First Ayah 1 الأية الأوليبِسْم ِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
وَالذَّارِيَاتِ ذَرْوًا
Swahili
Naapa kwa pepo zinazo tawanya,
|
Ayah 51:2 الأية
فَالْحَامِلَاتِ وِقْرًا
Swahili
Na zinazo beba mizigo,
|
Ayah 51:3 الأية
فَالْجَارِيَاتِ يُسْرًا
Swahili
Na zinazo kwenda kwa wepesi.
|
Ayah 51:4 الأية
فَالْمُقَسِّمَاتِ أَمْرًا
Swahili
Na zinazo gawanya kwa amri,
|
Ayah 51:5 الأية
إِنَّمَا تُوعَدُونَ لَصَادِقٌ
Swahili
Hakika mnayo ahidiwa bila ya shaka ni kweli,
|
Ayah 51:6 الأية
وَإِنَّ الدِّينَ لَوَاقِعٌ
Swahili
Na kwa hakika malipo bila ya shaka yatatokea.
|
Ayah 51:7 الأية
وَالسَّمَاءِ ذَاتِ الْحُبُكِ
Swahili
Naapa kwa mbingu zenye njia,
|
Ayah 51:8 الأية
إِنَّكُمْ لَفِي قَوْلٍ مُّخْتَلِفٍ
Swahili
Hakika nyinyi bila ya shaka mmo katika kauli inayo khitalifiana.
|
Ayah 51:9 الأية
يُؤْفَكُ عَنْهُ مَنْ أُفِكَ
Swahili
Anageuzwa kutokana na haki mwenye kugeuzwa.
|
Ayah 51:10 الأية
قُتِلَ الْخَرَّاصُونَ
Swahili
Wazushi wameangamizwa.
|
Ayah 51:11 الأية
الَّذِينَ هُمْ فِي غَمْرَةٍ سَاهُونَ
Swahili
Ambao wameghafilika katika ujinga.
|
Ayah 51:12 الأية
يَسْأَلُونَ أَيَّانَ يَوْمُ الدِّينِ
Swahili
Wanauliza: Ni lini hiyo siku ya malipo?
|
Ayah 51:13 الأية
يَوْمَ هُمْ عَلَى النَّارِ يُفْتَنُونَ
Swahili
Hiyo ni siku watakayo adhibiwa Motoni.
|
Ayah 51:14 الأية
ذُوقُوا فِتْنَتَكُمْ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تَسْتَعْجِلُونَ
Swahili
Onjeni adhabu yenu! Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyahimiza.
|
Ayah 51:15 الأية
إِنَّ الْمُتَّقِينَ فِي جَنَّاتٍ وَعُيُونٍ
Swahili
Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
|
Ayah 51:16 الأية
آخِذِينَ مَا آتَاهُمْ رَبُّهُمْ ۚ إِنَّهُمْ كَانُوا قَبْلَ ذَٰلِكَ مُحْسِنِينَ
Swahili
Wanapokea aliyo wapa Mola wao Mlezi. Kwa hakika hao walikuwa kabla ya haya
wakifanya mema.
|
Ayah 51:17 الأية
كَانُوا قَلِيلًا مِّنَ اللَّيْلِ مَا يَهْجَعُونَ
Swahili
Walikuwa wakilala kidogo tu usiku.
|
Ayah 51:18 الأية
وَبِالْأَسْحَارِ هُمْ يَسْتَغْفِرُونَ
Swahili
Na kabla ya alfajiri wakiomba maghfira.
|
Ayah 51:19 الأية
وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ
Swahili
Na katika mali yao ipo haki ya mwenye kuomba na asiye omba.
|
Ayah 51:20 الأية
وَفِي الْأَرْضِ آيَاتٌ لِّلْمُوقِنِينَ
Swahili
Na katika ardhi zipo Ishara kwa wenye yakini.
|
Ayah 51:21 الأية
وَفِي أَنفُسِكُمْ ۚ أَفَلَا تُبْصِرُونَ
Swahili
Na pia katika nafsi zenu - Je! Hamwoni?
|
Ayah 51:22 الأية
وَفِي السَّمَاءِ رِزْقُكُمْ وَمَا تُوعَدُونَ
Swahili
Na katika mbingu ziko riziki zenu na mliyo ahidiwa.
|
Ayah 51:23 الأية
فَوَرَبِّ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ إِنَّهُ لَحَقٌّ مِّثْلَ مَا أَنَّكُمْ
تَنطِقُونَ
Swahili
Basi naapa kwa Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, hakika haya ni kweli kama ilivyo
kweli kuwa nyinyi mnasema.
|
Ayah 51:24 الأية
هَلْ أَتَاكَ حَدِيثُ ضَيْفِ إِبْرَاهِيمَ الْمُكْرَمِينَ
Swahili
Je! Imekufikia hadithi ya wageni wa Ibrahim wanao hishimiwa?
