1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
قَدْ أَفْلَحَ الْمُؤْمِنُونَ
Qad aflaha almu/minoon
Swahili
HAKIKA wamefanikiwa Waumini,
|
Ayah 23:2 الأية
الَّذِينَ هُمْ فِي صَلَاتِهِمْ خَاشِعُونَ
Allatheena hum fee salatihimkhashiAAoon
Swahili
Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao,
|
Ayah 23:3 الأية
وَالَّذِينَ هُمْ عَنِ اللَّغْوِ مُعْرِضُونَ
Wallatheena hum AAani allaghwimuAAridoon
Swahili
Na ambao hujiepusha na mambo ya upuuzi,
|
Ayah 23:4 الأية
وَالَّذِينَ هُمْ لِلزَّكَاةِ فَاعِلُونَ
Wallatheena hum lizzakatifaAAiloon
Swahili
Na ambao wanatoa Zaka,
|
Ayah 23:5 الأية
وَالَّذِينَ هُمْ لِفُرُوجِهِمْ حَافِظُونَ
Wallatheena hum lifuroojihim hafithoon
Swahili
Na ambao wanazilinda tupu zao,
|
Ayah 23:6 الأية
إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ
مَلُومِينَ
Illa AAala azwajihim awma malakat aymanuhum fa-innahum ghayru maloomeen
Swahili
Isipo kuwa kwa wake zao au kwa iliyo wamiliki mikono yao ya kulia. Kwani hao si
wenye kulaumiwa.
|
Ayah 23:7 الأية
فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ
Famani ibtagha waraa thalikafaola-ika humu alAAadoon
Swahili
Lakini anaye taka kinyume cha haya, basi hao ndio warukao mipaka.
|
Ayah 23:8 الأية
وَالَّذِينَ هُمْ لِأَمَانَاتِهِمْ وَعَهْدِهِمْ رَاعُونَ
Wallatheena hum li-amanatihimwaAAahdihim raAAoon
Swahili
Na ambao wanazitimiza amana zao na ahadi zao,
|
Ayah 23:9 الأية
وَالَّذِينَ هُمْ عَلَىٰ صَلَوَاتِهِمْ يُحَافِظُونَ
Wallatheena hum AAala salawatihimyuhafithoon
Swahili
Na ambao Sala zao wanazihifadhi -
|
Ayah 23:10 الأية
أُولَٰئِكَ هُمُ الْوَارِثُونَ
Ola-ika humu alwarithoon
Swahili
Hao ndio warithi,
|
Ayah 23:11 الأية
الَّذِينَ يَرِثُونَ الْفِرْدَوْسَ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Allatheena yarithoona alfirdawsa humfeeha khalidoon
Swahili
Ambao watairithi Pepo ya Firdausi, wadumu humo.
|
Ayah 23:12 الأية
وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنسَانَ مِن سُلَالَةٍ مِّن طِينٍ
Walaqad khalaqna al-insana minsulalatin min teen
Swahili
Na kwa yakini tumemuumba mtu kutokana na asli ya udongo.
|
Ayah 23:13 الأية
ثُمَّ جَعَلْنَاهُ نُطْفَةً فِي قَرَارٍ مَّكِينٍ
Thumma jaAAalnahu nutfatan feeqararin makeen
Swahili
Kisha tukamjaalia awe tone ya mbegu ya uzazi katika kalio madhubuti.
|
Ayah 23:14 الأية
ثُمَّ خَلَقْنَا النُّطْفَةَ عَلَقَةً فَخَلَقْنَا الْعَلَقَةَ مُضْغَةً
فَخَلَقْنَا الْمُضْغَةَ عِظَامًا فَكَسَوْنَا الْعِظَامَ لَحْمًا ثُمَّ
أَنشَأْنَاهُ خَلْقًا آخَرَ ۚ فَتَبَارَكَ اللهُ أَحْسَنُ الْخَالِقِينَ
Thumma khalaqna annutfataAAalaqatan fakhalaqna alAAalaqata mudghatanfakhalaqna
almudghata AAithamanfakasawna alAAithama lahmanthumma ansha/nahu khalqan akhara
fatabarakaAllahu ahsanu alkhaliqeen
Swahili
Kisha tukaiumba tone kuwa damu iliyo ganda, na tukaiumba damu kuwa pande la
nyama, kisha tukaliumba pande la nyama kuwa mifupa, na mifupa tukaivika nyama.
Kisha tukamfanya kiumbe mwengine. Basi ametukuka Mwenyezi Mungu Mbora wa
waumbaji.
|
Ayah 23:15 الأية
ثُمَّ إِنَّكُم بَعْدَ ذَٰلِكَ لَمَيِّتُونَ
Thumma innakum baAAda thalikalamayyitoon
Swahili
Kisha hakika nyinyi baada ya hayo mtakufa.
|
Ayah 23:16 الأية
ثُمَّ إِنَّكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ تُبْعَثُونَ
Thumma innakum yawma alqiyamatitubAAathoon
Swahili
Kisha hakika nyinyi Siku ya Kiyama mtafufuliwa.
|
Ayah 23:17 الأية
وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَائِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ الْخَلْقِ
غَافِلِينَ
Walaqad khalaqna fawqakum sabAAa tara-iqawama kunna AAani alkhalqi ghafileen
Swahili
Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na
viumbe.
|
Ayah 23:18 الأية
وَأَنزَلْنَا مِنَ السَّمَاءِ مَاءً بِقَدَرٍ فَأَسْكَنَّاهُ فِي الْأَرْضِ ۖ
وَإِنَّا عَلَىٰ ذَهَابٍ بِهِ لَقَادِرُونَ
Waanzalna mina assama-imaan biqadarin faaskannahu fee al-ardiwa-inna AAala
thahabin bihi laqadiroon
Swahili
Na tumeteremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi na tukayatuliza katika ardhi. Na
hakika Sisi tunaweza kuyaondoa.
