1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ الْمَلِكِ
الْقُدُّوسِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ
Yusabbihu lillahi ma feeassamawati wama fee al-ardialmaliki alquddoosi
alAAazeezi alhakeem
Swahili
Viliomo mbinguni na viliomo katika ardhi vinamtakasa Mwenyezi Mungu, Mfalme,
Mtakatifu, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
|
Ayah 62:2 الأية
هُوَ الَّذِي بَعَثَ فِي الْأُمِّيِّينَ رَسُولًا مِّنْهُمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ
آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا
مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ
Huwa allathee baAAatha feeal-ommiyyeena rasoolan minhum yatloo AAalayhim
ayatihiwayuzakkeehim wayuAAallimuhumu alkitaba walhikmatawa-in kanoo min qablu
lafee dalalin mubeen
Swahili
Yeye ndiye aliye mpeleka Mtume kwenye watu wasio jua kusoma, awasomee Aya zake
na awatakase, na awafunze Kitabu na hikima, ijapo kuwa kabla ya haya walikuwa
katika upotofu ulio dhaahiri.
|
Ayah 62:3 الأية
وَآخَرِينَ مِنْهُمْ لَمَّا يَلْحَقُوا بِهِمْ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
Waakhareena minhum lamma yalhaqoobihim wahuwa alAAazeezu alhakeem
Swahili
Na kwa wengine ambao bado hawajaungana nao. Na Yeye ndiye Mwenye nguvu, Mwenye
hikima.
|
Ayah 62:4 الأية
ذَٰلِكَ فَضْلُ اللهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللهُ ذُو الْفَضْلِ
الْعَظِيمِ
Thalika fadlu Allahiyu/teehi man yashao wallahu thooalfadli alAAatheem
Swahili
Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu anayo mpa amtakaye. Na Mwenyezi Mungu ni
Mwenye fadhila kubwa.
|
Ayah 62:5 الأية
مَثَلُ الَّذِينَ حُمِّلُوا التَّوْرَاةَ ثُمَّ لَمْ يَحْمِلُوهَا كَمَثَلِ
الْحِمَارِ يَحْمِلُ أَسْفَارًا ۚ بِئْسَ مَثَلُ الْقَوْمِ الَّذِينَ كَذَّبُوا
بِآيَاتِ اللهِ ۚ وَاللهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ
Mathalu allatheena hummiloo attawratathumma lam yahmilooha kamathali
alhimariyahmilu asfaran bi/sa mathalu alqawmi allatheenakaththaboo bi-ayati
Allahi wallahula yahdee alqawma aththalimeen
Swahili
Mfano wa walio bebeshwa Taurati kisha wasiibebe, ni mfano wa punda anaye beba
vitabu vikubwa vikubwa. Mfano muovu mno wa watu walio kadhibisha Ishara za
Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.
|
Ayah 62:6 الأية
قُلْ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ هَادُوا إِن زَعَمْتُمْ أَنَّكُمْ أَوْلِيَاءُ لِلَّهِ
مِن دُونِ النَّاسِ فَتَمَنَّوُا الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ
Qul ya ayyuha allatheenahadoo in zaAAamtum annakum awliyao lillahimin dooni
annasi fatamannawoo almawta in kuntum sadiqeen
Swahili
Sema: Enyi mlio Mayahudi! Ikiwa nyinyi mnadai kuwa ni vipenzi vya Mwenyezi Mungu
pasipo kuwa watu wengine, basi yatamanini mauti, ikiwa mnasema kweli.
|
Ayah 62:7 الأية
وَلَا يَتَمَنَّوْنَهُ أَبَدًا بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيهِمْ ۚ وَاللهُ عَلِيمٌ
بِالظَّالِمِينَ
Wala yatamannawnahu abadan bimaqaddamat aydeehim wallahu AAaleemun biththalimeen
Swahili
Wala hawatayatamani kabisa, kwa sababu ya iliyo kwisha yatanguliza mikono yao.
Na Mwenyezi Mungu anawajua walio dhulumu.
|
Ayah 62:8 الأية
قُلْ إِنَّ الْمَوْتَ الَّذِي تَفِرُّونَ مِنْهُ فَإِنَّهُ مُلَاقِيكُمْ ۖ ثُمَّ
تُرَدُّونَ إِلَىٰ عَالِمِ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ فَيُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ
تَعْمَلُونَ
Qul inna almawta allathee tafirroonaminhu fa-innahu mulaqeekum thumma turaddoona
ila AAalimialghaybi washshahadati fayunabbi-okum bimakuntum taAAmaloon
Swahili
Sema: Hayo mauti mnayo yakimbia, bila ya shaka yatakukuteni. Kisha mtarudishwa
kwa Mwenye kuyajua yaliyo fichikana na yanayo onekana. Hapo atakwambieni mliyo
kuwa mkiyatenda.
|
Ayah 62:9 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ
فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ
إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ
Ya ayyuha allatheena amanooitha noodiya lissalati min yawmialjumuAAati fasAAaw
ila thikri Allahiwatharoo albayAAa thalikum khayrun lakum in kuntumtaAAlamoon
Swahili
Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Sala siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya
Mwenyezi Mungu, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.
|
Ayah 62:10 الأية
فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ
اللهِ وَاذْكُرُوا اللهَ كَثِيرًا لَّعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ
Fa-itha qudiyati assalatufantashiroo fee al-ardi wabtaghoo min fadliAllahi
wathkuroo Allaha katheeranlaAAallakum tuflihoon
Swahili
Na itakapo kwisha Sala, tawanyikeni katika nchi mtafute fadhila za Mwenyezi
Mungu, na mkumbukeni Mwenyezi Mungu kwa wingi ili mpate kufanikiwa.
|
Ayah 62:11 الأية
وَإِذَا رَأَوْا تِجَارَةً أَوْ لَهْوًا انفَضُّوا إِلَيْهَا وَتَرَكُوكَ قَائِمًا
ۚ قُلْ مَا عِندَ اللهِ خَيْرٌ مِّنَ اللهْوِ وَمِنَ التِّجَارَةِ ۚ وَاللهُ
خَيْرُ الرَّازِقِينَ
Wa-itha raaw tijaratan awlahwan infaddoo ilayha watarakooka qa-imanqul ma AAinda
Allahi khayrun mina allahwi wamina attijaratiwallahu khayru arraziqeen
Swahili
Na wanapo iona biashara au pumbao wanayakimbilia hayo na wakakuacha umesimama.
Sema: Yaliyoko kwa Mwenyezi Mungu ni bora kuliko pumbao na biashara. Na Mwenyezi
Mungu ni Mbora wa watoa riziki.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|