1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
المص
Alif-lam-meem-sad
Swahili
ALIF LAM MYM 'SAAD
|
Ayah 7:2 الأية
كِتَابٌ أُنزِلَ إِلَيْكَ فَلَا يَكُن فِي صَدْرِكَ حَرَجٌ مِّنْهُ لِتُنذِرَ بِهِ
وَذِكْرَىٰ لِلْمُؤْمِنِينَ
Kitabun onzila ilayka falayakun fee sadrika harajun minhu litunthirabihi
wathikra lilmu/mineen
Swahili
Kitabu kilicho teremshwa kwako - basi isiwe dhiki kifuani kwako kwa ajili yake,
upate kuonya kwacho, na kiwe ni ukumbusho kwa Waumini.
|
Ayah 7:3 الأية
اتَّبِعُوا مَا أُنزِلَ إِلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ وَلَا تَتَّبِعُوا مِن دُونِهِ
أَوْلِيَاءَ ۗ قَلِيلًا مَّا تَذَكَّرُونَ
IttabiAAoo ma onzila ilaykum minrabbikum wala tattabiAAoo min doonihi
awliyaaqaleelan ma tathakkaroon
Swahili
Fuateni mliyo teremshiwa kutoka kwa Mola Mlezi wenu, wala msifuate rafiki au
walinzi wengine badala yake. Ni machache mnayo yakumbuka.
|
Ayah 7:4 الأية
وَكَم مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَاهَا فَجَاءَهَا بَأْسُنَا بَيَاتًا أَوْ هُمْ
قَائِلُونَ
Wakam min qaryatin ahlaknahafajaaha ba/suna bayatan aw hum qa-iloon
Swahili
Na miji mingapi tuliiangamiza, ikaifikia adhabu yetu usiku au walipo kuwa
wamelala adhuhuri.
|
Ayah 7:5 الأية
فَمَا كَانَ دَعْوَاهُمْ إِذْ جَاءَهُم بَأْسُنَا إِلَّا أَن قَالُوا إِنَّا كُنَّا
ظَالِمِينَ
Fama kana daAAwahum ithjaahum ba/suna illa an qaloo innakunna thalimeen
Swahili
Basi hakikuwa kilio chao ilipo wafikia adhabu yetu, isipo kuwa kusema: Hakika
sisi tulikuwa wenye kudhulumu.
|
Ayah 7:6 الأية
فَلَنَسْأَلَنَّ الَّذِينَ أُرْسِلَ إِلَيْهِمْ وَلَنَسْأَلَنَّ الْمُرْسَلِينَ
Falanas-alanna allatheena orsilailayhim walanas-alanna almursaleen
Swahili
Na kwa yakini tutawauliza wale walio pelekewa Ujumbe, na pia tutawauliza hao
Wajumbe.
|
Ayah 7:7 الأية
فَلَنَقُصَّنَّ عَلَيْهِم بِعِلْمٍ ۖ وَمَا كُنَّا غَائِبِينَ
Falanaqussanna AAalayhim biAAilmin wamakunna gha-ibeen
Swahili
Tena tutawasimulia kwa ilimu; wala Sisi hatukuwa mbali.
|
Ayah 7:8 الأية
وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ
الْمُفْلِحُونَ
Walwaznu yawma-ithini alhaqqufaman thaqulat mawazeenuhu faola-ika humu
almuflihoon
Swahili
Na Siku hiyo kipimo kitakuwa kwa Haki. Basi watakao kuwa na uzani mzito, hao
ndio watakao fanikiwa.
|
Ayah 7:9 الأية
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا
كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ
Waman khaffat mawazeenuhu faola-ikaallatheena khasiroo anfusahum bima kanoo
bi-ayatinayathlimoon
Swahili
Na watakao kuwa na uzani khafifu, basi hao ndio walio zitia khasarani nafsi zao
kwa sababu ya kuzipinga Ishara zetu.
|
Ayah 7:10 الأية
وَلَقَدْ مَكَّنَّاكُمْ فِي الْأَرْضِ وَجَعَلْنَا لَكُمْ فِيهَا مَعَايِشَ ۗ
قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
Walaqad makkannakum fee al-ardiwajaAAalna lakum feeha maAAayisha qaleelan
matashkuroon
Swahili
Na hakika tumekuwekeni katika ardhi, na tumekujaalieni humo njia za kupatia
maisha. Ni kuchache kushukuru kwenu.
|
Ayah 7:11 الأية
وَلَقَدْ خَلَقْنَاكُمْ ثُمَّ صَوَّرْنَاكُمْ ثُمَّ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ
اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ لَمْ يَكُن مِّنَ السَّاجِدِينَ
Walaqad khalaqnakum thumma sawwarnakumthumma qulna lilmala-ikati osjudoo
li-adamafasajadoo illa ibleesa lam yakun mina assajideen
Swahili
Na hakika tulikuumbeni, kisha tukakutieni sura, kisha tukawaambia Malaika:
Msujudieni Adam. Basi wakasujudu isipo kuwa Iblisi, hakuwa miongoni mwa walio
sujudu.
|
Ayah 7:12 الأية
قَالَ مَا مَنَعَكَ أَلَّا تَسْجُدَ إِذْ أَمَرْتُكَ ۖ قَالَ أَنَا خَيْرٌ مِّنْهُ
خَلَقْتَنِي مِن نَّارٍ وَخَلَقْتَهُ مِن طِينٍ
Qala ma manaAAaka allatasjuda ith amartuka qala ana khayrun minhukhalaqtanee min
narin wakhalaqtahu min teen
Swahili
Mwenyezi Mungu akasema: Nini kilicho kuzuia kumsujudia nilipo kuamrisha?
Akasema: Mimi ni bora kuliko yeye. Umeniumba kwa moto, naye umemuumba kwa
udongo.
|
Ayah 7:13 الأية
قَالَ فَاهْبِطْ مِنْهَا فَمَا يَكُونُ لَكَ أَن تَتَكَبَّرَ فِيهَا فَاخْرُجْ
إِنَّكَ مِنَ الصَّاغِرِينَ
Qala fahbit minhafama yakoonu laka an tatakabbara feeha fakhrujinnaka mina
assaghireen
Swahili
Akasema: Basi teremka kutoka humo! Haikufalii kufanya kiburi humo. Basi toka!
Hakika wewe u miongoni mwa walio duni.
|
Ayah 7:14 الأية
قَالَ أَنظِرْنِي إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
Qala anthirnee ilayawmi yubAAathoon
Swahili
Akasema: Nipe muhula mpaka siku watakapo fufuliwa.
|
Ayah 7:15 الأية
قَالَ إِنَّكَ مِنَ الْمُنظَرِينَ
Qala innaka mina almunthareen
Swahili
Akasema: Utakuwa miongoni mwa walio pewa muhula.
|
Ayah 7:16 الأية
قَالَ فَبِمَا أَغْوَيْتَنِي لَأَقْعُدَنَّ لَهُمْ صِرَاطَكَ الْمُسْتَقِيمَ
Qala fabima aghwaytaneelaaqAAudanna lahum sirataka almustaqeem
Swahili
Akasema: Kwa kuwa umenihukumia upotofu, basi nitawavizia katika Njia yako Iliyo
Nyooka.
|
Ayah 7:17 الأية
ثُمَّ لَآتِيَنَّهُم مِّن بَيْنِ أَيْدِيهِمْ وَمِنْ خَلْفِهِمْ وَعَنْ
أَيْمَانِهِمْ وَعَن شَمَائِلِهِمْ ۖ وَلَا تَجِدُ أَكْثَرَهُمْ شَاكِرِينَ
Thumma laatiyannahum min bayniaydeehim wamin khalfihim waAAan aymanihim waAAan
shama-ilihimwala tajidu aktharahum shakireen
Swahili
Kisha nitawazukia mbele yao na nyuma yao na kuliani kwao na kushotoni kwao. Wala
hutawakuta wengi wao wenye shukrani.
|
Ayah 7:18 الأية
قَالَ اخْرُجْ مِنْهَا مَذْءُومًا مَّدْحُورًا ۖ لَّمَن تَبِعَكَ مِنْهُمْ
لَأَمْلَأَنَّ جَهَنَّمَ مِنكُمْ أَجْمَعِينَ
Qala okhruj minha mathoomanmadhooran laman tabiAAaka minhum laamlaanna
jahannamaminkum ajmaAAeen
Swahili
Akasema: Toka humo, nawe umekwisha fedheheka, umekwisha fukuzwa. Hapana shaka
atakaye kufuata miongoni mwao, basi nitaijaza Jahannam kwa nyinyi nyote.
|
Ayah 7:19 الأية
وَيَا آدَمُ اسْكُنْ أَنتَ وَزَوْجُكَ الْجَنَّةَ فَكُلَا مِنْ حَيْثُ شِئْتُمَا
وَلَا تَقْرَبَا هَٰذِهِ الشَّجَرَةَ فَتَكُونَا مِنَ الظَّالِمِينَ
Waya adamu oskun antawazawjuka aljannata fakula min haythu shi/tumawala taqraba
hathihi ashshajaratafatakoona mina aththalimeen
Swahili
Na wewe, Adam! Kaa wewe na mkeo katika Bustani hii, na kuleni humo mpendapo.