|
Ayah 23:19 الأية
فَأَنشَأْنَا لَكُم بِهِ جَنَّاتٍ مِّن نَّخِيلٍ وَأَعْنَابٍ لَّكُمْ فِيهَا
فَوَاكِهُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ
Faansha/na lakum bihi jannatinmin nakheelin waaAAnabin lakum feeha
fawakihukatheeratun waminha ta/kuloon
Swahili
Kwa maji hayo tukakufanyieni bustani za mitende na mizabibu, mnapata humo
matunda mengi, na katika hayo mnakula;
|
Ayah 23:20 الأية
وَشَجَرَةً تَخْرُجُ مِن طُورِ سَيْنَاءَ تَنبُتُ بِالدُّهْنِ وَصِبْغٍ
لِّلْآكِلِينَ
Washajaratan takhruju min toori saynaatanbutu bidduhni wasibghin lilakileen
Swahili
Na mti utokao katika mlima wa Sinai, unatoa mafuta na kuwa kitoweo kwa walao.
|
Ayah 23:21 الأية
وَإِنَّ لَكُمْ فِي الْأَنْعَامِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِي بُطُونِهَا
وَلَكُمْ فِيهَا مَنَافِعُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ
Wa-inna lakum fee al-anAAamilaAAibratan nusqeekum mimma fee butoonihawalakum
feeha manafiAAu katheeratun waminhata/kuloon
Swahili
Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika
vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia
mnawala.
|
Ayah 23:22 الأية
وَعَلَيْهَا وَعَلَى الْفُلْكِ تُحْمَلُونَ
WaAAalayha waAAala alfulki tuhmaloon
Swahili
Na juu yao na juu ya marikebu mnabebwa.
|
Ayah 23:23 الأية
وَلَقَدْ أَرْسَلْنَا نُوحًا إِلَىٰ قَوْمِهِ فَقَالَ يَا قَوْمِ اعْبُدُوا اللهَ
مَا لَكُم مِّنْ إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Walaqad arsalna noohan ilaqawmihi faqala ya qawmi oAAbudoo Allaha malakum min
ilahin ghayruhu afala tattaqoon
Swahili
Na hakika tulimtuma Nuhu kwa watu wake, akasema: Enyi watu wangu! Muabuduni
Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna mungu asiye kuwa Yeye. Basi je! Hamwogopi?
|
Ayah 23:24 الأية
فَقَالَ الْمَلَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَوْمِهِ مَا هَٰذَا إِلَّا بَشَرٌ
مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ وَلَوْ شَاءَ اللهُ لَأَنزَلَ
مَلَائِكَةً مَّا سَمِعْنَا بِهَٰذَا فِي آبَائِنَا الْأَوَّلِينَ
Faqala almalao allatheenakafaroo min qawmihi ma hatha illa basharunmithlukum
yureedu an yatafaddala AAalaykum walaw shaaAllahu laanzala mala-ikatan ma
samiAAnabihatha fee aba-ina al-awwaleen
Swahili
Walisema wale wakuu walio kufuru katika watu wake: Huyu si chochote ila ni mtu
tu kama nyinyi. Anataka kujipa ubora juu yenu. Na lau kuwa Mwenyezi Mungu
amependa basi yakini angeli teremsha Malaika. Hatukusikia haya kwa baba zetu wa
zamani.
|
Ayah 23:25 الأية
إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ بِهِ جِنَّةٌ فَتَرَبَّصُوا بِهِ حَتَّىٰ حِينٍ
In huwa illa rajulun bihi jinnatunfatarabbasoo bihi hatta heen
Swahili
Huyu si lolote ila ni mtu mwenye wazimu. Basi mngojeeni tu kwa muda.
|
Ayah 23:26 الأية
قَالَ رَبِّ انصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ
Qala rabbi onsurnee bimakaththaboon
Swahili
Akasema (Nuhu): Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa kuwa wamenikanusha.
|
Ayah 23:27 الأية
فَأَوْحَيْنَا إِلَيْهِ أَنِ اصْنَعِ الْفُلْكَ بِأَعْيُنِنَا وَوَحْيِنَا فَإِذَا
جَاءَ أَمْرُنَا وَفَارَ التَّنُّورُ ۙ فَاسْلُكْ فِيهَا مِن كُلٍّ زَوْجَيْنِ
اثْنَيْنِ وَأَهْلَكَ إِلَّا مَن سَبَقَ عَلَيْهِ الْقَوْلُ مِنْهُمْ ۖ وَلَا
تُخَاطِبْنِي فِي الَّذِينَ ظَلَمُوا ۖ إِنَّهُم مُّغْرَقُونَ
Faawhayna ilayhi ani isnaAAialfulka bi-aAAyunina wawahyina fa-ithajaa amruna
wafara attannooru faslukfeeha min kullin zawjayni ithnayni waahlaka illaman
sabaqa AAalayhi alqawlu minhum wala tukhatibneefee allatheena thalamoo innahum
mughraqoon
Swahili
Tukampa wahyi: Unda jahazi mbele ya macho yetu na uwongozi wetu! Basi itapo fika
amri yetu na ikafurika tanuri, hapo waingize ndani yake wa kila namna dume na
jike, na ahali zako, isipo kuwa yule ambaye katika wao juu yake imekwisha
tangulia kauli. Wala usinitajie hao walio dhulumu. Kwani hao bila ya shaka
watazamishwa.