|
Ayah 51:25 الأية
إِذْ دَخَلُوا عَلَيْهِ فَقَالُوا سَلَامًا ۖ قَالَ سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ
Swahili
Walipo ingia kwake wakasema: Salama! Na yeye akasema: Salama! Nyinyi ni watu
nisio kujueni.
|
Ayah 51:26 الأية
فَرَاغَ إِلَىٰ أَهْلِهِ فَجَاءَ بِعِجْلٍ سَمِينٍ
Swahili
Akenda kwa ahali yake na akaja na ndama aliye nona.
|
Ayah 51:27 الأية
فَقَرَّبَهُ إِلَيْهِمْ قَالَ أَلَا تَأْكُلُونَ
Swahili
Akawakaribisha, akasema: Mbona hamli?
|
Ayah 51:28 الأية
فَأَوْجَسَ مِنْهُمْ خِيفَةً ۖ قَالُوا لَا تَخَفْ ۖ وَبَشَّرُوهُ بِغُلَامٍ
عَلِيمٍ
Swahili
Akahisi kuwaogopa katika nafsi yake. Wakasema: Usiwe na khofu, nao wakambashiria
kupata kijana mwenye ilimu.
|
Ayah 51:29 الأية
فَأَقْبَلَتِ امْرَأَتُهُ فِي صَرَّةٍ فَصَكَّتْ وَجْهَهَا وَقَالَتْ عَجُوزٌ
عَقِيمٌ
Swahili
Ndipo mkewe akawaelekea, na huku anasema na akijipiga usoni kwa mastaajabu, na
kusema: Mimi ni kikongwe na tasa!
|
Ayah 51:30 الأية
قَالُوا كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ ۖ إِنَّهُ هُوَ الْحَكِيمُ الْعَلِيمُ
Swahili
Wakasema: Ndivyo vivyo hivyo alivyo sema Mola wako Mlezi. Hakika Yeye ni Mwenye
hikima na Mwenye kujua.
|
Ayah 51:31 الأية
قَالَ فَمَا خَطْبُكُمْ أَيُّهَا الْمُرْسَلُونَ
Swahili
AKASEMA: Basi ujumbe wenu ni nini, enyi mlio tumwa?
|
Ayah 51:32 الأية
قَالُوا إِنَّا أُرْسِلْنَا إِلَىٰ قَوْمٍ مُّجْرِمِينَ
Swahili
Wakasema: Hakika sisi tumetumwa kwa watu wakosefu,
|
Ayah 51:33 الأية
لِنُرْسِلَ عَلَيْهِمْ حِجَارَةً مِّن طِينٍ
Swahili
Tuwatupie mawe ya udongo,
|
Ayah 51:34 الأية
مُّسَوَّمَةً عِندَ رَبِّكَ لِلْمُسْرِفِينَ
Swahili
Yaliyo tiwa alama kutoka kwa Mola wako Mlezi kwa ajili ya wanao pindukia mipaka.
|
Ayah 51:35 الأية
فَأَخْرَجْنَا مَن كَانَ فِيهَا مِنَ الْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Kwa hivyo tutawatoa katika hao wale walio amini.
|
Ayah 51:36 الأية
فَمَا وَجَدْنَا فِيهَا غَيْرَ بَيْتٍ مِّنَ الْمُسْلِمِينَ
Swahili
Lakini hatukupata humo ila nyumba moja tu yenye Waislamu!
|
Ayah 51:37 الأية
وَتَرَكْنَا فِيهَا آيَةً لِّلَّذِينَ يَخَافُونَ الْعَذَابَ الْأَلِيمَ
Swahili
Na tukaacha humo Ishara kwa ajili ya wanao iogopa adhabu chungu.
|
Ayah 51:38 الأية
وَفِي مُوسَىٰ إِذْ أَرْسَلْنَاهُ إِلَىٰ فِرْعَوْنَ بِسُلْطَانٍ مُّبِينٍ
Swahili
Na katika khabari za Musa, tulipo mtuma kwa Firauni na hoja wazi.
|
Ayah 51:39 الأية
فَتَوَلَّىٰ بِرُكْنِهِ وَقَالَ سَاحِرٌ أَوْ مَجْنُونٌ
Swahili
Lakini alipuuza kwa sababu ya nguvu zake na akasema: Huyu ni mchawi au
mwendawazimu!
|
Ayah 51:40 الأية
فَأَخَذْنَاهُ وَجُنُودَهُ فَنَبَذْنَاهُمْ فِي الْيَمِّ وَهُوَ مُلِيمٌ
Swahili
Basi tukamkamata yeye na majeshi yake na tukawatupa baharini, na yeye ndiye wa
kulaumiwa.
|
Ayah 51:41 الأية
وَفِي عَادٍ إِذْ أَرْسَلْنَا عَلَيْهِمُ الرِّيحَ الْعَقِيمَ
Swahili
Na katika khabari za A'di tulipo wapelekea upepo wa kukata uzazi.
|
Ayah 51:42 الأية
مَا تَذَرُ مِن شَيْءٍ أَتَتْ عَلَيْهِ إِلَّا جَعَلَتْهُ كَالرَّمِيمِ
Swahili
Haukuacha chochote ulicho kifikia ila ulikifanya kama kilio nyambuka.
