Basi alipo fika ilinadiwa: Amebarikiwa aliomo katika moto huu na walioko
pembezoni mwake. Na ametakasika Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Na ingiza mkono wako katika mfuko wako, utatoka mweupe bila ya maradhi. Ni
katika Ishara tisa za kumpelekea Firauni na kaumu yake. Hakika hao walikuwa watu
waovu.
Na hakika tuliwapa Daudi na Sulaiman ilimu, na wakasema: Alhamdu Lillahi,
Kuhimidiwa kote ni kwa Mwenyezi Mungu aliye tufadhilisha kuliko wengi katika
waja wake Waumini.
Mpaka walipo fika kwenye bonde la wadudu chungu, alisema mdudu chungu mmoja:
Enyi wadudu chungu! Ingieni majumbani mwenu, asikupondeni Sulaiman na majeshi
yake bila ya wao kutambua.
Basi (Sulaiman) akatabasamu akacheka kwa neno hili, na akasema: Ee Mola wangu
Mlezi! Nizindue niishukuru neema yako uliyo nineemesha mimi na wazazi wangu, na
nipate kutenda mema uyapendayo, na uniingize kwa rehema yako katika waja wako
wema.
Nimemkuta yeye na watu wake wanalisujudia jua badala ya Mwenyezi Mungu; na
Shet'ani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia Njia. Kwa hivyo hawakuongoka,
Basi alipo fika (mjumbe) kwa Sulaiman, alisema (Sulaiman): Hivyo ndio nyinyi
mnanisaidia kwa mali? Aliyo nipa Mwenyezi Mungu ni bora zaidi kuliko aliyo
kupeni nyinyi. Lakini nyinyi mnafurahia hii zawadi yenu.
Akasema mwenye ilimu ya Kitabu: Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako.
Basi alipo kiona kimewekwa mbele yake, akasema: Haya ni katika fadhila zake Mola
wangu Mlezi, ili anijaribu nitashukuru au nitakufuru. Na mwenye kushukuru, kwa
hakika, anashukuru kwa manufaa ya nafsi yake; na anaye kufuru, kwa hakika Mola
wangu Mlezi ni Mkwasi na Karimu.
Basi (Malkia) alipo fika akaambiwa: Je! Kiti chako cha enzi ni kama hiki?
Akasema: Kama kwamba ndicho hichi. (Sulaiman na watu wake wakasema): Na sisi
tumepewa ilimu kabla yake (Malkia), na tukawa Waislamu.
Akaambiwa: Liingie behewa la hili jumba. Alipo liona alidhani ni maji, na
akapandisha nguo mpaka kwenye miundi yake. (Sulaiman) akasema: Hakika hilo ni
behewa lilio sakafiwa kwa viyoo! Akasema (Malkia): Mola wangu Mlezi! Mimi
nimejidhulumu nafsi yangu, na sasa nanyenyekea pamoja na Sulaiman kwa Mwenyezi
Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote.
Wakasema: Tuna kisirani nawe na wale walio pamoja nawe. Yeye akasema: Uaguzi wa
ukorofi wenu uko kwa Mwenyezi Mungu; lakini nyinyi ni watu mnao jaribiwa.
Wakasema: Apishaneni kwa Mwenyezi Mungu tutamshambulia usiku yeye na ahali zake;
kisha tutamwambia mrithi wake: Sisi hatukuona maangamizo ya watu wake, na sisi
bila ya shaka tunasema kweli.
Sema: Alhamdu Lillahi! Kuhimidiwa ni kwa Mwenyezi Mungu! Na amani ishuke juu ya
waja wake alio wateuwa. Je! Mwenyezi Mungu ni bora, au wale wanao washirikisha
naye?
AU NANI yule aliye ziumba mbingu na ardhi, na akakuteremshieni maji kutoka
mbinguni, na kwa hayo tukaziotesha bustani zenye kupendeza? Nyinyi hamna uwezo
wa kuiotesha miti yake. Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali hao ni
watu walio potoka.
Au nani yule aliye ifanya ardhi mahali pa kutua, na akajaalia ndani yake mito,
na akaweka milima? Na akaweka baina ya bahari mbili kiziwizi? Je! Yupo mungu
pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali wengi wao hawajui.
Au nani yule anaye mjibu mwenye shida pale anapo mwomba, na akaiondoa dhiki, na
akakufanyeni warithi wa ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Ni
machache mnayo yazingatia.
Au nani yule anaye kuongoeni katika giza la bara na bahari, na akazipeleka pepo
kuleta bishara kabla ya rehema zake? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu?
Ametukuka Mwenyezi Mungu juu ya wanao washirikisha naye.
Au nani anaye uanzisha uumbaji, kisha akaurejesha? Na nani anaye kuruzukuni
kutoka mbinguni na kwenye ardhi? Je! Yupo mungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Sema:
Leteni hoja zenu kama nyinyi ni wasema kweli.
Na unaiona milima unaidhunia imetulia; nayo inakwenda kama mwendo wa mawingu.
Huo ndio ufundi wa Mwenyezi Mungu aliye tengeneza vilivyo kila kitu. Hakika Yeye
anazo khabari za yote myatendayo.
Ama mimi nimeamrishwa nimuabudu Mola Mlezi wa mji huu aliye ufanya ni mtakatifu;
na ni vyake Yeye tu vitu vyote. Na nimeamrishwa niwe miongoni mwa Waislamu,
wenye kunyenyekea.
Na sema: Alhamdu Lillahi, Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu. Yeye
atakuonyesheni Ishara zake, na mtazijua. Na Mola wako Mlezi si mwenye
kughafilika na myatendayo.