Wala msiukaribie mti huu, mkawa katika wale walio dhulumu.
|
Ayah 7:20 الأية
فَوَسْوَسَ لَهُمَا الشَّيْطَانُ لِيُبْدِيَ لَهُمَا مَا وُورِيَ عَنْهُمَا مِن
سَوْآتِهِمَا وَقَالَ مَا نَهَاكُمَا رَبُّكُمَا عَنْ هَٰذِهِ الشَّجَرَةِ إِلَّا
أَن تَكُونَا مَلَكَيْنِ أَوْ تَكُونَا مِنَ الْخَالِدِينَ
Fawaswasa lahuma ashshaytanuliyubdiya lahuma ma wooriya AAanhuma minsaw-atihima
waqala ma nahakumarabbukuma AAan hathihi ashshajarati illaan takoona malakayni
aw takoona mina alkhalideen
Swahili
Basi Shet'ani aliwatia wasiwasi ili kuwafichulia tupu zao walizo fichiwa, na
akasema: Mola Mlezi wenu hakukukatazeni mti huu ila msije mkawa Malaika, au
msije mkawa katika wanao ishi milele.
|
Ayah 7:21 الأية
وَقَاسَمَهُمَا إِنِّي لَكُمَا لَمِنَ النَّاصِحِينَ
Waqasamahuma innee lakumalamina annasiheen
Swahili
Naye akawaapia: Kwa yakini mimi ni miongoni wa wanao kunasihini.
|
Ayah 7:22 الأية
فَدَلَّاهُمَا بِغُرُورٍ ۚ فَلَمَّا ذَاقَا الشَّجَرَةَ بَدَتْ لَهُمَا
سَوْآتُهُمَا وَطَفِقَا يَخْصِفَانِ عَلَيْهِمَا مِن وَرَقِ الْجَنَّةِ ۖ
وَنَادَاهُمَا رَبُّهُمَا أَلَمْ أَنْهَكُمَا عَن تِلْكُمَا الشَّجَرَةِ وَأَقُل
لَّكُمَا إِنَّ الشَّيْطَانَ لَكُمَا عَدُوٌّ مُّبِينٌ
Fadallahuma bighuroorin falammathaqa ashshajarata badat lahuma
saw-atuhumawatafiqa yakhsifani AAalayhimamin waraqi aljannati wanadahuma
rabbuhumaalam anhakuma AAan tilkuma ashshajaratiwaaqul lakuma inna ashshaytana
lakumaAAaduwwun mubeen
Swahili
Basi akawateka kwa khadaa. Walipo uonja ule mti, tupu zao zilifichuka na
wakaingia kujibandika majani ya Bustanini. Mola wao Mlezi akawaita: Je,
sikukukatazeni mti huo, na kukwambieni ya kwamba Shet'ani ni adui yenu wa
dhaahiri?
|
Ayah 7:23 الأية
قَالَا رَبَّنَا ظَلَمْنَا أَنفُسَنَا وَإِن لَّمْ تَغْفِرْ لَنَا وَتَرْحَمْنَا
لَنَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ
Qala rabbana thalamnaanfusana wa-in lam taghfir lana watarhamnalanakoonanna mina
alkhasireen
Swahili
Wakasema: Mola wetu Mlezi! tumejidhulumu nafsi zetu, na kama hutusamehe na
kuturehemu, hakika tutakuwa katika wenye kukhasirika.
|
Ayah 7:24 الأية
قَالَ اهْبِطُوا بَعْضُكُمْ لِبَعْضٍ عَدُوٌّ ۖ وَلَكُمْ فِي الْأَرْضِ مُسْتَقَرٌّ
وَمَتَاعٌ إِلَىٰ حِينٍ
Qala ihbitoo baAAdukumlibaAAdin AAaduwwun walakum fee al-ardi
mustaqarrunwamataAAun ila heen
Swahili
Akasema: Teremkeni! Mtakuwa nyinyi kwa nyinyi maadui. Na kwenye ardhi itakuwa
ndio makao yenu na starehe yenu mpaka ufike muda.
|
Ayah 7:25 الأية
قَالَ فِيهَا تَحْيَوْنَ وَفِيهَا تَمُوتُونَ وَمِنْهَا تُخْرَجُونَ
Qala feeha tahyawnawafeeha tamootoona waminha tukhrajoon
Swahili
Akasema: Humo mtaishi, na humo mtakufa, na kutoka humo mtatolewa.
|
Ayah 7:26 الأية
يَا بَنِي آدَمَ قَدْ أَنزَلْنَا عَلَيْكُمْ لِبَاسًا يُوَارِي سَوْآتِكُمْ
وَرِيشًا ۖ وَلِبَاسُ التَّقْوَىٰ ذَٰلِكَ خَيْرٌ ۚ ذَٰلِكَ مِنْ آيَاتِ اللهِ
لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ
Ya banee adama qad anzalnaAAalaykum libasan yuwaree saw-atikumwareeshan walibasu
attaqwa thalikakhayrun thalika min ayati AllahilaAAallahum yaththakkaroon
Swahili
Enyi wanaadamu! Tumekuteremshieni nguo za kuficha tupu zenu, na nguo za pambo.
Na nguo za uchamngu ndio bora. Hayo ni katika Ishara za Mwenyezi Mungu mpate
kukumbuka.
|
Ayah 7:27 الأية
يَا بَنِي آدَمَ لَا يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم
مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْآتِهِمَا ۗ
إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لَا تَرَوْنَهُمْ ۗ إِنَّا
جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ لِلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ
Ya banee adama layaftinannakumu ashshaytanu kama akhrajaabawaykum mina aljannati
yanziAAu AAanhuma libasahumaliyuriyahuma saw-atihima innahu yarakumhuwa
waqabeeluhu min haythu la tarawnahum innajaAAalna ashshayateena awliyaa
lillatheenala yu/minoon
Swahili
Eny wanaadamu! Asije Shet'ani kukufitinini kama alivyo watoa wazazi wenu Peponi,
akawavua nguo zao kuwaonyesha tupu zao. Hakika yeye na kabila yake wanakuoneni,
na nyinyi hamuwaoni. Hakika Sisi tumewafanya Mashet'ani kuwa ni marafiki wa
wasio amini.
|
Ayah 7:28 الأية
وَإِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً قَالُوا وَجَدْنَا عَلَيْهَا آبَاءَنَا وَاللهُ
أَمَرَنَا بِهَا ۗ قُلْ إِنَّ اللهَ لَا يَأْمُرُ بِالْفَحْشَاءِ ۖ أَتَقُولُونَ
عَلَى اللهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Wa-itha faAAaloo fahishatan qaloowajadna AAalayha abaana wallahuamarana biha qul
inna Allaha laya/muru bilfahsha-i ataqooloona AAalaAllahi ma la taAAlamoon
Swahili
Na wanapo fanya mambo machafu husema: Tumewakuta nayo baba zetu, na Mwenyezi
Mungu ametuamrisha hayo. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu haamrishi mambo machafu.
Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua?
|
Ayah 7:29 الأية
قُلْ أَمَرَ رَبِّي بِالْقِسْطِ ۖ وَأَقِيمُوا وُجُوهَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ
وَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۚ كَمَا بَدَأَكُمْ تَعُودُونَ
Qul amara rabbee bilqistiwaaqeemoo wujoohakum AAinda kulli masjidin
wadAAoohumukhliseena lahu addeena kama badaakumtaAAoodoon
Swahili
Sema: Mola Mlezi wangu ameamrisha uadilifu, na mumuelekeze nyuso zenu kila mnapo
sujudu, na muombeni Yeye kwa kumsafia Dini. Kama alivyo kuumbeni mwanzo ndivyo
mtavyo rudi,
|
Ayah 7:30 الأية
فَرِيقًا هَدَىٰ وَفَرِيقًا حَقَّ عَلَيْهِمُ الضَّلَالَةُ ۗ إِنَّهُمُ اتَّخَذُوا
الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ اللهِ وَيَحْسَبُونَ أَنَّهُم مُّهْتَدُونَ
Fareeqan hada wafareeqan haqqaAAalayhimu addalalatu innahumu
ittakhathooashshayateena awliyaa min dooni Allahiwayahsaboona annahum muhtadoon
Swahili
Hali ya kuwa kundi moja amelihidi, na kundi jengine limethibitikiwa na upotofu.
Kwa hakika hao waliwafanya mashet'ani kuwa ndio marafiki walinzi badala ya
Mwenyezi Mungu, na wanadhani kuwa wao wameongoka.
|
Ayah 7:31 الأية
يَا بَنِي آدَمَ خُذُوا زِينَتَكُمْ عِندَ كُلِّ مَسْجِدٍ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا
وَلَا تُسْرِفُوا ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُسْرِفِينَ
Ya banee adama khuthoozeenatakum AAinda kulli masjidin wakuloo washraboo
walatusrifoo innahu la yuhibbu almusrifeen
Swahili
Enyi wanaadamu! Chukueni pambo lenu kwenye kila pahala wakati wa ibada, na
kuleni, na kunyweni na wala msifanye ubadhirifu. Kwa hakika Yeye hapendi wanao
fanya israfu.
|
Ayah 7:32 الأية
قُلْ مَنْ حَرَّمَ زِينَةَ اللهِ الَّتِي أَخْرَجَ لِعِبَادِهِ وَالطَّيِّبَاتِ
مِنَ الرِّزْقِ ۚ قُلْ هِيَ لِلَّذِينَ آمَنُوا فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا
خَالِصَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ
يَعْلَمُونَ
Qul man harrama zeenata Allahiallatee akhraja liAAibadihi wattayyibatimina
arrizqi qul hiya lillatheena amanoofee alhayati addunya khalisatanyawma
alqiyamati kathalika nufassilu al-ayatiliqawmin yaAAlamoon
Swahili
Sema: Ni nani aliye harimisha pambo la Mwenyezi Mungu alilo watolea waja wake,
na vilivyo vizuri katika riziki. Sema hivyo ni kwa walio amini katika uhai wa
duniani, na Siku ya Kiyama vitakuwa vyao wao tu. Namna hivi tunazieleza Ishara
kwa watu wanao jua.
