuroon
Swahili
Na ni katika rehema zake amekufanyieni usiku na mchana mpate kupumzika humo na
mtafute fadhila zake, na ili mpate kushukuru.
|
Ayah 28:74 الأية
وَيَوْمَ يُنَادِيهِمْ فَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَائِيَ الَّذِينَ كُنتُمْ تَزْعُمُونَ
Wayawma yunadeehim fayaqoolu aynashuraka-iya allatheena kuntum tazAAumoon
Swahili
Na siku atakapo waita na akasema: Wako wapi hao mlio kuwa mkidai kuwa ni
washirika wangu?
|
Ayah 28:75 الأية
وَنَزَعْنَا مِن كُلِّ أُمَّةٍ شَهِيدًا فَقُلْنَا هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ
فَعَلِمُوا أَنَّ الْحَقَّ لِلَّهِ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ
WanazaAAna min kulli ommatinshaheedan faqulna hatoo burhanakumfaAAalimoo anna
alhaqqa lillahi wadallaAAanhum ma kanoo yaftaroon
Swahili
Na tutatoa shahidi katika kila umma, na tutasema: Leteni hoja zenu! Hapo watajua
kwamba hakika kweli ni ya Mwenyezi Mungu, na yatawapotea yale waliyo kuwa
wakiyazua.
|
Ayah 28:76 الأية
إِنَّ قَارُونَ كَانَ مِن قَوْمِ مُوسَىٰ فَبَغَىٰ عَلَيْهِمْ ۖ وَآتَيْنَاهُ مِنَ
الْكُنُوزِ مَا إِنَّ مَفَاتِحَهُ لَتَنُوءُ بِالْعُصْبَةِ أُولِي الْقُوَّةِ إِذْ
قَالَ لَهُ قَوْمُهُ لَا تَفْرَحْ ۖ إِنَّ اللهَ لَا يُحِبُّ الْفَرِحِينَ
Inna qaroona kana min qawmimoosa fabagha AAalayhim waataynahumina alkunoozi ma
inna mafatihahu latanoo-obilAAusbati olee alquwwati ith qalalahu qawmuhu la
tafrah inna Allaha layuhibbu alfariheen
Swahili
Hakika Qaruni alikuwa katika watu wa Musa, lakini aliwafanyia dhulma. Na tulimpa
khazina ambazo funguo zake zinawatopeza watu wenye nguvu kuzichukua. Walipo
mwambia watu wake: Usijigambe! Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wanao jigamba.
|
Ayah 28:77 الأية
وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ
الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ
فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ
Wabtaghi feema atakaAllahu addara al-akhirata walatansa naseebaka mina addunya
waahsinkama ahsana Allahu ilayka wala tabghialfasada fee al-ardi inna Allaha
layuhibbu almufsideen
Swahili
Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau
fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema
wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu
hawapendi mafisadi.
|
Ayah 28:78 الأية
قَالَ إِنَّمَا أُوتِيتُهُ عَلَىٰ عِلْمٍ عِندِي ۚ أَوَلَمْ يَعْلَمْ أَنَّ اللهَ
قَدْ أَهْلَكَ مِن قَبْلِهِ مِنَ الْقُرُونِ مَنْ هُوَ أَشَدُّ مِنْهُ قُوَّةً
وَأَكْثَرُ جَمْعًا ۚ وَلَا يُسْأَلُ عَن ذُنُوبِهِمُ الْمُجْرِمُونَ
Qala innama ooteetuhu AAalaAAilmin AAindee awa lam yaAAlam anna Allaha qad
ahlaka minqablihi mina alqurooni man huwa ashaddu minhu quwwatan
waaktharujamAAan wala yus-alu AAan thunoobihimu almujrimoon
Swahili
Akasema: Kwa hakika nimepewa haya kwa sababu ya ilimu niliyo nayo. Je! Hakujua
kwamba Mwenyezi Mungu kesha waangamiza, katika vizazi vya walio kabla yake, watu
walio kuwa wenye ngubvu zaidi kuliko yeye, na wenye makundi makubwa zaidi kuliko
yake. Na wakosefu hawataulizwa khabari ya dhambi zao.
