1st Ayah 1 الأية ١الأوليبِسْم ِ اللهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
يُسَبِّحُ لِلَّهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۖ لَهُ الْمُلْكُ
وَلَهُ الْحَمْدُ ۖ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ
Yusabbihu lillahi ma feeassamawati wama fee al-ardilahu almulku walahu alhamdu
wahuwa AAala kullishay-in qadeer
Swahili
Kinamtakasa Mwenyezi Mungu kila kilichomo katika mbingu na katika ardhi. Ufalme
ni wake, na sifa njema ni zake. Na Yeye ni Mwenye uweza juu ya kila kitu.
|
Ayah 64:2 الأية
هُوَ الَّذِي خَلَقَكُمْ فَمِنكُمْ كَافِرٌ وَمِنكُم مُّؤْمِنٌ ۚ وَاللهُ بِمَا
تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ
Huwa allathee khalaqakum faminkum kafirunwaminkum mu/minun wallahu bima
taAAmaloonabaseer
Swahili
Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye
Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda.
|
Ayah 64:3 الأية
خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ
ۖ وَإِلَيْهِ الْمَصِيرُ
Khalaqa assamawati wal-ardabilhaqqi wasawwarakum faahsana suwarakumwa-ilayhi
almaseer
Swahili
Ameziumba mbingu na ardhi kwa haki, na akakupeni sura, na akazifanya nzuri sura
zenu. Na marudio ni kwake.
|
Ayah 64:4 الأية
يَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَيَعْلَمُ مَا تُسِرُّونَ وَمَا
تُعْلِنُونَ ۚ وَاللهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ
YaAAlamu ma fee assamawatiwal-ardi wayaAAlamu ma tusirroona wamatuAAlinoona
wallahu AAaleemun bithati assudoor
Swahili
Anajua viliomo katika mbingu na ardhi, na anajua mnayo yaficha na mnayo
yatangaza. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliomo vifuani.
|
Ayah 64:5 الأية
أَلَمْ يَأْتِكُمْ نَبَأُ الَّذِينَ كَفَرُوا مِن قَبْلُ فَذَاقُوا وَبَالَ
أَمْرِهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ
Alam ya/tikum nabao allatheena kafaroomin qablu fathaqoo wabala amrihim walahum
AAathabunaleem
Swahili
Kwani haikukujieni khabari ya walio kufuru kabla, wakaonja matokeo mabaya ya
mambo yao? Na wao wana adhabu iliyo chungu.
|
Ayah 64:6 الأية
ذَٰلِكَ بِأَنَّهُ كَانَت تَّأْتِيهِمْ رُسُلُهُم بِالْبَيِّنَاتِ فَقَالُوا
أَبَشَرٌ يَهْدُونَنَا فَكَفَرُوا وَتَوَلَّوا ۚ وَّاسْتَغْنَى اللهُ ۚ وَاللهُ
غَنِيٌّ حَمِيدٌ
Thalika bi-annahu kanatta/teehim rusuluhum bilbayyinati faqalooabasharun
yahdoonana fakafaroo watawallaw wastaghnaAllahu wallahu ghaniyyun hameed
Swahili
Hayo ni kwa kuwa walikuwa wakiwajia Mitume wao kwa hoja zilizo wazi, nao
wakasema: Hivyo binaadamu ndio atuongoe? Basi wakakufuru, na wakageuka upande.
Mwenyezi Mungu akawa hana haja nao. Na Mwenyezi Mungu ni Mkwasi, si mhitaji,
naye ni Msifiwa.
|
Ayah 64:7 الأية
زَعَمَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَن لَّن يُبْعَثُوا ۚ قُلْ بَلَىٰ وَرَبِّي
لَتُبْعَثُنَّ ثُمَّ لَتُنَبَّؤُنَّ بِمَا عَمِلْتُمْ ۚ وَذَٰلِكَ عَلَى اللهِ
يَسِيرٌ
ZaAAama allatheena kafaroo an lanyubAAathoo qul bala warabbee latubAAathunna
thummalatunabbaonna bima AAamiltum wathalika AAalaAllahi yaseer
Swahili
Walio kufuru wanadai kuwa hawatafufuliwa. Sema: Kwani? Naapa kwa Mola wangu
Mlezi! Hapana shaka mtafufuliwa, na kisha hapana shaka mtaambiwa mliyo yatenda.
Na hayo ni mepesi kwa Mwenyezi Mungu.
|
Ayah 64:8 الأية
فَآمِنُوا بِاللهِ وَرَسُولِهِ وَالنُّورِ الَّذِي أَنزَلْنَا ۚ وَاللهُ بِمَا
تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ
Faaminoo billahiwarasoolihi wannoori allathee anzalna wallahubima taAAmaloona
khabeer
Swahili
Basi muaminini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na Nuru tuliyo iteremsha. Na
Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayo yatenda.