|
Ayah 7:33 الأية
قُلْ إِنَّمَا حَرَّمَ رَبِّيَ الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ
وَالْإِثْمَ وَالْبَغْيَ بِغَيْرِ الْحَقِّ وَأَن تُشْرِكُوا بِاللهِ مَا لَمْ
يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا وَأَن تَقُولُوا عَلَى اللهِ مَا لَا تَعْلَمُونَ
Qul innama harrama rabbiyaalfawahisha ma thahara minhawama batana wal-ithma
walbaghyabighayri alhaqqi waan tushrikoo billahi malam yunazzil bihi sultanan
waan taqooloo AAala Allahima la taAAlamoon
Swahili
Sema: Mola Mlezi wangu ameharimisha mambo machafu ya dhaahiri na ya siri, na
dhambi, na uasi bila ya haki, na kumshirikisha Mwenyezi Mungu na asicho kiletea
uthibitisho, na kumzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua.
|
Ayah 7:34 الأية
وَلِكُلِّ أُمَّةٍ أَجَلٌ ۖ فَإِذَا جَاءَ أَجَلُهُمْ لَا يَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً
ۖ وَلَا يَسْتَقْدِمُونَ
Walikulli ommatin ajalun fa-itha jaaajaluhum la yasta/khiroona saAAatan
walayastaqdimoon
Swahili
Na kila umma una muda wake. Utakapo fika muda wao basi hawatakawia hata saa
moja, wala hawatatangulia.
|
Ayah 7:35 الأية
يَا بَنِي آدَمَ إِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ رُسُلٌ مِّنكُمْ يَقُصُّونَ عَلَيْكُمْ
آيَاتِي ۙ فَمَنِ اتَّقَىٰ وَأَصْلَحَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ
يَحْزَنُونَ
Ya banee adama immaya/tiyannakum rusulun minkum yaqussoona AAalaykum
ayateefamani ittaqa waaslaha fala khawfunAAalayhim wala hum yahzanoon
Swahili
Enyi wanaadamu! Watakapo kufikieni Mitume miongoni mwenu wakakuelezeni Ishara
zangu, basi watakao mchamngu na wakatengenea haitakuwa khofu kwao, wala
hawatahuzunika.
|
Ayah 7:36 الأية
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ
النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Wallatheena kaththaboobi-ayatina wastakbaroo AAanhaola-ika as-habu annari
humfeeha khalidoon
Swahili
Na wale watakao kanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi, hao ni watu wa
Motoni; humo watadumu.
|
Ayah 7:37 الأية
فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ
ۚ أُولَٰئِكَ يَنَالُهُمْ نَصِيبُهُم مِّنَ الْكِتَابِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا جَاءَتْهُمْ
رُسُلُنَا يَتَوَفَّوْنَهُمْ قَالُوا أَيْنَ مَا كُنتُمْ تَدْعُونَ مِن دُونِ
اللهِ ۖ قَالُوا ضَلُّوا عَنَّا وَشَهِدُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ أَنَّهُمْ كَانُوا
كَافِرِينَ
Faman athlamu mimmani iftaraAAala Allahi kathiban aw kaththababi-ayatihi ola-ika
yanaluhum naseebuhummina alkitabi hatta itha jaat-humrusuluna yatawaffawnahum
qaloo ayna makuntum tadAAoona min dooni Allahi qaloo dallooAAanna washahidoo
AAala anfusihim annahum kanookafireen
Swahili
Basi ni nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, au
anaye zikanusha Ishara zake? Hao itawafikia sehemu yao waliyo andikiwa, mpaka
watakapo wafikia wajumbe wetu kuwafisha, watawaambia: Wako wapi mlio kuwa
mkiwaomba badala ya Mwenyezi Mungu? Watasema: Wametupotea! Na watajishuhudia
wenyewe kwamba walikuwa makafiri.
|
Ayah 7:38 الأية
قَالَ ادْخُلُوا فِي أُمَمٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُم مِّنَ الْجِنِّ وَالْإِنسِ
فِي النَّارِ ۖ كُلَّمَا دَخَلَتْ أُمَّةٌ لَّعَنَتْ أُخْتَهَا ۖ حَتَّىٰ إِذَا
ادَّارَكُوا فِيهَا جَمِيعًا قَالَتْ أُخْرَاهُمْ لِأُولَاهُمْ رَبَّنَا هَٰؤُلَاءِ
أَضَلُّونَا فَآتِهِمْ عَذَابًا ضِعْفًا مِّنَ النَّارِ ۖ قَالَ لِكُلٍّ ضِعْفٌ
وَلَٰكِن لَّا تَعْلَمُونَ
Qala odkhuloo fee omamin qad khalatmin qablikum mina aljinni wal-insi fee
annarikullama dakhalat ommatun laAAanat okhtaha hattaitha iddarakoo feeha
jameeAAan qalatokhrahum li-oolahum rabbana haola-iadalloona faatihim AAathaban
diAAfanmina annari qala likullin diAAfunwalakin la taAAlamoon
Swahili
Mwenyezi Mungu atasema: Ingieni Motoni pamoja na umma zilizo pita kabla yenu za
majini na watu. Kila utakapo ingia umma utawalaani wenzake. Mpaka watakapo
kusanyika wote humo, wa mwisho wao watawasema wa mwanzo wao: Mola wetu Mlezi!
Hawa ndio walio tupoteza; basi wape adhabu ya Motoni marudufu. Atasema: Itakuwa
kwenu nyote marudufu, lakini nyinyi hamjui tu.
|
Ayah 7:39 الأية
وَقَالَتْ أُولَاهُمْ لِأُخْرَاهُمْ فَمَا كَانَ لَكُمْ عَلَيْنَا مِن فَضْلٍ
فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْسِبُونَ
Waqalat oolahum li-okhrahumfama kana lakum AAalayna min fadlinfathooqoo
alAAathaba bima kuntum taksiboon
Swahili
Na wa mwanzo wao watawaambia wa mwisho wao: Basi nyinyi pia hamkuwa na ubora
kuliko sisi. Basi onjeni adhabu kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyachuma.
|
Ayah 7:40 الأية
إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ
لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ
الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي الْمُجْرِمِينَ
Inna allatheena kaththaboo bi-ayatinawastakbaroo AAanha la tufattahulahum abwabu
assama-i walayadkhuloona aljannata hatta yalija aljamalu feesammi alkhiyati
wakathalika najzee almujrimeen
Swahili
Hakika wale wanao zikanusha Ishara zetu na wakazifanyia kiburi hawatafunguliwa
milango ya mbingu, wala hawataingia Peponi mpaka apite ngamia katika tundu ya
sindano. Na hivi ndivyo tunavyo walipa wakosefu.
|
Ayah 7:41 الأية
لَهُم مِّن جَهَنَّمَ مِهَادٌ وَمِن فَوْقِهِمْ غَوَاشٍ ۚ وَكَذَٰلِكَ نَجْزِي
الظَّالِمِينَ
Lahum min jahannama mihadun waminfawqihim ghawashin wakathalika najzee
aththalimeen
Swahili
Jahannamu itakuwa kitanda chao na juu yao nguo za moto za kujifunika. Na hivi
ndivyo tunavyo walipa madhaalimu.
|
Ayah 7:42 الأية
وَالَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا
وُسْعَهَا أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Wallatheena amanoowaAAamiloo assalihati la nukallifunafsan illa wusAAaha ola-ika
as-habualjannati hum feeha khalidoon
Swahili
Na wale wanao amini na wakatenda mema - hatumkalifishi mtu yoyote ila kwa kiasi
cha uwezo wake - hao ndio watu wa Peponi. Wao watadumu humo.
|
Ayah 7:43 الأية
وَنَزَعْنَا مَا فِي صُدُورِهِم مِّنْ غِلٍّ تَجْرِي مِن تَحْتِهِمُ الْأَنْهَارُ ۖ
وَقَالُوا الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي هَدَانَا لِهَٰذَا وَمَا كُنَّا لِنَهْتَدِيَ
لَوْلَا أَنْ هَدَانَا اللهُ ۖ لَقَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ ۖ
وَنُودُوا أَن تِلْكُمُ الْجَنَّةُ أُورِثْتُمُوهَا بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
WanazaAAna ma fee sudoorihimmin ghillin tajree min tahtihimu al-anharu
waqalooalhamdu lillahi allathee hadanalihatha wama kunna linahtadiya lawlaan
hadana Allahu laqad jaat rusulurabbina bilhaqqi wanoodoo an tilkumualjannatu
oorithtumooha bima kuntum taAAmaloon
Swahili
Na tutaondoa chuki vifuani mwao, na mbele yao iwe inapita mito. Na watasema:
Alhamdulillah! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu, ambaye aliye tuhidi kufikia
haya. Wala hatukuwa wenye kuhidika wenyewe ingeli kuwa Mwenyezi Mungu
hakutuhidi. Hakika Mitume wa Mola wetu Mlezi walileta Haki. Na watanadiwa
kwamba: Hiyo ndiyo Pepo mliyo rithishwa kwa sababu ya mliyo kuwa mkiyafanya.