|
Ayah 23:28 الأية
فَإِذَا اسْتَوَيْتَ أَنتَ وَمَن مَّعَكَ عَلَى الْفُلْكِ فَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّهِ
الَّذِي نَجَّانَا مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Fa-itha istawayta anta waman maAAakaAAala alfulki faquli alhamdu lillahi
allatheenajjana mina alqawmi aththalimeen
Swahili
Basi utakapo tulia wewe na walio pamoja nawe humo marikebuni, sema:
Alhamdulillahi Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, aliye tuokoa na watu
madhaalimu!
|
Ayah 23:29 الأية
وَقُل رَّبِّ أَنزِلْنِي مُنزَلًا مُّبَارَكًا وَأَنتَ خَيْرُ الْمُنزِلِينَ
Waqul rabbi anzilnee munzalan mubarakanwaanta khayru almunzileen
Swahili
Na sema: Mola wangu Mlezi! Niteremshe mteremsho wenye baraka, na Wewe ni Mbora
wa wateremshaji.
|
Ayah 23:30 الأية
إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ وَإِن كُنَّا لَمُبْتَلِينَ
Inna fee thalika laayatinwa-in kunna lamubtaleen
Swahili
Hakika katika hayo yapo mazingatio. Na kwa yakini Sisi ni wenye kuwafanyia
mtihani.
|
Ayah 23:31 الأية
ثُمَّ أَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قَرْنًا آخَرِينَ
Thumma ansha/na min baAAdihim qarnan akhareen
Swahili
Kisha baada yao tukaanzisha kizazi kingine.
|
Ayah 23:32 الأية
فَأَرْسَلْنَا فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْهُمْ أَنِ اعْبُدُوا اللهَ مَا لَكُم مِّنْ
إِلَٰهٍ غَيْرُهُ ۖ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Faarsalna feehim rasoolan minhum anioAAbudoo Allaha ma lakum min ilahin
ghayruhuafala tattaqoon
Swahili
Tukawapelekea Mtume miongoni mwao, kuwaambia: Muabuduni Mwenyezi Mungu! Hamna
mungu asiye kuwa Yeye. Jee, hamwogopi?
|
Ayah 23:33 الأية
وَقَالَ الْمَلَأُ مِن قَوْمِهِ الَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِلِقَاءِ
الْآخِرَةِ وَأَتْرَفْنَاهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا مَا هَٰذَا إِلَّا بَشَرٌ
مِّثْلُكُمْ يَأْكُلُ مِمَّا تَأْكُلُونَ مِنْهُ وَيَشْرَبُ مِمَّا تَشْرَبُونَ
Waqala almalao min qawmihi allatheenakafaroo wakaththaboo biliqa-i
al-akhiratiwaatrafnahum fee alhayati addunyama hatha illa basharun mithlukum
ya/kulumimma ta/kuloona minhu wayashrabu mimma tashraboon
Swahili
Na wakubwa katika watu wake walio kufuru na wakakanusha mkutano wa Akhera, na
tukawadekeza kwa starehe katika maisha ya dunia, walisema: Huyu si chochote ila
ni binaadamu kama nyinyi; anakula mlacho, na anakunywa mnywacho.
|
Ayah 23:34 الأية
وَلَئِنْ أَطَعْتُم بَشَرًا مِّثْلَكُمْ إِنَّكُمْ إِذًا لَّخَاسِرُونَ
Wala-in ataAAtum basharan mithlakuminnakum ithan lakhasiroon
Swahili
Na nyinyi mkimt'ii mtu kama nyinyi basi hakika mtakuwa khasarani.
|
Ayah 23:35 الأية
أَيَعِدُكُمْ أَنَّكُمْ إِذَا مِتُّمْ وَكُنتُمْ تُرَابًا وَعِظَامًا أَنَّكُم
مُّخْرَجُونَ
AyaAAidukum annakum itha mittumwakuntum turaban waAAithaman annakummukhrajoon
Swahili
Hivyo anakuahidini ati ya kwamba mtakapo kufa na mkawa udongo na mifupa kuwa
mtatolewa?
|
Ayah 23:36 الأية
هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ لِمَا تُوعَدُونَ
Hayhata hayhata limatooAAadoon
Swahili
Hayawi! Hayawi hayo mnayo ahidiwa.
|
Ayah 23:37 الأية
إِنْ هِيَ إِلَّا حَيَاتُنَا الدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ
بِمَبْعُوثِينَ
In hiya illa hayatunaaddunya namootu wanahya wamanahnu bimabAAootheen
Swahili
Hapana ila uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi basi. Wala sisi
hatutafufuliwa.
|
Ayah 23:38 الأية
إِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ افْتَرَىٰ عَلَى اللهِ كَذِبًا وَمَا نَحْنُ لَهُ
بِمُؤْمِنِينَ
In huwa illa rajulun iftaraAAala Allahi kathiban wama nahnulahu bimu/mineen
Swahili
Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa
kumuamini.
|
Ayah 23:39 الأية
قَالَ رَبِّ انصُرْنِي بِمَا كَذَّبُونِ
Qala rabbi onsurnee bimakaththaboon
Swahili
Akasema: Mola wangu Mlezi! Ninusuru kwa sababu wananikanusha.
|
Ayah 23:40 الأية
قَالَ عَمَّا قَلِيلٍ لَّيُصْبِحُنَّ نَادِمِينَ
Qala AAamma qaleelin layusbihunnanadimeen
Swahili
(Mwenyezi Mungu) akasema: Baada ya muda mchache watakuwa wenye kujuta.