|
Ayah 51:43 الأية
وَفِي ثَمُودَ إِذْ قِيلَ لَهُمْ تَمَتَّعُوا حَتَّىٰ حِينٍ
Swahili
Na katika khabari za Thamudi walipo ambiwa: Jifurahisheni kwa muda mdogo tu.
|
Ayah 51:44 الأية
فَعَتَوْا عَنْ أَمْرِ رَبِّهِمْ فَأَخَذَتْهُمُ الصَّاعِقَةُ وَهُمْ يَنظُرُونَ
Swahili
Wakaasi amri ya Mola wao Mlezi. Basi uliwanyakua moto wa radi nao wanaona.
|
Ayah 51:45 الأية
فَمَا اسْتَطَاعُوا مِن قِيَامٍ وَمَا كَانُوا مُنتَصِرِينَ
Swahili
Basi hawakuweza kusimama wala hawakuwa wenye kujitetea.
|
Ayah 51:46 الأية
وَقَوْمَ نُوحٍ مِّن قَبْلُ ۖ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمًا فَاسِقِينَ
Swahili
Na kaumu ya Nuhu hapo mbele. Hakika hao walikuwa watu wapotovu.
|
Ayah 51:47 الأية
وَالسَّمَاءَ بَنَيْنَاهَا بِأَيْدٍ وَإِنَّا لَمُوسِعُونَ
Swahili
Na mbingu tumezifanya kwa nguvu na uwezo na hakika Sisi bila ya shaka ndio
twenye uwezo wa kuzitanua.
|
Ayah 51:48 الأية
وَالْأَرْضَ فَرَشْنَاهَا فَنِعْمَ الْمَاهِدُونَ
Swahili
Na ardhi tumeitandaza; basi watandazaji wazuri namna gani Sisi!
|
Ayah 51:49 الأية
وَمِن كُلِّ شَيْءٍ خَلَقْنَا زَوْجَيْنِ لَعَلَّكُمْ تَذَكَّرُونَ
Swahili
Na katika kila kitu tumeumba kwa jozi ili mzingatie.
|
Ayah 51:50 الأية
فَفِرُّوا إِلَى اللَّهِ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ مُّبِينٌ
Swahili
Basi kimbilieni kwa Mwenyezi Mungu, hakika mimi ni mwonyaji kwenu wa kubainisha
nitokae kwake.
|
Ayah 51:51 الأية
وَلَا تَجْعَلُوا مَعَ اللَّهِ إِلَٰهًا آخَرَ ۖ إِنِّي لَكُم مِّنْهُ نَذِيرٌ
مُّبِينٌ
Swahili
Wala msifanye kuwa kuna mungu mwengine pamoja na Mwenyezi Mungu. Hakika mimi ni
mwonyaji kwenu wa kubainisha nitokae kwake.
|
Ayah 51:52 الأية
كَذَٰلِكَ مَا أَتَى الَّذِينَ مِن قَبْلِهِم مِّن رَّسُولٍ إِلَّا قَالُوا سَاحِرٌ
أَوْ مَجْنُونٌ
Swahili
Basi ndio hivyo hivyo, hakuwajia kabla yao Mtume ila walisema: Huyu ni mchawi au
mwendawazimu.
|
Ayah 51:53 الأية
أَتَوَاصَوْا بِهِ ۚ بَلْ هُمْ قَوْمٌ طَاغُونَ
Swahili
Je! Wameambizana kwa haya? Bali hawa ni watu waasi.
|
Ayah 51:54 الأية
فَتَوَلَّ عَنْهُمْ فَمَا أَنتَ بِمَلُومٍ
Swahili
Basi waachilie mbali, nawe hulaumiwi.
|
Ayah 51:55 الأية
وَذَكِّرْ فَإِنَّ الذِّكْرَىٰ تَنفَعُ الْمُؤْمِنِينَ
Swahili
Na kumbusha, kwani ukumbusho huwafaa Waumini.
|
Ayah 51:56 الأية
وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ
Swahili
Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi.
|
Ayah 51:57 الأية
مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ
Swahili
Na sitaki kwao riziki, wala sitaki wanilishe.
|
Ayah 51:58 الأية
إِنَّ اللَّهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ
Swahili
Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti.
|
Ayah 51:59 الأية
فَإِنَّ لِلَّذِينَ ظَلَمُوا ذَنُوبًا مِّثْلَ ذَنُوبِ أَصْحَابِهِمْ فَلَا
يَسْتَعْجِلُونِ
Swahili
Hakika walio dhulumu wana fungu lao la adhabu kama fungu la wenzao. Basi
wasinihimize.
|
Ayah 51:60 الأية
فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ كَفَرُوا مِن يَوْمِهِمُ الَّذِي يُوعَدُونَ
Swahili
Ole wao walio ikanusha siku yao waliyo ahidiwa.
|
©
EsinIslam.Com Designed & produced by The Awqaf London. Please pray for us
|