|
Ayah 7:44 الأية
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ أَصْحَابَ النَّارِ أَن قَدْ وَجَدْنَا مَا
وَعَدَنَا رَبُّنَا حَقًّا فَهَلْ وَجَدتُّم مَّا وَعَدَ رَبُّكُمْ حَقًّا ۖ
قَالُوا نَعَمْ ۚ فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللهِ عَلَى
الظَّالِمِينَ
Wanada as-habualjannati as-haba annari an qadwajadna ma waAAadana rabbuna
haqqanfahal wajadtum ma waAAada rabbukum haqqan qaloonaAAam faaththana
mu-aththinun baynahum an laAAnatuAllahi AAala aththalimeen
Swahili
Na watu wa Peponi watawanadia watu wa Motoni: Sisi tumekuta aliyo tuahidi Mola
wetu Mlezi kuwa ni kweli. Je, na nyinyi pia mmekuta aliyo kuahidini Mola wenu
Mlezi kuwa ni kweli? Watasema: Ndiyo! Basi mtangazaji atawatangazia: Laana ya
Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu,
|
Ayah 7:45 الأية
الَّذِينَ يَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللهِ وَيَبْغُونَهَا عِوَجًا وَهُم
بِالْآخِرَةِ كَافِرُونَ
Allatheena yasuddoona AAansabeeli Allahi wayabghoonaha AAiwajan wahum
bil-akhiratikafiroon
Swahili
Wale ambao walikuwa wakizuilia Njia ya Mwenyezi Mungu, na wakataka kuipotosha,
nao wanaikanusha Akhera.
|
Ayah 7:46 الأية
وَبَيْنَهُمَا حِجَابٌ ۚ وَعَلَى الْأَعْرَافِ رِجَالٌ يَعْرِفُونَ كُلًّا
بِسِيمَاهُمْ ۚ وَنَادَوْا أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَن سَلَامٌ عَلَيْكُمْ ۚ لَمْ
يَدْخُلُوهَا وَهُمْ يَطْمَعُونَ
Wabaynahuma hijabunwaAAala al-aAArafi rijalun yaAArifoonakullan biseemahum
wanadaw as-habaaljannati an salamun AAalaykum lam yadkhuloohawahum yatmaAAoon
Swahili
Na baina ya makundi mawili hayo patakuwapo pazia. Na juu ya Mnyanyuko patakuwa
watu watakao wajua wote kwa alama zao, na wao watawaita watu wa Peponi: Assalamu
Alaykum, Amani juu yenu! Wao bado hawajaingia humo, lakini wanatumai.
|
Ayah 7:47 الأية
وَإِذَا صُرِفَتْ أَبْصَارُهُمْ تِلْقَاءَ أَصْحَابِ النَّارِ قَالُوا رَبَّنَا لَا
تَجْعَلْنَا مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Wa-itha surifat absaruhumtilqaa as-habi annari qaloorabbana la tajAAalna maAAa
alqawmi aththalimeen
Swahili
Na yanapo geuzwa macho yao kuelekea watu wa Motoni, watasema: Mola Mlezi wetu!
Usitujaalie kuwa pamoja na watu walio dhulumu.
|
Ayah 7:48 الأية
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ الْأَعْرَافِ رِجَالًا يَعْرِفُونَهُم بِسِيمَاهُمْ قَالُوا
مَا أَغْنَىٰ عَنكُمْ جَمْعُكُمْ وَمَا كُنتُمْ تَسْتَكْبِرُونَ
Wanada as-habual-aAArafi rijalan yaAArifoonahum biseemahumqaloo ma aghna AAankum
jamAAukum wamakuntum tastakbiroon
Swahili
Na hao watu wa Mnyanyukoni watawaita watu wanao wajua kwa alama zao. Watasema:
Kujumuika kwenu hakukufaini kitu, wala hicho mlicho kuwa mnafanyia kiburi.
|
Ayah 7:49 الأية
أَهَٰؤُلَاءِ الَّذِينَ أَقْسَمْتُمْ لَا يَنَالُهُمُ اللهُ بِرَحْمَةٍ ۚ
ادْخُلُوا الْجَنَّةَ لَا خَوْفٌ عَلَيْكُمْ وَلَا أَنتُمْ تَحْزَنُونَ
Ahaola-i allatheenaaqsamtum la yanaluhumu Allahu birahmatinodkhuloo aljannata la
khawfun AAalaykum wala antumtahzanoon
Swahili
Je, hawa sio wale mlio kuwa mkiwaapia kuwa Mwenyezi Mungu hatawafikishia rehema.
Ingieni Peponi, hapana khofu kwenu, wala hamtahuzunika!
|
Ayah 7:50 الأية
وَنَادَىٰ أَصْحَابُ النَّارِ أَصْحَابَ الْجَنَّةِ أَنْ أَفِيضُوا عَلَيْنَا مِنَ
الْمَاءِ أَوْ مِمَّا رَزَقَكُمُ اللهُ ۚ قَالُوا إِنَّ اللهَ حَرَّمَهُمَا
عَلَى الْكَافِرِينَ
Wanada as-habu anarias-haba aljannati an afeedoo AAalaynamina alma-i aw mimma
razaqakumu Allahu qalooinna Allaha harramahuma AAala alkafireen
Swahili
Na watu wa Motoni watawaita watu wa Peponi: Tumimieni maji, au chochote alicho
kuruzukuni Mwenyezi Mungu. Nao watasema: Hakika Mwenyezi Mungu ameviharimisha
hivyo kwa makafiri,
|
Ayah 7:51 الأية
الَّذِينَ اتَّخَذُوا دِينَهُمْ لَهْوًا وَلَعِبًا وَغَرَّتْهُمُ الْحَيَاةُ
الدُّنْيَا ۚ فَالْيَوْمَ نَنسَاهُمْ كَمَا نَسُوا لِقَاءَ يَوْمِهِمْ هَٰذَا وَمَا
كَانُوا بِآيَاتِنَا يَجْحَدُونَ
Allatheena ittakhathoodeenahum lahwan walaAAiban wagharrat-humu alhayatuaddunya
falyawma nansahum kamanasoo liqaa yawmihim hatha wama kanoobi-ayatina yajhadoon
Swahili
Ambao waliifanya dini yao kuwa ni pumbao na mchezo, na maisha ya dunia
yakawadanganya. Basi leo Sisi tunawasahau kama walivyo usahau mkutano wa Siku
yao hii, na kwa sababu ya kule kuzikataa Ishara zetu.
|
Ayah 7:52 الأية
وَلَقَدْ جِئْنَاهُم بِكِتَابٍ فَصَّلْنَاهُ عَلَىٰ عِلْمٍ هُدًى وَرَحْمَةً
لِّقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Walaqad ji/nahum bikitabin fassalnahuAAala AAilmin hudan warahmatan liqawmin
yu/minoon
Swahili
Na hakika tumewaletea Kitabu tulicho kipambanua kwa ilimu, uwongofu na rehema
kwa watu wenye kuamini.
|
Ayah 7:53 الأية
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ ۚ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ
الَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَل
لَّنَا مِن شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي
كُنَّا نَعْمَلُ ۚ قَدْ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ وَضَلَّ عَنْهُم مَّا كَانُوا
يَفْتَرُونَ
Hal yanthuroona illata/weelahu yawma ya/tee ta/weeluhu yaqoolu allatheenanasoohu
min qablu qad jaat rusulu rabbina bilhaqqifahal lana min shufaAAaa fayashfaAAoo
lanaaw nuraddu fanaAAmala ghayra allathee kunnanaAAmalu qad khasiroo anfusahum
wadalla AAanhum makanoo yaftaroon
Swahili
Je, lipo wanalo lingojea isipo kuwa matokeo yake? Siku yatapo fika matokeo yake
watasema wale walio kisahau: Kweli Mitume wa Mola Mlezi wetu walileta Haki! Je,
tunao waombezi ili watuombee? Au turudishwe ili tufanye yasiyo kuwa yale tuliyo
kuwa tukiyafanya? Bila ya shaka wamejikhasiri nafsi zao, na yamewapotea waliyo
kuwa wakiyazua.
|
Ayah 7:54 الأية
إِنَّ رَبَّكُمُ اللهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ
أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ يُغْشِي اللَّيْلَ النَّهَارَ يَطْلُبُهُ
حَثِيثًا وَالشَّمْسَ وَالْقَمَرَ وَالنُّجُومَ مُسَخَّرَاتٍ بِأَمْرِهِ ۗ أَلَا
لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ ۗ تَبَارَكَ اللهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ
Inna rabbakumu Allahu allatheekhalaqa assamawati wal-ardafee sittati ayyamin
thumma istawa AAalaalAAarshi yughshee allayla annahara yatlubuhuhatheethan
washshamsa walqamara wannujoomamusakhkharatin bi-amrihi ala lahu alkhalqu
wal-amrutabaraka Allahu rabbu alAAalameen
Swahili
Hakika Mola Mlezi wenu ni Mwenyezi Mungu aliye ziumba mbingu na ardhi katika
siku sita. Kisha akatawala juu ya Kiti cha Enzi. Huufunika usiku kwa mchana,
ufuatao upesi upesi. Na jua, na mwezi, na nyota zinazo tumika kwa amri yake.
Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa
viumbe vyote.
|
Ayah 7:55 الأية
ادْعُوا رَبَّكُمْ تَضَرُّعًا وَخُفْيَةً ۚ إِنَّهُ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ
OdAAoo rabbakum tadarruAAanwakhufyatan innahu la yuhibbu almuAAtadeen
Swahili
Muombeni Mola wenu Mlezi kwa unyenyekevu na kwa siri. Hakika Yeye hawapendi
warukao mipaka.
|
Ayah 7:56 الأية
وَلَا تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا وَادْعُوهُ خَوْفًا وَطَمَعًا
ۚ إِنَّ رَحْمَتَ اللهِ قَرِيبٌ مِّنَ الْمُحْسِنِينَ
Wala tufsidoo fee al-ardibaAAda islahiha wadAAoohu khawfan watamaAAaninna
rahmata Allahi qareebun mina almuhsineen
Swahili
Wala msifanye uharibifu katika nchi baada ya kuwa imekwisha tengenezwa. Na
muombeni kwa kuogopa na kwa kutumai. Hakika rehema ya Mwenyzi Mungu iko karibu
na wanao fanya mema.
|
Ayah 7:57 الأية
وَهُوَ الَّذِي يُرْسِلُ الرِّيَاحَ بُشْرًا بَيْنَ يَدَيْ رَحْمَتِهِ ۖ حَتَّىٰ
إِذَا أَقَلَّتْ سَحَابًا ثِقَالًا سُقْنَاهُ لِبَلَدٍ مَّيِّتٍ فَأَنزَلْنَا بِهِ
الْمَاءَ فَأَخْرَجْنَا بِهِ مِن كُلِّ الثَّمَرَاتِ ۚ كَذَٰلِكَ نُخْرِجُ
الْمَوْتَىٰ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Wahuwa allathee yursilu arriyahabushran bayna yaday rahmatihi hatta ithaaqallat
sahaban thiqalan suqnahu libaladinmayyitin faanzalna bihi almaa faakhrajnabihi
min kulli aththamarati kathalikanukhriju almawta laAAallakum tathakkaroon
Swahili
Na Yeye ndiye anaye peleka pepo (za kuvuma) kuwa ni bishara kabla ya kufika
rehema yake. Hata hizo pepo zinapo beba mawingu mazito tunayachunga mpaka kwenye
nchi iliyo kufa. Kisha tunateremsha kwayo maji, ndio kama hivyo tukatolesha kila
aina ya matunda. Basi hali kadhaalika tunavyo wafufua wafu, ili mpate kukumbuka.
|
Ayah 7:58 الأية
وَالْبَلَدُ الطَّيِّبُ يَخْرُجُ نَبَاتُهُ بِإِذْنِ رَبِّهِ ۖ وَالَّذِي خَبُثَ
لَا يَخْرُجُ إِلَّا نَكِدًا ۚ كَذَٰلِكَ نُصَرِّفُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَشْكُرُونَ
Walbaladu attayyibuyakhruju nabatuhu bi-ithni rabbihi wallatheekhabutha la
yakhruju illa nakidan kathalikanusarrifu al-ayati liqawmin yashkuroon
Swahili
Na ardhi njema, yenye udongo wa rutba, hutoa mimea yenye kukua vizuri yenye
uhai, kwa idhini ya Mola Mlezi wake. Na ardhi mbaya haitoi ila mimea michache,
isiyo na faida, tena kwa shida. Na hivyo ndivyo tunavyo zipambanua Ishara (Aya)
kwa watu wanao shukuru.
|
Ayah 7:59 الأية
لَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ
مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ إِنِّي أَخَافُ عَلَيْكُمْ عَذَابَ يَوْمٍ
عَظِيمٍ
Laqad arsalna noohan ilaqawmihi faqala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min
ilahin ghayruhu innee akhafu AAalaykumAAathaba yawmin AAatheem
Swahili
Tulimpeleka Nuhu kwa kaumu yake, naye akasema: Enyi kaumu yangu! Muabuduni
Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu
ya Siku iliyo kuu.
|
Ayah 7:60 الأية
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Qala almalao min qawmihi innalanaraka fee dalalin mubeen
Swahili
Wale watukufu katika kaumu yake wakasema: Hakika sisi tunakuona wewe umo katika
upotofu ulio dhaahiri.
|
Ayah 7:61 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي ضَلَالَةٌ وَلَٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ
الْعَالَمِينَ
Qala ya qawmi laysa bee dalalatunwalakinnee rasoolun min rabbi alAAalameen
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Mimi simo katika upotofu, lakini mimi ni Mtume
nitokaye kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
|
Ayah 7:62 الأية
أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنصَحُ لَكُمْ وَأَعْلَمُ مِنَ اللهِ مَا لَا
تَعْلَمُونَ
Oballighukum risalati rabbeewaansahu lakum waaAAlamu mina Allahi mala taAAlamoon
Swahili
Nakufikishieni Ujumbe wa Mola Mlezi wangu, na ninakunasihini; na ninayajua kwa
Mwenyezi Mungu msiyo yajua nyinyi.
|
Ayah 7:63 الأية
أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ
لِيُنذِرَكُمْ وَلِتَتَّقُوا وَلَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ
Awa AAajibtum an jaakum thikrunmin rabbikum AAala rajulin minkum
liyunthirakumwalitattaqoo walaAAallakum turhamoon
Swahili
Je, mnastaajabu kukujieni mawaidha yanayotoka kwa Mola Mlezi wenu kwa njia ya
mtu aliye ni mmoja katika nyinyi, ili akuonyeni na ili mumchemngu, na ili mpate
kurehemewa?
|
Ayah 7:64 الأية
فَكَذَّبُوهُ فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ فِي الْفُلْكِ وَأَغْرَقْنَا
الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا عَمِينَ
Fakaththaboohu faanjaynahu wallatheenamaAAahu fee alfulki waaghraqna allatheena
kaththaboobi-ayatina innahum kanoo qawmanAAameen
Swahili
Basi walimkanusha. Nasi tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye katika jahazi.
Na tukawazamisha wale walio kanusha Ishara zetu. Hakika hao walikuwa watu
vipofu.
|
Ayah 7:65 الأية
وَإِلَىٰ عَادٍ أَخَاهُمْ هُودًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ مَا لَكُم
مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۚ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Wa-ila AAadin akhahumhoodan qala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min ilahin
ghayruhu afala tattaqoon
Swahili
Na kwa A'adi tulimpeleka ndugu yao, Hud. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni
Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu ila Yeye. Basi je, hamumchi?
|
Ayah 7:66 الأية
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ إِنَّا لَنَرَاكَ فِي سَفَاهَةٍ
وَإِنَّا لَنَظُنُّكَ مِنَ الْكَاذِبِينَ
Qala almalao allatheenakafaroo min qawmihi inna lanaraka fee safahatinwa-inna
lanathunnuka mina alkathibeen
Swahili
Wakasema watukufu wa wale walio kufuru katika kaumu yake: Sisi tunakuona umo
katika upumbavu, na hakika sisi tunakufikiria kuwa wewe ni katika waongo.
|
Ayah 7:67 الأية
قَالَ يَا قَوْمِ لَيْسَ بِي سَفَاهَةٌ وَلَٰكِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ
الْعَالَمِينَ
Qala ya qawmi laysa bee safahatunwalakinnee rasoolun min rabbi alAAalameen
Swahili
Akasema: Enyi watu wangu! Mimi sina upumbavu. Lakini mimi ni Mtume niliye toka
kwa Mola Mlezi wa viumbe vyote.
|
Ayah 7:68 الأية
أُبَلِّغُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي وَأَنَا لَكُمْ نَاصِحٌ أَمِينٌ
Oballighukum risalati rabbeewaana lakum nasihun ameen
Swahili
Nakufikishieni ujumbe wa Mola wangu Mlezi. Na mimi kwenu ni mwenye kukunasihini,
muaminifu.
|
Ayah 7:69 الأية
أَوَعَجِبْتُمْ أَن جَاءَكُمْ ذِكْرٌ مِّن رَّبِّكُمْ عَلَىٰ رَجُلٍ مِّنكُمْ
لِيُنذِرَكُمْ ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ قَوْمِ نُوحٍ
وَزَادَكُمْ فِي الْخَلْقِ بَسْطَةً ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللهِ لَعَلَّكُمْ
تُفْلِحُونَ
Awa AAajibtum an jaakum thikrunmin rabbikum AAala rajulin minkum liyunthirakum
wathkurooith jaAAalakum khulafaa min baAAdi qawmi noohinwazadakum fee alkhalqi
bastatan fathkurooalaa Allahi laAAallakum tuflihoon
Swahili
Mnaona ajabu kukufikieni mawaidha yanayo toka kwa Mola wenu Mlezi kwa mtu aliye
mmoja wenu nyinyi ili akuonyeni? Na kumbukeni alivyo kufanyeni mshike pahala pa
kaumu ya Nuhu, na akakuzidisheni katika umbo. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi
Mungu ili mpate kufanikiwa.
|
Ayah 7:70 الأية
قَالُوا أَجِئْتَنَا لِنَعْبُدَ اللهَ وَحْدَهُ وَنَذَرَ مَا كَانَ يَعْبُدُ
آبَاؤُنَا ۖ فَأْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
Qaloo aji/tana linaAAbuda Allahawahdahu wanathara ma kana yaAAbudu abaonafa/tina
bima taAAiduna in kunta mina assadiqeen
Swahili
Wakasema: Je! Umetujia ili tumuabudu Mwenyezi Mungu peke yake, na tuyaache
waliyo kuwa wakiyaabudu baba zetu? Basi tuletee hayo unayo tuahidi, ukiwa
miongoni mwa wasemao kweli.
|
Ayah 7:71 الأية
قَالَ قَدْ وَقَعَ عَلَيْكُم مِّن رَّبِّكُمْ رِجْسٌ وَغَضَبٌ ۖ أَتُجَادِلُونَنِي
فِي أَسْمَاءٍ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا نَزَّلَ اللهُ بِهَا مِن
سُلْطَانٍ ۚ فَانتَظِرُوا إِنِّي مَعَكُم مِّنَ الْمُنتَظِرِينَ
Qala qad waqaAAa AAalaykum minrabbikum rijsun waghadabun atujadiloonanee fee
asma-insammaytumooha antum waabaokum manazzala Allahu biha min sultanin
fantathirooinnee maAAakum mina almuntathireen
Swahili
Akasema: Bila ya shaka adhabu na ghadhabu zimekwisha kukuangukieni kutoka kwa
Mola wenu Mlezi. Mnabishana nami kwa ajili ya majina tu mliyo yaita nyinyi na
baba zenu ambayo kwayo Mwenyezi Mungu hakuteremsha uthibitisho? Basi ngojeni,
mimi pia ni pamoja nanyi katika wanao ngoja.