|
Ayah 23:41 الأية
فَأَخَذَتْهُمُ الصَّيْحَةُ بِالْحَقِّ فَجَعَلْنَاهُمْ غُثَاءً ۚ فَبُعْدًا
لِّلْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Faakhathat-humu assayhatubilhaqqi fajaAAalnahum ghuthaanfabuAAdan lilqawmi
aththalimeen
Swahili
Basi ukawanyakua ukelele kwa haki, na tukawafanya kama takataka zinazo elea juu
ya maji. Ikapotelea mbali kaumu ya madhaalimu!
|
Ayah 23:42 الأية
ثُمَّ أَنشَأْنَا مِن بَعْدِهِمْ قُرُونًا آخَرِينَ
Thumma ansha/na min baAAdihimquroonan akhareen
Swahili
Kisha tukaleta baada yao vizazi vingine.
|
Ayah 23:43 الأية
مَا تَسْبِقُ مِنْ أُمَّةٍ أَجَلَهَا وَمَا يَسْتَأْخِرُونَ
Ma tasbiqu min ommatin ajalahawama yasta/khiroon
Swahili
Hapana umma uwezao kutanguliza ajali yake wala kuikawiza.
|
Ayah 23:44 الأية
ثُمَّ أَرْسَلْنَا رُسُلَنَا تَتْرَىٰ ۖ كُلَّ مَا جَاءَ أُمَّةً رَّسُولُهَا
كَذَّبُوهُ ۚ فَأَتْبَعْنَا بَعْضَهُم بَعْضًا وَجَعَلْنَاهُمْ أَحَادِيثَ ۚ
فَبُعْدًا لِّقَوْمٍ لَّا يُؤْمِنُونَ
Thumma arsalna rusulana tatrakulla ma jaa ommatan rasooluha
kaththaboohufaatbaAAna baAAdahum baAAdan wajaAAalnahumahadeetha fabuAAdan
liqawmin la yu/minoon
Swahili
Kisha tukawatuma Mitume wetu, mmoja baada ya mmoja. Kila umma alipo wafikia
Mtume wao walimkanusha. Tukawafuatanisha hawa baada ya hawa, na tukawafanya ni
hadithi za kusimuliwa. Wakapotelea mbali watu wasio amini.
|
Ayah 23:45 الأية
ثُمَّ أَرْسَلْنَا مُوسَىٰ وَأَخَاهُ هَارُونَ بِآيَاتِنَا وَسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
Thumma arsalna moosa waakhahuharoona bi-ayatina wasultaninmubeen
Swahili
Kisha tukamtuma Musa na nduguye, Haaruni, pamoja na ishara zetu na hoja zilizo
wazi.
|
Ayah 23:46 الأية
إِلَىٰ فِرْعَوْنَ وَمَلَئِهِ فَاسْتَكْبَرُوا وَكَانُوا قَوْمًا عَالِينَ
Ila firAAawna wamala-ihi fastakbaroowakanoo qawman AAaleen
Swahili
Kumwendea Firauni na wakuu wake. Lakini walijivuna, nao walikuwa watu majeuri.
|
Ayah 23:47 الأية
فَقَالُوا أَنُؤْمِنُ لِبَشَرَيْنِ مِثْلِنَا وَقَوْمُهُمَا لَنَا عَابِدُونَ
Faqaloo anu/minu libasharayni mithlinawaqawmuhuma lana AAabidoon
Swahili
Wakasema: Je, tuwaamini wanaadamu wawili hawa kama sisi, na ambao watu wao ni
watumwa wetu?
|
Ayah 23:48 الأية
فَكَذَّبُوهُمَا فَكَانُوا مِنَ الْمُهْلَكِينَ
Fakaththaboohuma fakanoomina almuhlakeen
Swahili
Basi wakawakanusha, na wakawa miongoni mwa walio angamizwa.
|
Ayah 23:49 الأية
وَلَقَدْ آتَيْنَا مُوسَى الْكِتَابَ لَعَلَّهُمْ يَهْتَدُونَ
Walaqad atayna moosaalkitaba laAAallahum yahtadoon
Swahili
Na hakika tulimpa Musa Kitabu ili wapate kuongoka.
|
Ayah 23:50 الأية
وَجَعَلْنَا ابْنَ مَرْيَمَ وَأُمَّهُ آيَةً وَآوَيْنَاهُمَا إِلَىٰ رَبْوَةٍ ذَاتِ
قَرَارٍ وَمَعِينٍ
WajaAAalna ibna maryama waommahu ayatanwaawaynahuma ila rabwatin thatiqararin
wamaAAeen
Swahili
Na tukamfanya mwana wa Mariamu na mama yake kuwa ni Ishara, na tukawapa
makimbilio kwenda mahali palipo inuka penye utulivu na chemchem za maji.
|
Ayah 23:51 الأية
يَا أَيُّهَا الرُّسُلُ كُلُوا مِنَ الطَّيِّبَاتِ وَاعْمَلُوا صَالِحًا ۖ إِنِّي
بِمَا تَعْمَلُونَ عَلِيمٌ
Ya ayyuha arrusulukuloo mina attayyibati waAAmaloo salihaninnee bima taAAmaloona
AAaleem
Swahili
Enyi Mitume! Kuleni vyakula vizuri na tendeni mema. Hakika Mimi ni Mjuzi wa
mnayo yatenda.
|
Ayah 23:52 الأية
وَإِنَّ هَٰذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاتَّقُونِ
Wa-inna hathihi ommatukum ommatan wahidatanwaana rabbukum fattaqoon
Swahili
Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi
nicheni Mimi.
