1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
إِذَا جَاءَكَ الْمُنَافِقُونَ قَالُوا نَشْهَدُ إِنَّكَ لَرَسُولُ اللهِ ۗ
وَاللهُ يَعْلَمُ إِنَّكَ لَرَسُولُهُ وَاللهُ يَشْهَدُ إِنَّ الْمُنَافِقِينَ
لَكَاذِبُونَ
Itha jaaka almunafiqoonaqaloo nashhadu innaka larasoolu Allahi wallahuyaAAlamu
innaka larasooluhu wallahu yashhadu innaalmunafiqeena lakathiboon
Swahili
Wanapo kujia wanaafiki husema: Tunashuhudia ya kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi
Mungu. Na Mwenyezi Mungu anajua kuwa wewe ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na
Mwenyezi Mungu anashuhudia ya kuwa hakika wanaafiki ni waongo.
|
Ayah 63:2 الأية
اتَّخَذُوا أَيْمَانَهُمْ جُنَّةً فَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللهِ ۚ إِنَّهُمْ سَاءَ
مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ
Ittakhathoo aymanahum junnatanfasaddoo AAan sabeeli Allahi innahum saa makanoo
yaAAmaloon
Swahili
Wamevifanya viapo vyao ni kinga, na wao wakajizuia kuifuata Njia ya Mwenyezi
Mungu. Hakika ni mabaya kabisa waliyo kuwa wakiyafanya.
|
Ayah 63:3 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ آمَنُوا ثُمَّ كَفَرُوا فَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ فَهُمْ
لَا يَفْقَهُونَ
Thalika bi-annahum amanoothumma kafaroo fatubiAAa AAala quloobihim fahum
layafqahoon
Swahili
Hayo ni kwa sababu ya kuwa waliamini, kisha wakakufuru; kwa hivyo umepigwa
muhuri juu ya nyoyo zao. Kwa hivyo hawafahamu lolote.
|
Ayah 63:4 الأية
وَإِذَا رَأَيْتَهُمْ تُعْجِبُكَ أَجْسَامُهُمْ ۖ وَإِن يَقُولُوا تَسْمَعْ
لِقَوْلِهِمْ ۖ كَأَنَّهُمْ خُشُبٌ مُّسَنَّدَةٌ ۖ يَحْسَبُونَ كُلَّ صَيْحَةٍ
عَلَيْهِمْ ۚ هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ ۚ قَاتَلَهُمُ اللهُ ۖ أَنَّىٰ
يُؤْفَكُونَ
Wa-itha raaytahum tuAAjibuka ajsamuhumwa-in yaqooloo tasmaAA liqawlihim
kaannahum khushubunmusannadatun yahsaboona kulla sayhatinAAalayhim humu
alAAaduwwu fahtharhum qatalahumuAllahu anna yu/fakoon
Swahili
Na unapo waona, miili yao inakupendeza, na wakisema, unasikiliza usemi wao.
Lakini wao ni kama magogo yaliyo egemezwa. Wao hudhania kila ukelele unao pigwa
ni kwa ajili yao. Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie
mbali! Vipi wanapotoka na haki?
|
Ayah 63:5 الأية
وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللهِ لَوَّوْا
رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ
Wa-itha qeela lahum taAAalawyastaghfir lakum rasoolu Allahi lawwaw
ruoosahumwaraaytahum yasuddoona wahum mustakbiroon
Swahili
Na wanapo ambiwa: Njooni ili Mtume wa Mwenyezi Mungu akuombeeni maghfira,
huvigeuza vichwa vyao, na unawaona wanageuka nao wamejaa kiburi.
|
Ayah 63:6 الأية
سَوَاءٌ عَلَيْهِمْ أَسْتَغْفَرْتَ لَهُمْ أَمْ لَمْ تَسْتَغْفِرْ لَهُمْ لَن
يَغْفِرَ اللهُ لَهُمْ ۚ إِنَّ اللهَ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الْفَاسِقِينَ
Sawaon AAalayhim astaghfarta lahum amlam tastaghfir lahum lan yaghfira Allahu
lahum inna Allahala yahdee alqawma alfasiqeen
Swahili
Sawa sawa kwao, ukiwatakia maghfira au hukuwatakia maghfira, Mwenyezi Mungu
hatawaghufiria. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.