|
Ayah 64:9 الأية
يَوْمَ يَجْمَعُكُمْ لِيَوْمِ الْجَمْعِ ۖ ذَٰلِكَ يَوْمُ التَّغَابُنِ ۗ وَمَن
يُؤْمِن بِاللهِ وَيَعْمَلْ صَالِحًا يُكَفِّرْ عَنْهُ سَيِّئَاتِهِ وَيُدْخِلْهُ
جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ ذَٰلِكَ
الْفَوْزُ الْعَظِيمُ
Yawma yajmaAAukum liyawmi aljamAAi thalikayawmu attaghabuni waman yu/min
billahiwayaAAmal salihan yukaffir AAanhu sayyi-atihiwayudkhilhu jannatin tajree
min tahtihaal-anharu khalideena feeha abadan thalikaalfawzu alAAatheem
Swahili
Siku atakayo kukusanyeni kwa ajili ya Siku ya Mkusanyiko; hiyo ni siku ya
kupunjana. Na anaye muamini Mwenyezi Mungu na akatenda mema, atamfutia maovu
yake, na atamuingiza katika Mabustani yenye kupitiwa kati yake na mito, watadumu
humo milele. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
|
Ayah 64:10 الأية
وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ
خَالِدِينَ فِيهَا ۖ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ
Wallatheena kafaroo wakaththaboobi-ayatina ola-ika as-habuannari khalideena
feeha wabi/sa almaseer
Swahili
Na walio kufuru na wakakadhibisha Ishara zetu, hao ni watu wa Motoni, watadumu
humo milele. Na hayo ndiyo marudio mabaya.
|
Ayah 64:11 الأية
مَا أَصَابَ مِن مُّصِيبَةٍ إِلَّا بِإِذْنِ اللهِ ۗ وَمَن يُؤْمِن بِاللهِ
يَهْدِ قَلْبَهُ ۚ وَاللهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ
Ma asaba min museebatinilla bi-ithni Allahi waman yu/min billahiyahdi qalbahu
wallahu bikulli shay-in AAaleem
Swahili
Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Na mwenye kumuamini
Mwenyezi Mungu huuongoa moyo wake. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu.
|
Ayah 64:12 الأية
وَأَطِيعُوا اللهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ ۚ فَإِن تَوَلَّيْتُمْ فَإِنَّمَا
عَلَىٰ رَسُولِنَا الْبَلَاغُ الْمُبِينُ
WaateeAAoo Allaha waateeAAooarrasoola fa-in tawallaytum fa-innama AAalarasoolina
albalaghu almubeen
Swahili
Na mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume. Mkigeuka, basi hakika juu ya Mtume
wetu ni kufikisha (Ujumbe wake) kwa uwazi tu.
|
Ayah 64:13 الأية
اللهُ لَا إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ۚ وَعَلَى اللهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ
Allahu la ilaha illahuwa waAAala Allahi falyatawakkali almu/minoon
Swahili
Mwenyezi Mungu, hapana mungu isipo kuwa Yeye. Na juu ya Mwenyezi Mungu
nawategemee Waumini.
|
Ayah 64:14 الأية
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ مِنْ أَزْوَاجِكُمْ وَأَوْلَادِكُمْ عَدُوًّا
لَّكُمْ فَاحْذَرُوهُمْ ۚ وَإِن تَعْفُوا وَتَصْفَحُوا وَتَغْفِرُوا فَإِنَّ
اللهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Ya ayyuha allatheena amanooinna min azwajikum waawladikum AAaduwwan lakum
fahtharoohumwa-in taAAfoo watasfahoo wataghfiroo fa-inna Allahaghafoorun raheem
Swahili
Enyi mlio amini! Hakika miongoni mwa wake zenu na watoto wenu wamo maadui zenu.
Basi tahadharini nao. Na mkisamehe, na mkapuuza, na mkaghufiria basi hakika
Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, Mwenye kurehemu.
|
Ayah 64:15 الأية
إِنَّمَا أَمْوَالُكُمْ وَأَوْلَادُكُمْ فِتْنَةٌ ۚ وَاللهُ عِندَهُ أَجْرٌ
عَظِيمٌ
Innama amwalukum waawladukumfitnatun wallahu AAindahu ajrun AAatheem
Swahili
Hakika mali yenu na watoto wenu ni jaribio. Na kwa Mwenyezi Mungu upo ujira
mkubwa.
|
Ayah 64:16 الأية
فَاتَّقُوا اللهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ وَاسْمَعُوا وَأَطِيعُوا وَأَنفِقُوا خَيْرًا
لِّأَنفُسِكُمْ ۗ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ
Fattaqoo Allaha maistataAAtum wasmaAAoo waateeAAoo waanfiqookhayran li-anfusikum
waman yooqa shuhha nafsihi faola-ikahumu almuflihoon
Swahili
Basi mcheni Mwenyezi Mungu kama mwezavyo, na sikieni, na t'iini, na toeni,
itakuwa kheri kwa nafsi zenu. Na mwenye kuepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi
hao ndio walio fanikiwa.
|
Ayah 64:17 الأية
إِن تُقْرِضُوا اللهَ قَرْضًا حَسَنًا يُضَاعِفْهُ لَكُمْ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ۚ
وَاللهُ شَكُورٌ حَلِيمٌ
In tuqridoo Allaha qardanhasanan yudaAAifhu lakum wayaghfir lakum
wallahushakoorun haleem
Swahili
Mkimkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mzuri, atakuzidishieni mardufu, na
atakusameheni. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa shukra, Mpole.
|
Ayah 64:18 الأية
عَالِمُ الْغَيْبِ وَالشَّهَادَةِ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ
AAalimu alghaybi washshahadatialAAazeezu alhakeem
Swahili
Mwenye kujua siri na dhaahiri, Mwenye nguvu, Mwenye hikima.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|