|
Ayah 23:53 الأية
فَتَقَطَّعُوا أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍ بِمَا لَدَيْهِمْ
فَرِحُونَ
FataqattaAAoo amrahum baynahumzuburan kullu hizbin bima ladayhim farihoon
Swahili
Lakini walikatiana jambo lao mapande mbali mbali. Kila kundi likifurahia kwa
waliyo nayo.
|
Ayah 23:54 الأية
فَذَرْهُمْ فِي غَمْرَتِهِمْ حَتَّىٰ حِينٍ
Fatharhum fee ghamratihim hattaheen
Swahili
Basi waache katika ghafla yao kwa muda.
|
Ayah 23:55 الأية
أَيَحْسَبُونَ أَنَّمَا نُمِدُّهُم بِهِ مِن مَّالٍ وَبَنِينَ
Ayahsaboona annama numidduhumbihi min malin wabaneen
Swahili
Je! Wanadhani ya kuwa kwa vile tunavyo wapa mali na watoto
|
Ayah 23:56 الأية
نُسَارِعُ لَهُمْ فِي الْخَيْرَاتِ ۚ بَل لَّا يَشْعُرُونَ
NusariAAu lahum fee alkhayratibal la yashAAuroon
Swahili
Ndio tunawahimizia kheri? Lakini wenyewe hawatambui.
|
Ayah 23:57 الأية
إِنَّ الَّذِينَ هُم مِّنْ خَشْيَةِ رَبِّهِم مُّشْفِقُونَ
Inna allatheena hum min khashyatirabbihim mushfiqoon
Swahili
Kwa hakika hao ambao kwa kumwogopa Mola wao Mlezi wananyenyekea,
|
Ayah 23:58 الأية
وَالَّذِينَ هُم بِآيَاتِ رَبِّهِمْ يُؤْمِنُونَ
Wallatheena hum bi-ayatirabbihim yu/minoon
Swahili
Na wale ambao Ishara za Mola wao Mlezi wanaziamini,
|
Ayah 23:59 الأية
وَالَّذِينَ هُم بِرَبِّهِمْ لَا يُشْرِكُونَ
Wallatheena hum birabbihim layushrikoon
Swahili
Na wale ambao Mola wao Mlezi hawamshirikishi,
|
Ayah 23:60 الأية
وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوا وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَىٰ
رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ
Wallatheena yu/toona maataw waquloobuhum wajilatun annahum ila rabbihim
rajiAAoon
Swahili
Na wale ambao wanatoa walicho pewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa
watarejea kwa Mola wao Mlezi,
|
Ayah 23:61 الأية
أُولَٰئِكَ يُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَهُمْ لَهَا سَابِقُونَ
Ola-ika yusariAAoona feealkhayrati wahum laha sabiqoon
Swahili
Basi wote hao ndio wanao kimbilia katika mambo ya kheri, na ndio watakao
tangulia kuyafikia.
|
Ayah 23:62 الأية
وَلَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَلَدَيْنَا كِتَابٌ يَنطِقُ
بِالْحَقِّ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Wala nukallifu nafsan illawusAAaha waladayna kitabun yantiqu bilhaqqiwahum la
yuthlamoon
Swahili
Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho
kweli. Nao hawatadhulumiwa.
|
Ayah 23:63 الأية
بَلْ قُلُوبُهُمْ فِي غَمْرَةٍ مِّنْ هَٰذَا وَلَهُمْ أَعْمَالٌ مِّن دُونِ ذَٰلِكَ
هُمْ لَهَا عَامِلُونَ
Bal quloobuhum fee ghamratin min hathawalahum aAAmalun min dooni thalika hum
lahaAAamiloon
Swahili
Lakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo
vifanya.
|
Ayah 23:64 الأية
حَتَّىٰ إِذَا أَخَذْنَا مُتْرَفِيهِم بِالْعَذَابِ إِذَا هُمْ يَجْأَرُونَ
Hatta itha akhathnamutrafeehim bilAAathabi itha hum yaj-aroon
Swahili
Hata tutakapo watia katika adhabu wale walio dekezwa kwa starehe kati yao, hapo
ndipo watapo yayatika.
|
Ayah 23:65 الأية
لَا تَجْأَرُوا الْيَوْمَ ۖ إِنَّكُم مِّنَّا لَا تُنصَرُونَ
La taj-aroo alyawma innakum minnala tunsaroon
Swahili
Msiyayatike leo! Hakika nyinyi hamtanusurika nasi.
|
Ayah 23:66 الأية
قَدْ كَانَتْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ
تَنكِصُونَ
Qad kanat ayatee tutlaAAalaykum fakuntum AAala aAAqabikum tankisoon
Swahili
Hakika zilikuwa Aya zangu mkisomewa, nanyi mkirudi nyuma juu ya visigino vyenu,
|
Ayah 23:67 الأية
مُسْتَكْبِرِينَ بِهِ سَامِرًا تَهْجُرُونَ
Mustakbireena bihi samiran tahjuroon
Swahili
Na huku mkitakabari na usiku mkiizungumza (Qur'ani) kwa dharau.
|
Ayah 23:68 الأية
أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا الْقَوْلَ أَمْ جَاءَهُم مَّا لَمْ يَأْتِ آبَاءَهُمُ
الْأَوَّلِينَ
Afalam yaddabbaroo alqawla am jaahumma lam ya/ti abaahumu al-awwaleen
Swahili
Je, hawakuifikiri kauli, au yamewajia yasiyo wafikia baba zao wa zamani?
|
Ayah 23:69 الأية
أَمْ لَمْ يَعْرِفُوا رَسُولَهُمْ فَهُمْ لَهُ مُنكِرُونَ
Am lam yaAArifoo rasoolahum fahum lahumunkiroon
Swahili
Au hawakumjua Mtume wao, ndio maana wanamkataa?