|
Ayah 7:72 الأية
فَأَنجَيْنَاهُ وَالَّذِينَ مَعَهُ بِرَحْمَةٍ مِّنَّا وَقَطَعْنَا دَابِرَ
الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا ۖ وَمَا كَانُوا مُؤْمِنِينَ
Faanjaynahu wallatheenamaAAahu birahmatin minna waqataAAna dabiraallatheena
kaththaboo bi-ayatinawama kanoo mu/mineen
Swahili
Basi tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye kwa rehema zetu, na tukakata
mizizi ya wale walio zikanusha Ishara zetu, na hawakuwa wenye kuamini.
|
Ayah 7:73 الأية
وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمْ صَالِحًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ مَا
لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ
هَٰذِهِ نَاقَةُ اللهِ لَكُمْ آيَةً ۖ فَذَرُوهَا تَأْكُلْ فِي أَرْضِ اللهِ ۖ
وَلَا تَمَسُّوهَا بِسُوءٍ فَيَأْخُذَكُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Wa-ila thamooda akhahum salihanqala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min ilahin
ghayruhu qad jaatkum bayyinatunmin rabbikum hathihi naqatu Allahi lakum
ayatanfatharooha ta/kul fee ardi Allahi walatamassooha bisoo-in faya/khuthakum
AAathabunaleem
Swahili
Na kwa Thamud tulimpeleka ndugu yao, Saleh. Akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni
Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye. Hakika imekwisha kukufikieni Ishara
iliyo wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Huyu ni ngamia jike wa Mwenyezi Mungu
aliye ni Ishara kwenu. Basi mwachieni ale kwenye ardhi ya Mwenyezi Mungu, wala
msimdhuru, isije kukushukieni adhabu chungu.
|
Ayah 7:74 الأية
وَاذْكُرُوا إِذْ جَعَلَكُمْ خُلَفَاءَ مِن بَعْدِ عَادٍ وَبَوَّأَكُمْ فِي
الْأَرْضِ تَتَّخِذُونَ مِن سُهُولِهَا قُصُورًا وَتَنْحِتُونَ الْجِبَالَ بُيُوتًا
ۖ فَاذْكُرُوا آلَاءَ اللهِ وَلَا تَعْثَوْا فِي الْأَرْضِ مُفْسِدِينَ
Wathkuroo ithjaAAalakum khulafaa min baAAdi AAadin wabawwaakumfee al-ardi
tattakhithoona min suhooliha qusooranwatanhitoona aljibala buyootan
fathkurooalaa Allahi wala taAAthaw fee al-ardimufsideen
Swahili
Na kumbukeni alivyo kufanyeni wa kushika pahala pa A'adi na akakuwekeni vizuri
katika nchi, mnajenga majumba ya fakhari katika nyanda zake, na mnachonga
majumba katika milima. Basi zikumbukeni neema za Mwenyezi Mungu wala msitende
uovu katika nchi kwa ufisadi.
|
Ayah 7:75 الأية
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لِلَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا
لِمَنْ آمَنَ مِنْهُمْ أَتَعْلَمُونَ أَنَّ صَالِحًا مُّرْسَلٌ مِّن رَّبِّهِ ۚ
قَالُوا إِنَّا بِمَا أُرْسِلَ بِهِ مُؤْمِنُونَ
Qala almalao allatheenaistakbaroo min qawmihi lillatheena istudAAifooliman amana
minhum ataAAlamoona anna salihanmursalun min rabbihi qaloo inna bima orsilabihi
mu/minoon
Swahili
Waheshimiwa wa kaumu yake wanao jivuna waliwaambia wanao onewa wenye kuamini
miongoni mwao: Je, mnaitakidi ya kwamba Saleh ametumwa na Mola Mlezi wake?
Wakasema: Hakika sisi tunayaamini yale aliyo tumwa.
|
Ayah 7:76 الأية
قَالَ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا إِنَّا بِالَّذِي آمَنتُم بِهِ كَافِرُونَ
Qala allatheena istakbaroo innabillathee amantum bihi kafiroon
Swahili
Wakasema wale wanao jivuna: Sisi tunayakataa hayo mnayo yaamini.
|
Ayah 7:77 الأية
فَعَقَرُوا النَّاقَةَ وَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ وَقَالُوا يَا صَالِحُ
ائْتِنَا بِمَا تَعِدُنَا إِن كُنتَ مِنَ الْمُرْسَلِينَ
FaAAaqaroo annaqata waAAatawAAan amri rabbihim waqaloo ya salihui/tina bima
taAAiduna in kunta minaalmursaleen
Swahili
Na wakamuuwa yule ngamia, na wakaasi amri ya Mola Mlezi wao, na wakasema: Ewe
Saleh! Tuletee unayo tuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.
|
Ayah 7:78 الأية
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ
Faakhathat-humu arrajfatu faasbahoofee darihim jathimeen
Swahili
Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na kulipo kucha wakawa majumbani mwao
kifudifudi wamekwisha kufa.
|
Ayah 7:79 الأية
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَةَ رَبِّي
وَنَصَحْتُ لَكُمْ وَلَٰكِن لَّا تُحِبُّونَ النَّاصِحِينَ
Fatawalla AAanhum waqala yaqawmi laqad ablaghtukum risalata rabbee
wanasahtulakum walakin la tuhibboona annasiheen
Swahili
Basi Saleh akwaacha na akasema: Enyi watu wangu! Nilikufikishieni Ujumbe wa Mola
wangu Mlezi, na nikakunasihini, lakini nyinyi hamwapendi wenye nasaha.
|
Ayah 7:80 الأية
وَلُوطًا إِذْ قَالَ لِقَوْمِهِ أَتَأْتُونَ الْفَاحِشَةَ مَا سَبَقَكُم بِهَا مِنْ
أَحَدٍ مِّنَ الْعَالَمِينَ
Walootan ith qalaliqawmihi ata/toona alfahishata ma sabaqakum bihamin ahadin
mina alAAalameen
Swahili
Na tulimtuma Lut', alipo waambia watu wake: Je, mnafanya uchafu ambao
hajakutangulieni yeyote kwa uchafu huo katika viumbe vyote!
|
Ayah 7:81 الأية
إِنَّكُمْ لَتَأْتُونَ الرِّجَالَ شَهْوَةً مِّن دُونِ النِّسَاءِ ۚ بَلْ أَنتُمْ
قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ
Innakum lata/toona arrijalashahwatan min dooni annisa-i bal antum
qawmunmusrifoon
Swahili
Hivyo nyinyi mnawaingilia wanaume kwa matamanio mkwawacha wanawake? Kumbe nyinyi
ni watu wafujaji!
|
Ayah 7:82 الأية
وَمَا كَانَ جَوَابَ قَوْمِهِ إِلَّا أَن قَالُوا أَخْرِجُوهُم مِّن قَرْيَتِكُمْ ۖ
إِنَّهُمْ أُنَاسٌ يَتَطَهَّرُونَ
Wama kana jawabaqawmihi illa an qaloo akhrijoohum min qaryatikuminnahum onasun
yatatahharoon
Swahili
Na haikuwa jawabu ya kaumu yake isipo kuwa kuambizana: Wafukuzeni katika mji
wenu, maana hao ni watu wanao jitakasa.
|
Ayah 7:83 الأية
فَأَنجَيْنَاهُ وَأَهْلَهُ إِلَّا امْرَأَتَهُ كَانَتْ مِنَ الْغَابِرِينَ
Faanjaynahu waahlahu illaimraatahu kanat mina alghabireen
Swahili
Basi tukamwokoa yeye na watu wake, isipo kuwa mkewe, alikuwa miongoni mwa walio
bakia nyuma.
|
Ayah 7:84 الأية
وَأَمْطَرْنَا عَلَيْهِم مَّطَرًا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ
الْمُجْرِمِينَ
Waamtarna AAalayhim mataranfanthur kayfa kana AAaqibatualmujrimeen
Swahili
Na tukawamiminia mvua. Basi tazama jinsi ulivyo kuwa mwisho wa wakosefu.
|
Ayah 7:85 الأية
وَإِلَىٰ مَدْيَنَ أَخَاهُمْ شُعَيْبًا ۗ قَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ مَا
لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ قَدْ جَاءَتْكُم بَيِّنَةٌ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ
فَأَوْفُوا الْكَيْلَ وَالْمِيزَانَ وَلَا تَبْخَسُوا النَّاسَ أَشْيَاءَهُمْ وَلَا
تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ بَعْدَ إِصْلَاحِهَا ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن
كُنتُم مُّؤْمِنِينَ
Wa-ila madyana akhahumshuAAayban qala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min
ilahin ghayruhu qad jaatkum bayyinatunmin rabbikum faawfoo alkayla walmeezana
walatabkhasoo annasa ashyaahum walatufsidoo fee al-ardi baAAda islahiha
thalikumkhayrun lakum in kuntum mu/mineen
Swahili
Na kwa watu wa Madyana tulimtuma ndugu yao Shua'ib. Akasema: Enyi watu wangu!