|
Ayah 28:79 الأية
فَخَرَجَ عَلَىٰ قَوْمِهِ فِي زِينَتِهِ ۖ قَالَ الَّذِينَ يُرِيدُونَ الْحَيَاةَ
الدُّنْيَا يَا لَيْتَ لَنَا مِثْلَ مَا أُوتِيَ قَارُونُ إِنَّهُ لَذُو حَظٍّ
عَظِيمٍ
Fakharaja AAala qawmihi fee zeenatihiqala allatheena yureedoona alhayata
addunyaya layta lana mithla ma ootiya qaroonuinnahu lathoo haththin AAatheem
Swahili
Basi akawatokea watu wake katika pambo lake. Wakasema wale walio kuwa wanataka
maisha ya duniani: Laiti tungeli kuwa tunayo kama aliyo pewa Qaruni! Hakika yeye
ni mwenye bahati kubwa.
|
Ayah 28:80 الأية
وَقَالَ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَيْلَكُمْ ثَوَابُ اللهِ خَيْرٌ لِّمَنْ
آمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا وَلَا يُلَقَّاهَا إِلَّا الصَّابِرُونَ
Waqala allatheena ootooalAAilma waylakum thawabu Allahi khayrun liman
amanawaAAamila salihan wala yulaqqahailla assabiroon
Swahili
Na wakasema wale walio pewa ilimu: Ole wenu! Malipo ya Mwenyezi Mungu ni bora
kwa mwenye kuamini na akatenda mema. Wala hawatapewa hayo isipo kuwa wenye
subira.
|
Ayah 28:81 الأية
فَخَسَفْنَا بِهِ وَبِدَارِهِ الْأَرْضَ فَمَا كَانَ لَهُ مِن فِئَةٍ يَنصُرُونَهُ
مِن دُونِ اللهِ وَمَا كَانَ مِنَ الْمُنتَصِرِينَ
Fakhasafna bihi wabidarihial-arda fama kana lahu min fi-atin yansuroonahumin
dooni Allahi wama kana mina almuntasireen
Swahili
Basi tukamdidimiza yeye na nyumba yake katika ardhi; wala halikuwepo kundi
lolote la kumnusuru kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa wanao jitetea.
|
Ayah 28:82 الأية
وَأَصْبَحَ الَّذِينَ تَمَنَّوْا مَكَانَهُ بِالْأَمْسِ يَقُولُونَ وَيْكَأَنَّ
اللهَ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ ۖ لَوْلَا أَن
مَّنَّ اللهُ عَلَيْنَا لَخَسَفَ بِنَا ۖ وَيْكَأَنَّهُ لَا يُفْلِحُ
الْكَافِرُونَ
Waasbaha allatheenatamannaw makanahu bil-amsi yaqooloona waykaannaAllaha yabsutu
arrizqa liman yashaomin AAibadihi wayaqdiru lawla an manna AllahuAAalayna
lakhasafa bina waykaannahu la yuflihualkafiroon
Swahili
Na wale walio tamani kuwa pahala pake jana, wakawa wanasema: Kumbe Mwenyezi
Mungu humkunjulia riziki amtakaye katika waja wake, na humdhikisha amtakaye.