|
Ayah 23:70 الأية
أَمْ يَقُولُونَ بِهِ جِنَّةٌ ۚ بَلْ جَاءَهُم بِالْحَقِّ وَأَكْثَرُهُمْ لِلْحَقِّ
كَارِهُونَ
Am yaqooloona bihi jinnatun bal jaahumbilhaqqi waaktharuhum lilhaqqi karihoon
Swahili
Au wanasema: Ana wazimu? Bali amewajia kwa Haki, na wengi wao wanaichukia Haki.
|
Ayah 23:71 الأية
وَلَوِ اتَّبَعَ الْحَقُّ أَهْوَاءَهُمْ لَفَسَدَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ
وَمَن فِيهِنَّ ۚ بَلْ أَتَيْنَاهُم بِذِكْرِهِمْ فَهُمْ عَن ذِكْرِهِم
مُّعْرِضُونَ
Walawi ittabaAAa alhaqqu ahwaahumlafasadati assamawatu wal-arduwaman feehinna
bal ataynahum bithikrihim fahum AAanthikrihim muAAridoon
Swahili
Na lau kuwa Haki ingeli fuata matamanio yao, basi zingeli haribika mbingu na
ardhi na waliomo ndani. Bali tumewaletea ukumbusho wao, nao wanajitenga mbali na
ukumbusho wao.
|
Ayah 23:72 الأية
أَمْ تَسْأَلُهُمْ خَرْجًا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيْرٌ ۖ وَهُوَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
Am tas-aluhum kharjan fakharajurabbika khayrun wahuwa khayru arraziqeen
Swahili
Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora
wa wanao ruzuku.
|
Ayah 23:73 الأية
وَإِنَّكَ لَتَدْعُوهُمْ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Wa-innaka latadAAoohum ila siratinmustaqeem
Swahili
Na kwa yakini wewe unawaita kwenye Njia Iliyo Nyooka.
|
Ayah 23:74 الأية
وَإِنَّ الَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِالْآخِرَةِ عَنِ الصِّرَاطِ لَنَاكِبُونَ
Wa-inna allatheena layu/minoona bil-akhirati AAani assiratilanakiboon
Swahili
Na hakika wale wasio iamini Akhera wanajitenga na Njia hiyo.
|
Ayah 23:75 الأية
وَلَوْ رَحِمْنَاهُمْ وَكَشَفْنَا مَا بِهِم مِّن ضُرٍّ لَّلَجُّوا فِي
طُغْيَانِهِمْ يَعْمَهُونَ
Walaw rahimnahum wakashafnama bihim min durrin lalajjoo fee
tughyanihimyaAAmahoon
Swahili
Na lau tungeli warehemu na tukawaondolea shida waliyo nayo bila ya shaka wangeli
endelea katika upotofu wao vile vile, wakitangatanga.
|
Ayah 23:76 الأية
وَلَقَدْ أَخَذْنَاهُم بِالْعَذَابِ فَمَا اسْتَكَانُوا لِرَبِّهِمْ وَمَا
يَتَضَرَّعُونَ
Walaqad akhathnahum bilAAathabifama istakanoo lirabbihim wama yatadarraAAoon
Swahili
Na hakika tuliwatia adhabu kali; lakini hawakuelekea kwa Mola wao Mlezi wala
hawakunyenyekea.
|
Ayah 23:77 الأية
حَتَّىٰ إِذَا فَتَحْنَا عَلَيْهِم بَابًا ذَا عَذَابٍ شَدِيدٍ إِذَا هُمْ فِيهِ
مُبْلِسُونَ
Hatta itha fatahnaAAalayhim baban tha AAathabin shadeedin ithahum feehi
mublisoon
Swahili
Mpaka tulipo wafungulia mlango wa adhabu kali, hapo ndipo wakawa wenye kukata
tamaa.
|
Ayah 23:78 الأية
وَهُوَ الَّذِي أَنشَأَ لَكُمُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَالْأَفْئِدَةَ ۚ
قَلِيلًا مَّا تَشْكُرُونَ
Wahuwa allathee anshaa lakumu assamAAawal-absara wal-af-idata qaleelan
matashkuroon
Swahili
Na Yeye ndiye aliye kuumbieni kusikia na kuona na nyoyo za kufahamu. Ni kuchache
mno kushukuru kwenu.
|
Ayah 23:79 الأية
وَهُوَ الَّذِي ذَرَأَكُمْ فِي الْأَرْضِ وَإِلَيْهِ تُحْشَرُونَ
Wahuwa allathee tharaakum feeal-ardi wa-ilayhi tuhsharoon
Swahili
Na Yeye ndiye aliye kuenezeni katika ardhi, na kwake Yeye mtakusanywa.
|
Ayah 23:80 الأية
وَهُوَ الَّذِي يُحْيِي وَيُمِيتُ وَلَهُ اخْتِلَافُ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ ۚ
أَفَلَا تَعْقِلُونَ
Wahuwa allathee yuhyeewayumeetu walahu ikhtilafu allayli wannahariafala
taAAqiloon
Swahili
Na Yeye ndiye anaye huisha na kufisha, na yake Yeye mabadiliko ya usiku na
mchana. Basi je! Hamfahamu?
|
Ayah 23:81 الأية
بَلْ قَالُوا مِثْلَ مَا قَالَ الْأَوَّلُونَ
Bal qaloo mithla ma qalaal-awwaloon
Swahili
Bali wanasema kama walivyo sema watu wa kwanza.
|
Ayah 23:82 الأية
قَالُوا أَإِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَامًا أَإِنَّا لَمَبْعُوثُونَ
Qaloo a-itha mitnawakunna turaban waAAithamana-inna lamabAAoothoon
Swahili
Walisema: Je! Tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa?