Muabuduni Mwenyezi Mungu. Hamna mungu mwengine isipo kuwa Yeye. Imekwisha
kufikieni hoja wazi kutoka kwa Mola Mlezi wenu. Basi timizeni sawasawa vipimo na
mizani, wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye uharibifu katika nchi,
baada ya kuwa imekwisha tengenea. Hivi ndivyo bora kwenu ikiwa nyinyi ni
Waumini.
|
Ayah 7:86 الأية
وَلَا تَقْعُدُوا بِكُلِّ صِرَاطٍ تُوعِدُونَ وَتَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللهِ
مَنْ آمَنَ بِهِ وَتَبْغُونَهَا عِوَجًا ۚ وَاذْكُرُوا إِذْ كُنتُمْ قَلِيلًا
فَكَثَّرَكُمْ ۖ وَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ
Wala taqAAudoo bikulli siratintooAAidoona watasuddoona AAan sabeeli Allahi man
amanabihi watabghoonaha AAiwajan wathkuroo ithkuntum qaleelan fakaththarakum
wanthurookayfa kana AAaqibatu almufsideen
Swahili
Wala msikae katika kila njia mkitisha watu, na kuwazuilia na Njia ya Mwenyezi
Mungu wale wenye kumuamini, na mkataka njia ipotoke. Na kumbukeni mlipo kuwa
wachache, naye akakufanyeni kuwa wengi. Na tazameni jinsi ulivyo kuwa mwisho wa
mafisadi.
|
Ayah 7:87 الأية
وَإِن كَانَ طَائِفَةٌ مِّنكُمْ آمَنُوا بِالَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ وَطَائِفَةٌ
لَّمْ يُؤْمِنُوا فَاصْبِرُوا حَتَّىٰ يَحْكُمَ اللهُ بَيْنَنَا ۚ وَهُوَ خَيْرُ
الْحَاكِمِينَ
Wa-in kana ta-ifatun minkum amanoobillathee orsiltu bihi wata-ifatun lamyu/minoo
fasbiroo hatta yahkumaAllahu baynana wahuwa khayru alhakimeen
Swahili
Na kama liko kundi miongoni mwenu lililo amini haya niliyo tumwa, na kundi
jengine halikuamini, basi subirini mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu baina yetu. Naye
ndiye Mbora wa wenye kuhukumu.
|
Ayah 7:88 الأية
قَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ اسْتَكْبَرُوا مِن قَوْمِهِ لَنُخْرِجَنَّكَ يَا
شُعَيْبُ وَالَّذِينَ آمَنُوا مَعَكَ مِن قَرْيَتِنَا أَوْ لَتَعُودُنَّ فِي
مِلَّتِنَا ۚ قَالَ أَوَلَوْ كُنَّا كَارِهِينَ
Qala almalao allatheenaistakbaroo min qawmihi lanukhrijannaka ya shuAAaybu
wallatheenaamanoo maAAaka min qaryatina aw lataAAoodunna feemillatina qala awa
law kunna kariheen
Swahili
WAHESHIMIWA WALIO TAKABARI katika kaumu yake wakasema: Ewe Shua'ib! Tutakutoa
wewe pamoja na wale walio kuamini katika mji wetu, au mrejee katika mila yetu.
Akasema: Je, ingawa tunaichukia?
|
Ayah 7:89 الأية
قَدِ افْتَرَيْنَا عَلَى اللهِ كَذِبًا إِنْ عُدْنَا فِي مِلَّتِكُم بَعْدَ إِذْ
نَجَّانَا اللهُ مِنْهَا ۚ وَمَا يَكُونُ لَنَا أَن نَّعُودَ فِيهَا إِلَّا أَن
يَشَاءَ اللهُ رَبُّنَا ۚ وَسِعَ رَبُّنَا كُلَّ شَيْءٍ عِلْمًا ۚ عَلَى اللهِ
تَوَكَّلْنَا ۚ رَبَّنَا افْتَحْ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمِنَا بِالْحَقِّ وَأَنتَ
خَيْرُ الْفَاتِحِينَ
Qadi iftarayna AAala Allahikathiban in AAudna fee millatikum baAAda ithnajjana
Allahu minha wamayakoonu lana an naAAooda feeha illa an yashaaAllahu rabbuna
wasiAAa rabbuna kulla shay-inAAilman AAala Allahi tawakkalna rabbanaiftah
baynana wabayna qawmina bilhaqqiwaanta khayru alfatiheen
Swahili
Bila ya shaka itakuwa tumemzulia uwongo Mwenyezi Mungu tukirudi katika mila yenu
baada ya kwisha tuokoa nayo Mwenyezi Mungu. Wala haiwi kwetu sisi kuirejea mila
hiyo, ila akitaka Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu. Ujuzi wa Mola Mlezi wetu
umeenea katika kila kitu. Kwa Mwenyezi Mungu tunategemea. Ewe Mola Mlezi wetu!
Tuhukumie baina yetu na kaumu yetu kwa haki, nawe ndiye mbora wa wanao hukumu.
|
Ayah 7:90 الأية
وَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ لَئِنِ اتَّبَعْتُمْ شُعَيْبًا
إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ
Waqala almalao allatheenakafaroo min qawmihi la-ini ittabaAAtum shuAAayban
innakum ithanlakhasiroon
Swahili
Na waheshimiwa walio kufuru katika kaumu yake wakasema: Mkimfuata Shua'ib, basi
hakika hapo nyinyi mtakuwa mlio khasiri.
|
Ayah 7:91 الأية
فَأَخَذَتْهُمُ الرَّجْفَةُ فَأَصْبَحُوا فِي دَارِهِمْ جَاثِمِينَ
Faakhathat-humu arrajfatu faasbahoofee darihim jathimeen
Swahili
Basi tetemeko la ardhi likawanyakua, na wakaamkia majumbani mwao wamejifudikiza,
wamekwisha kufa.
|
Ayah 7:92 الأية
الَّذِينَ كَذَّبُوا شُعَيْبًا كَأَن لَّمْ يَغْنَوْا فِيهَا ۚ الَّذِينَ كَذَّبُوا
شُعَيْبًا كَانُوا هُمُ الْخَاسِرِينَ
Allatheena kaththabooshuAAayban kaan lam yaghnaw feeha allatheena
kaththabooshuAAayban kanoo humu alkhasireen
Swahili
Wale walio mkanusha Shua'ib wakawa kama kwamba hawakuwako. Walio mkanusha
Shua'ib ndio walio kuwa wenye kukhasiri.
|
Ayah 7:93 الأية
فَتَوَلَّىٰ عَنْهُمْ وَقَالَ يَا قَوْمِ لَقَدْ أَبْلَغْتُكُمْ رِسَالَاتِ رَبِّي
وَنَصَحْتُ لَكُمْ ۖ فَكَيْفَ آسَىٰ عَلَىٰ قَوْمٍ كَافِرِينَ
Fatawalla AAanhum waqala yaqawmi laqad ablaghtukum risalati rabbee
wanasahtulakum fakayfa asa AAala qawmin kafireen
Swahili
Basi akawaachilia mbali na akasema: Enyi kaumu yangu! Nimekufikishieni Ujumbe wa
Mola Mlezi wangu, na nimekunasihini; basi vipi niwahuzunikie watu makafiri?
|
Ayah 7:94 الأية
وَمَا أَرْسَلْنَا فِي قَرْيَةٍ مِّن نَّبِيٍّ إِلَّا أَخَذْنَا أَهْلَهَا
بِالْبَأْسَاءِ وَالضَّرَّاءِ لَعَلَّهُمْ يَضَّرَّعُونَ
Wama arsalna fee qaryatin minnabiyyin illa akhathna ahlaha bilba/sa-iwaddarra-i
laAAallahum yaddarraAAoon
Swahili
Na hatukumtuma Nabii yeyote katika mji ila tuliwapatiliza wakaazi wake kwa taabu
na mashaka ili wapate kunyenyekea.
|
Ayah 7:95 الأية
ثُمَّ بَدَّلْنَا مَكَانَ السَّيِّئَةِ الْحَسَنَةَ حَتَّىٰ عَفَوا وَّقَالُوا قَدْ
مَسَّ آبَاءَنَا الضَّرَّاءُ وَالسَّرَّاءُ فَأَخَذْنَاهُم بَغْتَةً وَهُمْ لَا
يَشْعُرُونَ
Thumma baddalna makana assayyi-atialhasanata hatta AAafaw waqaloo qadmassa
abaana addarraowassarrao faakhathnahum baghtatanwahum la yashAAuroon
Swahili
Kisha Sisi hubadilisha mahala pa ubaya kwa wema, hata wakazidi, na wakasema:
Taabu na raha ziliwafikia baba zetu. Basi kwa ghafla tukawashika, hali ya kuwa
hawajatambua.
|
Ayah 7:96 الأية
وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَىٰ آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِم
بَرَكَاتٍ مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَٰكِن كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُم بِمَا
كَانُوا يَكْسِبُونَ
Walaw anna ahla alqura amanoowattaqaw lafatahna AAalayhim barakatinmina assama-i
wal-ardi walakinkaththaboo faakhathnahum bima kanooyaksiboon
Swahili
Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli
wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi
tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.
|
Ayah 7:97 الأية
أَفَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا بَيَاتًا وَهُمْ نَائِمُونَ
Afaamina ahlu alqura an ya/tiyahumba/suna bayatan wahum na-imoon
Swahili
Je, watu wa mijini wameaminisha ya kuwa adhabu yetu haitawafika usiku, nao
wamelala?
|
Ayah 7:98 الأية
أَوَأَمِنَ أَهْلُ الْقُرَىٰ أَن يَأْتِيَهُم بَأْسُنَا ضُحًى وَهُمْ يَلْعَبُونَ
Awa amina ahlu alqura an ya/tiyahumba/suna duhan wahum yalAAaboon
Swahili
Au watu wa mijini wameaminisha ya kuwa adhabu yetu haitawafika mchana, nao
wanacheza?