Ingeli kuwa Mwenyezi Mungu hakutufanyia hisani angeli tudidimiza. Kumbe makafiri
hawafanikiwi!
|
Ayah 28:83 الأية
تِلْكَ الدَّارُ الْآخِرَةُ نَجْعَلُهَا لِلَّذِينَ لَا يُرِيدُونَ عُلُوًّا فِي
الْأَرْضِ وَلَا فَسَادًا ۚ وَالْعَاقِبَةُ لِلْمُتَّقِينَ
Tilka addaru al-akhiratunajAAaluha lillatheena la yureedoonaAAuluwwan fee
al-ardi wala fasadan walAAaqibatulilmuttaqeen
Swahili
Hayo ndiyo makaazi ya Akhera, tumewafanyia wale wasio taka kujitukuza duniani
wala ufisadi. Na mwisho mwema ni wa wachamngu.
|
Ayah 28:84 الأية
مَن جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ خَيْرٌ مِّنْهَا ۖ وَمَن جَاءَ بِالسَّيِّئَةِ
فَلَا يُجْزَى الَّذِينَ عَمِلُوا السَّيِّئَاتِ إِلَّا مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Man jaa bilhasanatifalahu khayrun minha waman jaa bissayyi-atifala yujza
allatheena AAamiloo assayyi-atiilla ma kanoo yaAAmaloon
Swahili
Atakaye tenda wema atapata malipo bora kuliko huo wema alio utenda. Na atakaye
tenda uovu, hawalipwi watendao uovu ila waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 28:85 الأية
إِنَّ الَّذِي فَرَضَ عَلَيْكَ الْقُرْآنَ لَرَادُّكَ إِلَىٰ مَعَادٍ ۚ قُل رَّبِّي
أَعْلَمُ مَن جَاءَ بِالْهُدَىٰ وَمَنْ هُوَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Inna allathee farada AAalaykaalqur-ana laradduka ila maAAadin qulrabbee aAAlamu
man jaa bilhuda waman huwafee dalalin mubeen
Swahili
Hakika aliye kulazimisha kuifuata Qur'ani hapana shaka atakurudisha pahala pa
marejeo. Sema: Mola wangu Mlezi ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuja na uwongofu,
na nani aliyomo katika upotofu ulio dhaahiri.
|
Ayah 28:86 الأية
وَمَا كُنتَ تَرْجُو أَن يُلْقَىٰ إِلَيْكَ الْكِتَابُ إِلَّا رَحْمَةً مِّن
رَّبِّكَ ۖ فَلَا تَكُونَنَّ ظَهِيرًا لِّلْكَافِرِينَ
Wama kunta tarjoo an yulqailayka alkitabu illa rahmatan min rabbikafala
takoonanna thaheeran lilkafireen
Swahili
Nawe hukuwa unataraji kuletewa Kitabu; lakini ni rehema tu ya Mola wako Mlezi.
Basi usiwe msaidizi wa makafiri.
|
Ayah 28:87 الأية
وَلَا يَصُدُّنَّكَ عَنْ آيَاتِ اللهِ بَعْدَ إِذْ أُنزِلَتْ إِلَيْكَ ۖ وَادْعُ
إِلَىٰ رَبِّكَ ۖ وَلَا تَكُونَنَّ مِنَ الْمُشْرِكِينَ
Wala yasuddunnaka AAan ayatiAllahi baAAda ith onzilat ilayka wadAAu ilarabbika
wala takoonanna mina almushrikeen
Swahili
Wala wasikuzuie kuzifuata Aya za Mwenyezi Mungu baada ya kuteremshiwa wewe. Na
lingania kwa Mola wako Mlezi, wala usiwe miongoni mwa washirikina.
|
Ayah 28:88 الأية
وَلَا تَدْعُ مَعَ اللهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۘ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ كُلُّ
شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ ۚ لَهُ الْحُكْمُ وَإِلَيْهِ تُرْجَعُونَ
Wala tadAAu maAAa Allahi ilahanakhara la ilaha illa huwa kullushay-in halikun
illa wajhahu lahu alhukmuwa-ilayhi turjaAAoon
Swahili
Wala usimwombe pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwenginewe. Hapana mungu ila Yeye.
Kila kitu kitaangamia isipo kuwa Yeye. Hukumu iko kwake, na kwake mtarejezwa.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|
|