|
Ayah 23:83 الأية
لَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَآبَاؤُنَا هَٰذَا مِن قَبْلُ إِنْ هَٰذَا إِلَّا
أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ
Laqad wuAAidna nahnu waabaonahatha min qablu in hatha illa asateerual-awwaleen
Swahili
Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo
vya watu wa zamani.
|
Ayah 23:84 الأية
قُل لِّمَنِ الْأَرْضُ وَمَن فِيهَا إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Qul limani al-ardu waman feehain kuntum taAAlamoon
Swahili
Sema: Ni ya nani ardhi na viliomo ndani yake, kama nyinyi mnajua?
|
Ayah 23:85 الأية
سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Sayaqooloona lillahi qul afalatathakkaroon
Swahili
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu! Sema: Basi, je, hamkumbuki?
|
Ayah 23:86 الأية
قُلْ مَن رَّبُّ السَّمَاوَاتِ السَّبْعِ وَرَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ
Qul man rabbu assamawatiassabAAi warabbu alAAarshi alAAatheem
Swahili
Sema: Ni nani Mola Mlezi wa mbingu saba na Mola Mlezi wa A'rshi Kuu?
|
Ayah 23:87 الأية
سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ
Sayaqooloona lillahi qul afalatattaqoon
Swahili
Watasema: Ni vya Mwenyezi Mungu. Sema: Basi je, hamwogopi?
|
Ayah 23:88 الأية
قُلْ مَن بِيَدِهِ مَلَكُوتُ كُلِّ شَيْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ
إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Qul man biyadihi malakootu kulli shay-inwahuwa yujeeru wala yujaru AAalayhi in
kuntumtaAAlamoon
Swahili
Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda,
wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua?
|
Ayah 23:89 الأية
سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ
Sayaqooloona lillahi qul faannatusharoon
Swahili
Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika?
|
Ayah 23:90 الأية
بَلْ أَتَيْنَاهُم بِالْحَقِّ وَإِنَّهُمْ لَكَاذِبُونَ
Bal ataynahum bilhaqqiwa-innahum lakathiboon
Swahili
Bali tumewaletea Haki, na kwa yakini hao ni waongo.
|
Ayah 23:91 الأية
مَا اتَّخَذَ اللهُ مِن وَلَدٍ وَمَا كَانَ مَعَهُ مِنْ إِلَٰهٍ ۚ إِذًا
لَّذَهَبَ كُلُّ إِلَٰهٍ بِمَا خَلَقَ وَلَعَلَا بَعْضُهُمْ عَلَىٰ بَعْضٍ ۚ
سُبْحَانَ اللهِ عَمَّا يَصِفُونَ
Ma ittakhatha Allahumin waladin wama kana maAAahu min ilahin ithanlathahaba
kullu ilahin bima khalaqa walaAAalabaAAduhum AAala baAAdin subhana AllahiAAamma
yasifoon
Swahili
Mwenyezi Mungu hana mwana yeyote, wala hanaye mungu mwengine. Inge kuwa hivyo
basi kila mungu angeli chukua alivyo umba, na baadhi yao wangeli washinda
wengine. Mwenyezi Mungu ameepukana na sifa wanazo msifu.
|
Ayah 23:92 الأية
عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَتَعَالَىٰ عَمَّا يُشْرِكُونَ
AAalimi alghaybi washshahadatifataAAala AAamma yushrikoon
Swahili
Mjuzi wa siri na dhaahiri, na ametukuka juu ya hayo wanayo mshirikisha nayo.
|
Ayah 23:93 الأية
قُل رَّبِّ إِمَّا تُرِيَنِّي مَا يُوعَدُونَ
Qul rabbi imma turiyannee mayooAAadoon
Swahili
Sema: Mola wangu Mlezi! Ukinionyesha adhabu waliyo ahidiwa,
|
Ayah 23:94 الأية
رَبِّ فَلَا تَجْعَلْنِي فِي الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
Rabbi fala tajAAalnee fee alqawmi aththalimeen
Swahili
Mola wangu Mlezi! Usinijaalie katika watu madhaalimu hao.
|
Ayah 23:95 الأية
وَإِنَّا عَلَىٰ أَن نُّرِيَكَ مَا نَعِدُهُمْ لَقَادِرُونَ
Wa-inna AAala an nuriyaka manaAAiduhum laqadiroon
Swahili
Na hakika Sisi ni waweza wa kukuonyeshsa tuliyo waahidi.
|
Ayah 23:96 الأية
ادْفَعْ بِالَّتِي هِيَ أَحْسَنُ السَّيِّئَةَ ۚ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ
IdfaAA billatee hiya ahsanu assayyi-atanahnu aAAlamu bima yasifoon
Swahili
Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo.
|
Ayah 23:97 الأية
وَقُل رَّبِّ أَعُوذُ بِكَ مِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ
Waqul rabbi aAAoothu bika min hamazatiashshayateen
Swahili
Na sema: Mola wangu Mlezi! Najikinga kwako na wasiwasi wa mashet'ani.
|
Ayah 23:98 الأية
وَأَعُوذُ بِكَ رَبِّ أَن يَحْضُرُونِ
WaaAAoothu bika rabbi an yahduroon
Swahili
Na najikinga kwako, Mola wangu Mlezi, wasinikaribie.
|
Ayah 23:99 الأية
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ
Hatta itha jaa ahadahumualmawtu qala rabbi irjiAAoon
Swahili
Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe.