|
Ayah 7:99 الأية
أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللهِ إِلَّا الْقَوْمُ
الْخَاسِرُونَ
Afaaminoo makra Allahi falaya/manu makra Allahi illa alqawmu alkhasiroon
Swahili
Je, wamejiaminisha na mipango ya Mwenyezi Mungu? Kwani hawajiaminishi na mipango
ya Mwenyezi Mungu ila watu wenye kukhasiri.
|
Ayah 7:100 الأية
أَوَلَمْ يَهْدِ لِلَّذِينَ يَرِثُونَ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ أَهْلِهَا أَن لَّوْ
نَشَاءُ أَصَبْنَاهُم بِذُنُوبِهِمْ ۚ وَنَطْبَعُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ لَا
يَسْمَعُونَ
Awa lam yahdi lillatheena yarithoonaal-arda min baAAdi ahliha an law nashao
asabnahumbithunoobihim wanatbaAAu AAala quloobihimfahum la yasmaAAoon
Swahili
Je, hawahidiki hawa wanao rithi ardhi baada ya wale wenyewe kwamba tukitaka
tutawapatiliza kwa madhambi yao, na tutapiga muhuri juu ya nyoyo zao, na kwa
hivyo hawatasikia?
|
Ayah 7:101 الأية
تِلْكَ الْقُرَىٰ نَقُصُّ عَلَيْكَ مِنْ أَنبَائِهَا ۚ وَلَقَدْ جَاءَتْهُمْ
رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَمَا كَانُوا لِيُؤْمِنُوا بِمَا كَذَّبُوا مِن قَبْلُ
ۚ كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللهُ عَلَىٰ قُلُوبِ الْكَافِرِينَ
Tilka alqura naqussu AAalaykamin anba-iha walaqad jaat-hum rusuluhum
bilbayyinatifama kanoo liyu/minoo bima kaththaboomin qablu kathalika yatbaAAu
Allahu AAalaquloobi alkafireen
Swahili
Miji hiyo, tunakusimulia baadhi ya khabari zake. Na hapana shaka Mitume wao
waliwafikia kwa hoja zilizo waziwazi. Lakini hawakuwa wenye kuamini waliyo
yakanusha zamani. Namna hivi Mwenyezi Mungu anazipiga muhuri nyoyo za makafiri.
|
Ayah 7:102 الأية
وَمَا وَجَدْنَا لِأَكْثَرِهِم مِّنْ عَهْدٍ ۖ وَإِن وَجَدْنَا أَكْثَرَهُمْ
لَفَاسِقِينَ
Wama wajadna li-aktharihimmin AAahdin wa-in wajadna aktharahum lafasiqeen
Swahili
Wala hatukuwaona wengi wao kuwa wanatimiza ahadi; bali kwa hakika tuliwakuta
wengi wao ni wapotofu.
|
Ayah 7:103 الأية
ثُمَّ بَعَثْنَا مِن بَعْدِهِم مُّوسَىٰ بِآيَاتِنَا إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ
فَظَلَمُوا بِهَا ۖ فَانظُرْ كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُفْسِدِينَ
Thumma baAAathna min baAAdihim moosabi-ayatina ila firAAawna
wamala-ihifathalamoo biha fanuthurkayfa kana AAaqibatu almufsideen
Swahili
Kisha baada yao tukamtuma Musa na Ishara zetu kwa Firauni na waheshimiwa wake.
Nao wakazikataa. Basi tazama ulikuwaje mwisho wa waharibifu.
|
Ayah 7:104 الأية
وَقَالَ مُوسَىٰ يَا فِرْعَوْنُ إِنِّي رَسُولٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ
Waqala moosa yafirAAawnu innee rasoolun min rabbi alAAalameen
Swahili
Na Musa alisema: Ewe Firauni! Hakika mimi ni Mtume nitokaye kwa Mola Mlezi wa
viumbe vyote.
|
Ayah 7:105 الأية
حَقِيقٌ عَلَىٰ أَن لَّا أَقُولَ عَلَى اللهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ قَدْ جِئْتُكُم
بِبَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَأَرْسِلْ مَعِيَ بَنِي إِسْرَائِيلَ
Haqeequn AAala an laaqoola AAala Allahi illa alhaqqa qadji/tukum bibayyinatin
min rabbikum faarsil maAAiya banee isra-eel
Swahili
Inafaa nisiseme juu ya Mwenyezi Mungu ila lilio la Haki. Nami hakika nimekujieni
na dalili waziwazi kutokana na Mola Mlezi wenu. Basi waache Wana wa Israili
wende nami.
|
Ayah 7:106 الأية
قَالَ إِن كُنتَ جِئْتَ بِآيَةٍ فَأْتِ بِهَا إِن كُنتَ مِنَ الصَّادِقِينَ
Qala in kunta ji/ta bi-ayatinfa/ti biha in kunta mina assadiqeen
Swahili
Akasema Firauni: Ikiwa umekuja na Ishara, basi ilete ukiwa ni katika wasemao
kweli.
|
Ayah 7:107 الأية
فَأَلْقَىٰ عَصَاهُ فَإِذَا هِيَ ثُعْبَانٌ مُّبِينٌ
Faalqa AAasahu fa-ithahiya thuAAbanun mubeen
Swahili
Basi akaitupa fimbo yake, na mara ikawa nyoka dhaahiri.
|
Ayah 7:108 الأية
وَنَزَعَ يَدَهُ فَإِذَا هِيَ بَيْضَاءُ لِلنَّاظِرِينَ
WanazaAAa yadahu fa-itha hiya baydaolinnathireen
Swahili
Na akatoa mkono wake, mara ukawa mweupe kwa watazamao.
|
Ayah 7:109 الأية
قَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِ فِرْعَوْنَ إِنَّ هَٰذَا لَسَاحِرٌ عَلِيمٌ
Qala almalao min qawmi firAAawnainna hatha lasahirun AAaleem
Swahili
Wakasema waheshimiwa wa kaumu ya Firauni: Hakika huyo ni mchawi mjuzi.
|
Ayah 7:110 الأية
يُرِيدُ أَن يُخْرِجَكُم مِّنْ أَرْضِكُمْ ۖ فَمَاذَا تَأْمُرُونَ
Yureedu an yukhrijakum min ardikumfamatha ta/muroon
Swahili
Anataka kukutoeni katika nchi yenu. Basi mnatoa shauri gani?
|
Ayah 7:111 الأية
قَالُوا أَرْجِهْ وَأَخَاهُ وَأَرْسِلْ فِي الْمَدَائِنِ حَاشِرِينَ
Qaloo arjih waakhahu waarsilfee almada-ini hashireen
Swahili
Wakasema: Mwache kidogo yeye na nduguye, na watume mijini wakusanyao,
|
Ayah 7:112 الأية
يَأْتُوكَ بِكُلِّ سَاحِرٍ عَلِيمٍ
Ya/tooka bikulli sahirin AAaleem
Swahili
Wakuletee kila mchawi mjuzi.
|
Ayah 7:113 الأية
وَجَاءَ السَّحَرَةُ فِرْعَوْنَ قَالُوا إِنَّ لَنَا لَأَجْرًا إِن كُنَّا نَحْنُ
الْغَالِبِينَ
Wajaa assaharatufirAAawna qaloo inna lana laajran in kunnanahnu alghalibeen
Swahili
Wakaja wachawi kwa Firauni, wakasema: Hakika tutapata ujira ikiwa tutashinda.
|
Ayah 7:114 الأية
قَالَ نَعَمْ وَإِنَّكُمْ لَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ
Qala naAAam wa-innakum laminaalmuqarrabeen
Swahili
Akasema: Naam! Nanyi bila ya shaka mtakuwa katika wa karibu nami.
|
Ayah 7:115 الأية
قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِمَّا أَن تُلْقِيَ وَإِمَّا أَن نَّكُونَ نَحْنُ
الْمُلْقِينَ
Qaloo ya moosa immaan tulqiya wa-imma an nakoona nahnu almulqeen
Swahili
Wakasema: Ewe Musa! Je, utatupa wewe, au tutakuwa sisi tutao tupa?
|
Ayah 7:116 الأية
قَالَ أَلْقُوا ۖ فَلَمَّا أَلْقَوْا سَحَرُوا أَعْيُنَ النَّاسِ
وَاسْتَرْهَبُوهُمْ وَجَاءُوا بِسِحْرٍ عَظِيمٍ
Qala alqoo falamma alqaw saharooaAAyuna annasi wastarhaboohum wajaoobisihrin
AAatheem
Swahili
Akasema: Tupeni! Basi walipo tupa waliyazuga macho ya watu na wakawatia khofu,
na wakaleta uchawi mkubwa.
|
Ayah 7:117 الأية
وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ مُوسَىٰ أَنْ أَلْقِ عَصَاكَ ۖ فَإِذَا هِيَ تَلْقَفُ مَا
يَأْفِكُونَ
Waawhayna ila moosaan alqi AAasaka fa-itha hiya talqafu maya/fikoon
Swahili
Nasi tukamfunulia Musa kumwambia: Tupa fimbo yako. Mara ikavimeza vyote vile
walivyo vibuni.
|
Ayah 7:118 الأية
فَوَقَعَ الْحَقُّ وَبَطَلَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
FawaqaAAa alhaqqu wabatala makanoo yaAAmaloon
Swahili
Kweli ikathibiti na yakabat'ilika waliyo kuwa wakiyatenda.
|
Ayah 7:119 الأية
فَغُلِبُوا هُنَالِكَ وَانقَلَبُوا صَاغِرِينَ
Faghuliboo hunalika wanqalaboosaghireen
Swahili
Kwa hivyo walishindwa hapo, na wakageuka kuwa wadogo.
|
|