|
Ayah 63:7 الأية
هُمُ الَّذِينَ يَقُولُونَ لَا تُنفِقُوا عَلَىٰ مَنْ عِندَ رَسُولِ اللهِ
حَتَّىٰ يَنفَضُّوا ۗ وَلِلَّهِ خَزَائِنُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَلَٰكِنَّ
الْمُنَافِقِينَ لَا يَفْقَهُونَ
Humu allatheena yaqooloona latunfiqoo AAala man AAinda rasooli Allahi
hattayanfaddoo walillahi khaza-inu assamawatiwal-ardi walakinna almunafiqeena
layafqahoon
Swahili
Hao ndio wanao sema: Msitoe mali kwa ajili ya walioko kwa Mtume wa Mwenyezi
Mungu, ili waondokelee mbali! Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye khazina za mbingu
na ardhi, lakini wanaafiki hawafahamu.
|
Ayah 63:8 الأية
يَقُولُونَ لَئِن رَّجَعْنَا إِلَى الْمَدِينَةِ لَيُخْرِجَنَّ الْأَعَزُّ مِنْهَا
الْأَذَلَّ ۚ وَلِلَّهِ الْعِزَّةُ وَلِرَسُولِهِ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَلَٰكِنَّ
الْمُنَافِقِينَ لَا يَعْلَمُونَ
Yaqooloona la-in rajaAAna ilaalmadeenati layukhrijanna al-aAAazzu minha
al-athallawalillahi alAAizzatu walirasoolihi walilmu/mineena
walakinnaalmunafiqeena la yaAAlamoon
Swahili
Wanasema: Tukirejea Madina mwenye utukufu zaidi bila ya shaka atamfukuza aliye
mnyonge. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye utukufu - Yeye, na Mtume wake, na
Waumini. Lakini wanaafiki hawajui.
|
Ayah 63:9 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُلْهِكُمْ أَمْوَالُكُمْ وَلَا أَوْلَادُكُمْ
عَن ذِكْرِ اللهِ ۚ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْخَاسِرُونَ
Ya ayyuha allatheena amanoola tulhikum amwalukum wala awladukumAAan thikri
Allahi waman yafAAal thalikafaola-ika humu alkhasiroon
Swahili
Enyi mlio amini! Yasikusahaulisheni mali yenu, wala watoto wenu, kumkumbuka
Mwenyezi Mungu. Na wenye kufanya hayo ndio walio khasiri.
|
Ayah 63:10 الأية
وَأَنفِقُوا مِن مَّا رَزَقْنَاكُم مِّن قَبْلِ أَن يَأْتِيَ أَحَدَكُمُ الْمَوْتُ
فَيَقُولَ رَبِّ لَوْلَا أَخَّرْتَنِي إِلَىٰ أَجَلٍ قَرِيبٍ فَأَصَّدَّقَ وَأَكُن
مِّنَ الصَّالِحِينَ
Waanfiqoo min ma razaqnakummin qabli an ya/tiya ahadakumu almawtu fayaqoola
rabbilawla akhkhartanee ila ajalin qareebin faassaddaqawaakun mina assaliheen
Swahili
Na toeni katika tulicho kupeni kabla hayajamfikia mmoja wenu mauti, tena hapo
akasema: Mola wangu Mlezi! Huniakhirishi muda kidogo nipate kutoa sadaka, na
niwe katika watu wema?
|
Ayah 63:11 الأية
وَلَن يُؤَخِّرَ اللهُ نَفْسًا إِذَا جَاءَ أَجَلُهَا ۚ وَاللهُ خَبِيرٌ بِمَا
تَعْمَلُونَ
Walan yu-akhkhira Allahu nafsan ithajaa ajaluha wallahu khabeerun bimataAAmaloon
Swahili
Wala Mwenyezi Mungu hataiakhirisha nafsi yoyote inapo fika ajali yake; na
Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|