|
Ayah 23:100 الأية
لَعَلِّي أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ
قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ
LaAAallee aAAmalu salihanfeema taraktu kalla innaha kalimatun huwa qa-iluhawamin
wara-ihim barzakhun ila yawmi yubAAathoon
Swahili
Ili nitende mema sasa badala ya yale niliyo yaacha. Wapi! Hii ni kauli aisemayo
yeye tu. Na nyuma yao kipo kizuizi mpaka siku watapo fufuliwa.
|
Ayah 23:101 الأية
فَإِذَا نُفِخَ فِي الصُّورِ فَلَا أَنسَابَ بَيْنَهُمْ يَوْمَئِذٍ وَلَا
يَتَسَاءَلُونَ
Fa-itha nufikha fee assoorifala ansaba baynahum yawma-ithin walayatasaaloon
Swahili
Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala
hawataulizana.
|
Ayah 23:102 الأية
فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
Faman thaqulat mawazeenuhu faola-ikahumu almuflihoon
Swahili
Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio wenye kufanikiwa.
|
Ayah 23:103 الأية
وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي
جَهَنَّمَ خَالِدُونَ
Waman khaffat mawazeenuhu faola-ikaallatheena khasiroo anfusahum fee jahannama
khalidoon
Swahili
Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio walio zitia khasarani nafsi
zao, na katika Jahannamu watadumu.
|
Ayah 23:104 الأية
تَلْفَحُ وُجُوهَهُمُ النَّارُ وَهُمْ فِيهَا كَالِحُونَ
Talfahu wujoohahumu annaruwahum feeha kalihoon
Swahili
Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana.
|
Ayah 23:105 الأية
أَلَمْ تَكُنْ آيَاتِي تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ فَكُنتُم بِهَا تُكَذِّبُونَ
Alam takun ayatee tutlaAAalaykum fakuntum biha tukaththiboon
Swahili
Je! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi mkizikanusha?
|
Ayah 23:106 الأية
قَالُوا رَبَّنَا غَلَبَتْ عَلَيْنَا شِقْوَتُنَا وَكُنَّا قَوْمًا ضَالِّينَ
Qaloo rabbana ghalabatAAalayna shiqwatuna wakunna qawman dalleen
Swahili
Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa watu tulio potea.
|
Ayah 23:107 الأية
رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْهَا فَإِنْ عُدْنَا فَإِنَّا ظَالِمُونَ
Rabbana akhrijna minhafa-in AAudna fa-inna thalimoon
Swahili
Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi kweli sisi ni wenye
kudhulumu.
|
Ayah 23:108 الأية
قَالَ اخْسَئُوا فِيهَا وَلَا تُكَلِّمُونِ
Qala ikhsaoo feeha walatukallimoon
Swahili
Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala msinisemeze.
|
Ayah 23:109 الأية
إِنَّهُ كَانَ فَرِيقٌ مِّنْ عِبَادِي يَقُولُونَ رَبَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا
وَارْحَمْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّاحِمِينَ
Innahu kana fareequn min AAibadeeyaqooloona rabbana amanna faghfirlana warhamna
waanta khayru arrahimeen
Swahili
Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu likisema: Mola wetu Mlezi!
Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe Mbora wa wanao rehemu.
|
Ayah 23:110 الأية
فَاتَّخَذْتُمُوهُمْ سِخْرِيًّا حَتَّىٰ أَنسَوْكُمْ ذِكْرِي وَكُنتُم مِّنْهُمْ
تَضْحَكُونَ
Fattakhathtumoohumsikhriyyan hatta ansawkum thikree wakuntumminhum tadhakoon
Swahili
Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni kunikumbuka, na mlikuwa
mkiwacheka.
|
Ayah 23:111 الأية
إِنِّي جَزَيْتُهُمُ الْيَوْمَ بِمَا صَبَرُوا أَنَّهُمْ هُمُ الْفَائِزُونَ
Innee jazaytuhumu alyawma bima sabarooannahum humu alfa-izoon
Swahili
Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyo subiri. Bila ya shaka hao ndio wenye
kufuzu.
|
Ayah 23:112 الأية
قَالَ كَمْ لَبِثْتُمْ فِي الْأَرْضِ عَدَدَ سِنِينَ
Qala kam labithtum fee al-ardiAAadada sineen
Swahili
Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya miaka?
|
Ayah 23:113 الأية
قَالُوا لَبِثْنَا يَوْمًا أَوْ بَعْضَ يَوْمٍ فَاسْأَلِ الْعَادِّينَ
Qaloo labithna yawman aw baAAdayawmin fas-ali alAAaddeen
Swahili
Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu.
|
Ayah 23:114 الأية
قَالَ إِن لَّبِثْتُمْ إِلَّا قَلِيلًا ۖ لَّوْ أَنَّكُمْ كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Qala in labithtum illaqaleelan law annakum kuntum taAAlamoon
Swahili
Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua.
|
Ayah 23:115 الأية
أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا
تُرْجَعُونَ
Afahasibtum annama khalaqnakumAAabathan waannakum ilayna la turjaAAoon
Swahili
Je! Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu
hamtarudishwa?
|
Ayah 23:116 الأية
فَتَعَالَى اللهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ
الْكَرِيمِ
FataAAala Allahualmaliku alhaqqu la ilaha illa huwarabbu alAAarshi alkareem
Swahili
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa
A'rshi Tukufu.
|
Ayah 23:117 الأية
وَمَن يَدْعُ مَعَ اللهِ إِلَٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا
حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ
Waman yadAAu maAAa Allahi ilahanakhara la burhana lahu bihi fa-innamahisabuhu
AAinda rabbihi innahu la yuflihualkafiroon
Swahili
Na anaye muomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe hana ushahidi wa
hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika
makafiri hawafanikiwi.
|
|